Mzozo wa Ukraine: Kipi tunachokojua kuhusu vifaru 200 vya T-72 vya Poland vilivyotumwa kwenda Ukraine?

Kama sehemu ya usaidizi wa kijeshi, Poland imehamisha vifaru 200 vya T-72 na dazeni kadhaa za magari ya kivita ya BMP-1 hadi Ukraine, na jumla ya usaidizi wa kijeshi wa Poland umezidi zloty bilioni saba (dola bilioni 1.5), inaripoti Redio ya Poland.

Kutumwa kwa vifaru hivyo kulithibitishwa rasmi huko Warsaw.

"Sitakupa takwimu maalum, lakini ninaweza kuthibitisha maneno ya Waziri Mkuu ambayo Poland imetoa, inasambaza na itaendelea kuipatia Ukraine msaada wa kijeshi, haswa vifaru vya ya T-72.

''Nisingependa kuzungumzia kwa undani, lakini huu, bila shaka, ni msaada muhimu,'' Pawel Soloch, mkuu wa Ofisi ya Usalama wa Kitaifa ya Poland, aliiambia Polsat News.

Vyombo vya habari vya Poland pia vimeandika kwamba kati ya silaha ambazo Warszawa ilikabidhi kwa Kyiv ni '2S1 Gvozdika' ndege zinazojiendesha zenyewe na mifumo mingi ya roketi ya Grad, pamoja na makombora ya kurushwa juu ya anga hadi sehemu nyingine ya anga kwa ndege za MiG-29 na Su-27.

Redio ya Poland inaongeza kuwa Ukraine pia itapokea ndege zisizo na rubani kutoka kwa WB Electronics, roketi aina ya 'Piorun' inayoweza kubebeka na binadamu yenye mifumo ya ulinzi wa anga na kiasi kikubwa cha risasi.

Wataalamu wa kundi la Oryx, ambalo linachambua data juu ya silaha kutoka vyanzo vya wazi, pia waliripoti juu ya usambazaji wa vifaa kwa Ukraine kutoka Poland.

Ni nini kinachojulikana kuhusu kutumika kwa vifaru vya T-72

Kifaru kikubwa zaidi cha vita aina ya T-72 ilitengenezwa huko Uralvagonzavod wakati wa enzi ya Soviet.

Jeshi la Soviet lilipitisha na kunza kukitumia mwaka wa 1973.

Kwa miaka 30 ya uzalishaji, kimeboreshwa mara 14.

Kifaru cha T-72 kilishiriki katika migogoro mingi ya kijeshi - katika vita vya Lebanon na Syria, katika vita vya Iraq na Iran, katika migogoro baada ya kuanguka kwa Yugoslavia, huko Chechnya, katika vita vya Urusi na Georgia mwaka 2008, katika vita vya Nagorno-Karabakh na katika vita vya mashariki mwa Ukraine.

Mwanzoni mwa 2014, vikosi vya jeshi vya Ukraine vilikuwa na vifaru 600 ya T-72 kwenye hifadhi.

Lakini kwa kuzuka kwa uhasama huko Donbass, Wizara ya Ulinzi ilianza tena matumizi ya vifaru hivyo.

Vifaru hivyo vilibadilishwa na kuwa vya kisasa na moja ya kampuni ya utengezaji zana za kivita ya Ukraine.

Vifaru vya T-72 viliwekwa injini yenye nguvu zaidi (840 hp), ikilinganishwa na vifaru T-80, ulinzi ulioboreshwa, kituo cha redio cha kisasa cha dijitali na mfumo wa satelaiti.

Vifaru vya kuona usiku viliwekwa mirija ya kuboresha picha ya kizazi cha tatu.

Marekebisho anuwai ya vifaru vya T-72 pia hutumiwa kikamilifu katika uvamizi wa Ukraine vya mwaka 2022 na jeshi la Urusi.

Vifaru vya washirika

Na kuanza kwa uvamizi wa Urusi mnamo Februari 24, Ukraine iligeukia washirika kwa msaada.

Mapema mwezi wa Aprili, The New York Times, ikitoa mfano wa afisa wa Marekani ambaye hakutajwa jina, iliripoti kwamba Marekani ilikuwa ikijadiliana na washirika wa NATO juu ya uwezekano wa uhamisho wa vifaru vilivyotengenezwa wakati wa Usovieti kwa Ukraine.

Vifaru vya kwanza vya T-72, BMP-1 na howitzer vilianza kuhamishiwa Ukraine, Jamhuri ya Czech.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa kundi la kwanza lilijumuisha vifaru zaidi ya dazeni.

Kulingana na Redio ya huko, Poland ina karibu vifaru 400 vya T-72.

Kulingana na uamuzi wa Wizara ya Ulinzi ya Poland, mnamo mwaka 2019 baadhi yao yalibadilishwa, lakini, kama maelezo ya uchapishaji, jeshi la Ukraine lilihamishwa haswa vifaa visivyo vya kisasa.

Marekani pia ilikubali kuhamisha mifumo ya makombora ya kuzuia ndege ya S-300 kutoka kwa maghala ya silaha ya nchi za Ulaya Mashariki hadi Ukraine.

Slovakia tayari imewasilisha rasmi suala lenye utata kama hilo.

Kabla ya kuanza kwa uvamizi wa Urusi na katika hatua zake za awali, nchi za NATO zilikwepa kuipatia Ukraine silaha ambazo zinachukuliwa kuwa za kukera, zikiogopa kwamba hii ingeipa Urusi sababu za kuzungumzia mzozo huo wa moja kwa moja na muungano huo.

Lakini baada ya kushuhudia ukatili huko Bucha na miji mingine inayokaliwa na Urusi, msimamo wa nchi za Magharibi ulibadilika.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema kuwa umoja huo hausambazi tena silaha zinazotolewa kwa Kyiv kama njia ya kujihami na kutaka kufanya mashambulizi.