Fahamu programu yenye akili bandia inayoweza kusaidia kubaini magonjwa ya ngozi

Kampuni ya mawasiliano ya Google imezindua programu inayotumia akili bandia kusaidia kubaini ugonjwa wa ngozi, hali ya nywele na kucha kwa kuzingatia picha zilizowekwa na wateja.

Majaribio ya programu hiyo inayofahamika kama "dermatology assist tool", iliyozinduliwa katika mkutano wa wabunifu wa kila mwaka, itatambuliwa rasmi baadaye mwaka huu, kampuni hiyo imesema.

Programu hiyo imeruhusiwa kutumika kama programu ya matibabu barani Ulaya.

Mtaalamu wa ugonjwa wa saratani amesema programu hiyo ya kisasa zaidi itawezesha madaktari kutoa tiba stahiki kwa wagonjwa.

Programu hiyo yenye akili bandia inaweza kutambua magonjwa 288 ya ngozi lakini haikubuniwa kuwa mbadala wa utambuzi wa magonjwa na tiba yake, kampuni ya Google imesema.

Imechukua miaka mitatu kuunda programu hiyo na imewezeshwa kutambua data za picha 65,000 za magonjwa mbalimbali ya ngozi pamoja na mamilioni ya picha zinazoonesha alama ambazo watu walikuwa na wasiwasi nazo pamoja na maelfu ya picha ya ngozi zilizo salama.

Pamoja na kutumia picha hizo, programu hiyo pia inahitaji wagonjwa kujibu maswali kadhaa mtandaoni.

Pia imezingatia programu za awali zilizobuniwa na kampuni hiyo za kubaini dalili za aina fulani za saratani na ugonjwa wa kifua kifuu.

Kwa sasa hakuna kati ya programu hizo ambayo imeidhinishwa kama mbadala wa kutambua magonjwa ya binadamu.

Google imesema kuna utafutaji wa suala la ngozi, nywele na kucha bilioni 10 katika mtandao wake kila mwaka.

Programu hiyo bado haijaidhinishwa na Shirika la Marekani la Usimamizi wa Chakula na Dawa, lakini programu moja ya kujifunza iliyoundwa na kampuni ya Uingereza hivi karibuni iliidhinishwa na shirika hilo kama msaidizi wa utambuzi wa magonjwa ya saratani ya mapafu.

Profesa Tim Underwood, mkuu wa sayansi ya saratani chuo kikuu cha Southampton, amesema programu kama hizo zina uwezo wa kutoa tiba muafaka kwa wagonjwa.

"Programu zinazotumia akili bandia katika magonjwa ya saratani na nyanja zingine za tiba, huwa zinasaidia katika utambuzi wa ugonjwa na tiba inayoweza kutolewa kwa mgonjwa," amesema.

Uchambuzi

Hii sio mara ya kwanza programu inayotumia akili bandia inazinduliwa lakini ni muhimu kwasababu watu watakuwa na uwezo wa kuitumia wala sio madaktari.

Google inachukulia programu hiyo kama iliyo bora zaidi ikilinganishwa na kujitafutia taarifa wewe mwenyewe, lakini sio kwamba ni mbadala wa ushauri wa tiba.

Pia tunajua kuwa intaneti ni chanzo cha kuzua wasiwasi mwingi katika masuala ya tiba na taarifa za uwongo. Sasa basi, jinsi watu watakavyotumia programu yenyewe imetengenezwa kwa muundo unatoa kipaumbele katika usalama.

Pia katika programu kama hizi, kinachoangaliwa, unazinagtia kuvutia kila mmoja mwenye ugonjwa huo au kuondoa wale wenye afya zao ili kuepuka wasiwasi usio na msingi?