Nazanin Zaghari-Ratcliffe: Kwa nini ameachiliwa sasa?

Chanzo cha picha, PA Media
Ni takriban miaka sita tangu Nazanin Zaghari-Ratcliffe azuiliwe kwa mara ya kwanza na mamlaka ya Iran mwezi Aprili 2016. Tangu wakati huo kulikuwa na majaribio ya mara kwa mara ya kutaka aachiliwe - lakini yote yalishindikana.
Kwa nini amerudi nyumbani sasa?
Jibu la msingi ni mahusiano ya London-Tehran ni bora kuliko yalivyokuwa.
Maafisa wa kikosi maalum cha Revolutionary Guards huko Iran na mahakama ya Iran hawaoni tena kuwa wanamuhitaji Bi Zaghari-Ratcliffe kwa ajili ya kujiinua katika mahusiano na Uingereza.
Alikuwa kibaraka wa kidiplomasia aliyeshikiliwa mateka na mamlaka ya Iran kuweka shinikizo kwa London.
Ikiwa Tehran alitaka kufanya vizuri, wangemtendea vyema, kumpa ufikiaji wa usaidizi wa matibabu, labda kuongeza kutembeleana mara kwa mara, ikiwezekana hata kumruhusu kukaa kwa muda kutoka jela.
Ikiwa Tehran alitaka kutoa shinikizo kwa London, basi hali yake inaweza kuwa mbaya zaidi na marupurupu yanaweza kuondolewa.
Kulipa deni 'tofauti kubwa'
Uingereza kulipa deni la kihistoria la £400m kwa mizinga iliyouzwa lakini haijawasilishwa ingepelekea mabadiliko makubwa.
Kwa miaka mingi, Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO) ilidai masuala hayo mawili hayakuwa na uhusiano.
Lakini kiutendaji, Wairani walifanya kuwa suala moja.
Baadhi ya FCDO walitaka kulipa deni lakini walizuiwa mwanzoni kwa ukosefu wa utayari ndani ya Hazina na Marekani, wakihofia ingewazawadia utekaji nyara na hata kufadhili ugaidi.
Pia kulikuwa na hofu kwamba Marekani ingeiadhibu taasisi yoyote ya fedha ya Uingereza ambayo ililipa fedha hizo kwa wizara ya ulinzi ya Iran kwa kukiuka vikwazo vya kimataifa.
Pia kuna kutotulia kabisa kwa familia kufanya kampeni na diplomasia ya Uingereza.
Mwanzoni kulikuwa na makosa, kama vile madai ya uwongo ya Boris Johnson kwamba Bi Zaghari-Ratcliffe amekuwa akiwafunza waandishi wa habari nchini Iran, madai ambayo yaliifanya Iran kuwafungulia mashtaka mapya.

Chanzo cha picha, Family Handout
Lakini kampeni ya bila kuchoka ya mume wa Nazanin, Richard Ratcliffe, na wengine iliendelea kushinikiza serikali ya Uingereza.
Na hilo lilidhihirishwa na kazi ya wanadiplomasia wa Uingereza nyuma ya pazia, wakikataa kuiacha Iran isahau kuhusu kesi hiyo.
Kulikuwa na karibu mpango wa kuwaachilia wafungwa mwaka jana lakini haukufanikiwa.
Lakini tangu wakati huo wanadiplomasia wa Uingereza wameitembelea Iran mara kadhaa kujaribu kufikia makubaliano mapya.
Maafisa wa Iran katika Wizara yao ya Mambo ya Nje mara kwa mara walichanganywa kwamba mzozo huu uliingia katika uhusiano wa Uingereza na Iran.

Chanzo cha picha, Reuters
Lakini wanadiplomasia wa Iran hawakuwa na mamlaka - IRGC na majaji walikuwa.
Hatimaye, watu wa kutosha na serikali ya Iran walionekana kutambua kwamba uhusiano wa uhasama wa kudumu na Uingereza haukuwa katika maslahi bora ya Tehran.
Hilo linaweza kutumika moja kwa moja kwa mazungumzo yanayofanyika Vienna, yaliyoundwa kufufua makubaliano ambayo Iran ilipunguza shughuli zake za nyuklia kwa malipo ya kuona vikwazo vya kiuchumi vimeondolewa.
Makubaliano mapya?
Uchumi wa Iran umekuwa ukiyumba, Iran inataka kukubaliana na mpango mpya, na uhusiano bora na Uingereza unaweza kufanya hilo kutokea.
Mpango huo bado haujakubaliwa lakini wanadiplomasia wanasema makubaliano yanakaribia.
Na katika wiki za hivi karibuni, wakati wa mzozo wa Ukraine, maslahi ya Uingereza na Iran pia yamekaribiana zaidi.
Ikiwa vikwazo vinaweza kuondolewa na Iran kuanza kuuza mafuta yake tena, hiyo inaweza kusaidia kupunguza bei ya nishati duniani.
Hiyo ni kwa maslahi ya Uingereza na Iran.
Katika muktadha huo, pande zote mbili zinaweza kutaka kufuta safu za kidiplomasia na kufanya makubaliano zaidi.















