Madhya Pradesh: Kwa nini Jimbo hili la India linabomoa makazi ya Waislamu?

Serikali ya jimbo hilo inasema ubomoaji huu ni aina ya adhabu

Chanzo cha picha, Madhya Pradesh police via Twitter

Maelezo ya picha, Serikali ya jimbo hilo inasema ubomoaji huu ni aina ya adhabu
Muda wa kusoma: Dakika 3

Watu waliokuja kubomoa nyumba yake walikuja mapema asubuhi, anakumbuka Shaikh Mohammad Rafiq mwenye umri wa miaka 72.

Bw. Rafik ni muuzaji wa vinywaji baridi katika jimbo la Madhya Pradesh nchini India. Yeye na mwanawe wa kiume walikuwa na usiku mrefu. "Ni wakati wa Ramadhani, kwa hivyo biashara yetu nakuwa na shughuli nyingi nyakati za usiku baada ya watu kufuturi," alisema.

Nje,mamia ya maafisa waliokuwa na magari ya ubomuaji walikuwa wamezingira nyumba yake - iliyopo katika mtaa wenye wakazi wengi wa Kiislamu mjini Khargone - kila mmoja anajaribu kuwarai wasibomoe nyumba zao. Walipomaliza shughuli yao, kilichobakia ni vifusi. alisema.

"Tulitishika sana kiasi cha kutotamka hata neno moja- tuliwatazama kimya kimya wakibomoa kila kitu."

Nyumba na maduka kadhaa ya Waislamu yamebomolewa katika jimbo la Madhya Pradesh kufuatia ghasia za kijamii zilizozuka Aprili 10, siku ya tamasha la Kihindu la Ram Navami.

Mitandao ya kijamii imejaa picha za kusikitisha za tingatinga kubwa za rangi ya manjano zikifanya ubomozi katikati ya vitongoji, huku familia zinazolia zikitizama bila msaada.

Hili limezua ghadhabu, huku wakosoaji wakitaja kuwa ni jaribio la kisiri la kuwatenga Waislamu milioni 200 wa India linalofanywa na chama cha Waziri Mkuu Narendra Modi cha BJP, ambacho pia kiko madarakani huko Madhya Pradesh.

Serikali ya jimbo hilo imewaelekezea kidole cha lawama: "Ikiwa Waislamu watafanya mashambulizi kama haya, basi wasitarajie haki," Waziri wa Mambo ya Ndani Narottam Mishra alikiambia kituo cha habari cha NDTV.

Pia imeibua wasiwasi mkubwa kuhusu "njia ya kutojali" iliyotumiwa kutekeleza ubomoaji huo, huku wataalam wakisema hakuna uhalali wa kisheria wa kufanya hivyo. Wengine wameuta kama mfano wa adhabu ya pamoja dhidi ya Waislamu

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

"Unawaadhibu kwa njia isiyo sawa watu wa jamii moja bila kufuata utaratibu wowote unaostahili. Hii sio tu kinyume cha sheria, lakini pia inaweka mfano hatari," alisema Ashhar Warsi, wakili mkuu anayeishi mjini Indore katika jimbo hilo.

"Ujumbe ni huu: Ukihoji au kukabiliana nasi kwa njia yoyote, tutakufuata, tuchukue nyumba yako, mali yako na kukuangusha."

Ghasia hizo zilianza mara ya kwanza wakati maandamano makubwa ya waumini wa Kihindu yalipopita vitongoji na misikiti ya Waislamu, wakicheza muziki wa uchochezi ulioshinikiza vurugu dhidi ya jamii ya wachache.

Waislamu wameshutumu polisi kwa kuruhusu makundi ya Wahindu kuwashambulia. Video zinazoonyesha wanaume waliochanganyikiwa wakichomoa mapanga na kuchafua misikiti katika hatua ambayo imekuwa ya kushangaza tangu Jumapili.

Shahbaz Khan, 28, alidai kuwa waumini wa Kihindu walivunja minara ya msikiti wa eneo hilo katika jiji la Sendhwa - takriban maili 85 (137km) kutoka Khargone - na kuwakimbiza Waislamu kwa mawe.

Lakini "hofu ya kweli" ilishuhudiwa siku iliyofuata, wakati mamlaka "ilipotoka mahali popote" na kubomoa nyumba yake, alisema.

"Mke wangu na dada yangu walilia na kuwasihi polisi waturuhusu kuchukua vitu vyetu - angalau waache watoe vitabu ya kidini(Quran) nje ya nyumba - lakini walipuuzwa," alisema, akizungumza kutoka msikitini ambako anajificha.

Ubomoaji umekuwa ukiendelea tangu Jumatatu

Chanzo cha picha, Madhya Pradesh police via Twitter

Maelezo ya picha, Ubomoaji umekuwa ukiendelea tangu Jumatatu

Serikali ya jimbo hilo inasema ubomoaji huu ni aina ya adhabu dhidi ya wale wanaodaiwa kushiriki katika kurusha mawe na uchomaji moto. "Nyumba ambazo mawe hayo yametoka zitageuzwa kuwa rundo la mawe zenyewe," Bw Mishra alisema hivi majuzi.

Kisheria, hata hivyo, hatua hiyo imehalalishwa kwa misingi ya ujenzi usioidhinishwa - polisi wanadai kuwa wanalenga uvamizi haramu wa watu wanaochuchumaa kwenye ardhi ya umma.

Mkusanjaji ushuru wa Wilaya ya Khargone #Anugraha P alisema "ni mchanganyiko wa zote mbili".

"Kutafuta wahalifu mmoja baada ya mwingine ni mchakato unaochukua muda, kwa hivyo tuliangalia maeneo yote yaliyokumbwa ghasia na kubomoa majengo yote haramu ili kutoa funzo kwa wale wafanya fujo," alifafanua.

Lakini Bw Rafiq alisema hakukuwa na visa vya ghasia katika mtaa wake. "Nina hata karatasi zangu zote za mali kuthibitisha kuwa si haramu," aliongeza. "Lakini polisi walikataa kunisikiliza na kuninyang'anya nyumba yangu."

Wataalamu pia wanahoji mantiki hii - wanasema kuwa kuadhibu mtu kwa madai ya uhalifu kwa kutumia sheria zilizokusudiwa kwa mwingine hakuna maana.

"Uhalali unatumika kama kisingizio - nyumba hizi hazikuwa halali hata kabla ya maandamano ya kidini. Huwezi kuchagua kulipiza kisasi kwa sababu hiyo ni ukiukaji wa taratibu zote zinazofaa," mwanasayansi wa siasa Rahul Verma, anasema. "Jimbo linaonyesha mwenendo wa kulipiza kisasi."

Bw Warsi anasema ingawa serikali ina uwezo wa kubomoa majengo haramu, kuna utaratibu unaozingatiw - kumpatia mmiliki ilani, kuwapa nafasi ya kujibu au kutuma maombi ya mahakama - ambayo yanafaa kufuatwa kabla ya hapo.

Polisi wanashikilia kuwa walitoa notisi kwa watu wanaodaiwa kuvamia eneo hilo, lakini familia tatu ambazo BBC ilizungumza nazo zilikanusha hilo.

Kando na hilo, kuna vifungu vingine chini ya sheria ya serikali (Sheria ya Shirika la Manispaa ya Madhya Pradesh, 1956), kama vile kumtaka mshtakiwa kulipa faini, ambayo mamlaka inaweza kutumia kwanza, Bw Warsi anaongeza.

"Ubomoaji wa mali unatakiwa kuwa suluhu la mwisho."

Lakini hii si mara ya kwanza kwa serikali ya Madhya Pradesh ya Waziri Mkuu Shivraj Singh Chouhan inatumia njia hii kama hatua ya kutumikia haki. Serikali imebomoa nyumba za watuhumiwa wa ubakaji, majambazi na wahalifu wengine siku za nyuma.