Ushauri wa maombi ya kazi: "Nilipata kazi ya ndoto yangu baada ya maombi 400 na mahojiano ya kazi 25 "

Mwezi Machi 2020, wakati Ruth Ozavize Ossai , alipohamia nchini Uingereza, hakudhani kuwa angehitaji kutuma maombi 400 ya kazi ndio apate kazi ya iliyokuwa ndoto yake.

Ruth, ambaye ni Mnigeria , alisoma uhandisi wa kemia katika Chuo kikuu cha Oyo kilichopo katika jimbo la kusini mwa nchi hiyo la Akwa Ibom slakini baadaye alibadilisha taaluma yake yake na kuwa ya afya na usalama.

Mama huyu mwenye umri wa miaka 30 aliiambia BBC jinsi alivyoendelea kutuma maombi ya kazi na bila kukata tamaa.

Mwezi Juni 2020, Ruth [kwanza alikubali dkazi iliyo nje ya taaluma yake kutokana na kukata tamaa, lakini hilo halikumzuwia kuendelea kutuma maombi ya kazi . Juhudi zake za bila kukoma hatimaye zilizaa matunda wakati Ruth alipopata kazi iliyokuwa ndoto yake katika taasisi ya huduma za afya ta DHU baada ya maombi ta kazi 400 na kufanya mahojiano ya kazi 400

"Ni maombi niliyoyatuma katika mwaka 2021 ambapo niliyahesabu, sijaongeza yale ambayo niliyatuma katika mwaka 2020 ," Ruth aliiambia idhaa ya BBC Pidgin.

"Kila siku, Jumatatu hadi Ijumaa, Niliendelea kutuma maombi ya kazi, nikiwasilisha maombi 10 hadi 15 kila siku."

"Wakati mume wangu aliponisaidia kuhesabu maombio yote ya kazi niliyoyatuma, tuligundua kuwa yalikuwa zaidi ya 400."

Ruth Ossai alisema kuwa mwaka mzima alioutumia kuomba kazi haukuathiri kujithamini kwake isipokuwa maendeleo yake kitaaluma.

"Kwahiyo sikuongeza chochote kwenye uzoefu wangu wa kazi (CV) katika kipindi hiki. Hatahivyo namshukuru Mungu sikuwa bila la kufanya."

"Sikuwa ninafanya kosa lolote"

Ruth Ossai alisema kuwa hakuwa amefanya kosa lolote au kuwa sahihi katika mitihani yake kadhaa ya kuomba kazi .

Aliongeza kuwa yalikuwa ni maelezo yale yale ya uzoefu wa kazi aliyowasilisha katika maombi yaliyompatia kazi ya ndoto yake.

Sababu ambazo huenda zilisababisha kuchelewa kuajiriwa kwake"

Ruth Ossai anaorodhesha baadhi ya changamoto ambazo huenda zilimzuwia kuwa mtahiniwa aliyechaguliwa na baadhi ya wajiri.

  • Uzoefu wa kazi : bado hana uzoefu wa kufany akazi nchini uingereza kama meneja wa afya na usalama wa kiafya.
  • Kutojua kuendesha gari : Kutokuwa na ujuzi wa kuendesha gari kwa Ruth kulichangia kuchelewa kuajiriwa kwake, kwani kazi nyingi za afya na usalama wa kiafya huhitaji mfanyakazi kuendesha gari kutoka ieneo moja kuelekea jingine kuchunguza usalama wa kiafya
  • Eneo la kazi : Maeneo mengi ambayo Ruth alikuwa anaomba kufanyia kazi yalikuw ambali na nyumbani ikwake. Hatahivyo aliazimia kuhama, aliendelea kuomba kazi mbali na mji wake
  • Utaalamu : Kazi zake za awali za Ruth kama mhandisi mkemia pia zilichangia katia kuchelewa kwake kuajiriwa, kwani mara nyingi alifanya kazi katika viwanda vya uzalishaji nchini Nigeria.

Ushauri wa Ruth Ossai ni kwamba unapoomba kazi unahitaji kujiandaa ili kufanikiwa katika mahojiano ya kazi

Kulingana na uzoefu wa Bi.Ossai haya ndiyo mambo anayowashauri watu kuyafaya wanapojiandaa kuhojiwa kwa ajili ya kazi:

  • Fanya utafiti kuhusu kampuni - Fanya utafiti na ujifunze zaidi kuhsu kampuni unayotaka kuifanyia kazi, ni yapi maadili yake muhimu, malengo yake na uangalie kama yanaendana na kile unachokitaka
  • Usidhani kuwa unafahamu kila kitu - Kuna haja ya kuelewa zaidi na usidhani kwamba unajua zaidi
  • Nenda mtandaoni na chunguza maswali yanayowea kuulizwa - Jaribu kuangalia maswali ambayo muajiri anaweza kukuuliza wakati wa kukuhoji. "Waajiri mara kwa mara hupata maswali yao mtandaoni na kuyatengeneza kulingana na viwango vyao ."
  • Jenga kujiamini kwako- Jaribu kujibu maswali yaliyoulizwa na muulizaji kwa kujiamini na utoe mifano. Muonekano wako ni muhimu sana
  • Kuwa tayari kila mara kujifunza - Ruth Ossai anasema mingi kati ya mitihani ya kazi kama vile neno "Niko tayari kujifunza'' " kwasababu wanamtafuta mtu ambaye wanaweza kumfundisha na sio mtu "anayejua kila kitu"

Ruth Ossai anasema kwamba sasa, mambo mengi yamebadilika sasa baada ya kazi iliyokuwa ndoto yake .

Sasa ameridhika kwa kufanya kazi iyake anayoipenda na kupata mshahara mzuri

"Ninafanya kile ninachojua kukifanya, kwahiyo, kukua kitaaluma na kuelewa ni nini kinachotokea haitakuwa vigumu''

"Hadi sasa mambo ni mazuri, wafanyakazi wenzangu na wakuu wangu wa kazi wamefurahi kwani nimewapunguzia mzigo wa kazi."

"Ni vizuri kwa mtu kutokana tamaa kwasababu chochote unachotaka kukifanya maishani mwako hatimaye utakifanya ," anashauri Ruth.

"Unapaswa kuweka nguvu zako zote na moyo wako wote na jiamini, usikate tamaa, endelea kusonga mbele."

Watu wengi, hasa nchini Nigeria, wanaweza kuamini kuwa ni rahisi kupata kazi ng'ambo mara unapohamia huko.