Covid-19 miaka miwili: Mambo matano tuliyojifunza tangu kuzuka kwa janga la corona

Ni miaka miwili tangu Shirika la Afya Duniani kutangaza rasmi kwamba mlipuko wa Covid-19 ulikuwa janga la kimataifa.

Tangu, tarehe 11 Machi 2020, ulimwengu umebadilika kwa kiwango kikubwa - kuanzia jinsi tunavyofanya kazi hadi matibabu yanayopatikana.

Haya hapa mambo matano tuliyojifunza tangu kuanza kwa janga la corona.

1. Chanjo za MRNA zinafanya kazi na zinaweza kutengenezwa haraka

Mara baada ya janga kuanza, watafiti walianza mbio ya kutengeneza chanjo ambayo ingewalinda watu dhidi ya Covid-19.

Baadhi ya makampuni ya dawa yaliamua kutumia aina ya teknolojia ambayo matokeo yake haijawahi kutumika kutengeneza chanjo iliyoidhinishwa kwa matumizi ya binadamu - mRNA.

Hatua hiyo ilisaidia. Sio tu kwamba Pfizer-BioNTech (na baadaye, Moderna) iliweza kutengeneza chanjo ya Covd-19 haraka kuliko mtu mwingine yeyote anayetumia mRNA, lakini kwa kufanya hivyo pia ilifungua mlango wa matibabu mapya kwa kutumia teknolojia kama hiyo.

Mchakato huo unafanya kazi kuchukua kipande kidogo cha msimbo wa kijeni, unaoitwa mRNA, na kuipaka kwenye mafuta.

Katika chanjo za coronavirus mRNA inaelekeza seli zetu kuunda sehemu ndogo ya virusi vya Covid-19.

Kipande hiki hakina madhara lakini mfumo wa kinga ya mwili unaweza kujifunza kukitambua ili uwe tayari kushambulia virusi halisi vya Covid-19 iwapo utaambukizwa

2. Covid-19 inasambaa kupitia hewa kwa urahisi kuliko tulivyofikiria awali

Karibu miezi minne baada ya mlipuko wa Covid-19 kutangazwa, Shirika la Afya Duniani liliweka ujumbe kwenye mtandao wake wa Twitter kusema : "UKWELI: #COVID19 haiambukizwi kupitia hewa."

Wakati huo wataalamu wa WHO hawakuwa wakiwashauri watu kuvalia barakoa.

"Hakuna ushahidi mahususi unaoashiria kuwa uvaaji wa barakoa una faida yoyote," mkurugenzi mtendaji wa mpango wa dharura wa afya wa WHO, Dk Michael Ryan.

"Hatushauri utumiaji wa barakoa pengini ujiskie mgonjwa," aliongeza Maria Van Kerkhove, Kiongozi wa Kiufundi wa Covid-19.

Lakini kile tulichojifunza tangu kuzuka kuanza kimebadilisha maoni hayo. WHO sasa inasema watu wanapaswa "kufanya kuvaa barakoa kuwa sehemu ya kawaida ya kuwa karibu na watu wengine."

Hii ni kwa sababu kuna ushahidi unaoongezeka kwamba Covid-19 haiambukizwi tu kupitia matone makubwa ya mate au kamasi ambayo iko hewani kwa muda mfupi baada ya mtu kukohoa au kupiga chafya, au kwa kugusa sehemu iliyo na virusi.

WHO sasa inasema "inaweza pia kuenea kupitia aerosols" - chembe ndogo zaidi ambazo zinaweza kubaki kwenye hewa kwa muda mrefu zaidi.

Kuvuta hewa yenye virusi

Katika tahariri, Jarida la Matibabu la Uingereza lilisema: "Watu wanapokaribiana, wana uwezekano mkubwa wa kuambukizwa virusi kwa kuvuta hewa kuliko kuruka hewani kwa matone makubwa ya mate yanayotua machoni mwao, puani, au. midomo."

"Usambazaji wa SARS-CoV-2 baada ya sehemu inayoguswa na watu wengi kama vile milango sasa unachukuliwa kuwa mdogo."

Utafiti umepata mifano ambapo watu walio na Covid wameambukiza wengine ambao walikuwa umbali wa zaidi ya mita mbili au wamepata virusi kwenye anga ambayo mtu aliyeambukizwa alikuwepo dakika au saa kadhaa awali.

"Mnambo Machi [2020], watu walikuwa wakinipigia simu kuniuliza ni kwa muda gani walihitaji kuloweka kopo la maharagwe kwenyemaji yenye dawa kabla ya kuileta nyumbani. Kila mtu alikuwa mwangalifu," alisema. Paula Cannon, Profesa Mashuhuri wa Biolojia ya Molecular Microbiology & Immunology katika Shule ya Keck ya Tiba ya USC.

"Tangu wakati huo tumejifunza kuwa virusi vinavyopatikana katika chumba ambacho hakina hewa ya kutosha -inayotplewa na watu ambao hawajavalia barakoa wanapozungumza au kuimba au kupumua tu - ndio sababu inayowezekana kueneza na sababu ndio kwa nini baa na migahawa ya ndani ni hatari sana."

Kunawa mikono na kuosha maeneo yanayoguswa na watu wengi bado ni jambo ambalo linatiliwa mkazo lakini cha msingi zaidi ni kuvalia barakoa na kuwa katika chumba kilicho na nafasi ya kuingiza hewa safi.

3. Wengi wetu sasa tunafanya kazi nyumbani, na tutaendelea kufanya hivyo

Mamilioni ya watu kote duniani walilazimika kufanya kazi nyumbani wakati wa janga la corona.

Ni kitu ambacho hakingewezekana kiufundi miaka michache iliyopita, lakini Covid ameonyesha kwamba inawezekana. Hali ambayo inaweza kubadilisha jinsi mamilioni ya wanavyofanya kazi.

Kampuni kubwa ya mitandao ya kijamii ya Twitter iligonga vichwa vya habari kote duniani mnamo Mei 2020 iliposema: "Wafanyikazi wa Twitter sasa wanaweza kufanya kazi wakiwa nyumbani milele... miezi michache iliyopita imethibitisha kuwa tunaweza kuifanya kazi hiyo."

Hata hivyo, iliongeza kuwa wafanyikazi walihitaji "kufanya majukumu ambayo yanaweza kufanyika kazi nyumbani".

Facebook ilitoa tangazo kama hilo mapema mwaka huu, lakini sio tu wakuu wa kampuni za teknolojia wanafanya mabadiliko hayp.

Kura ya maoni ya kampuni 1,200 iliofanywa na kampuni ya utafiti ya Enterprise Technology ilionyesha kuwa asilimia ya wafanyikazi ambao wanafanya ya kudumu nyumbani kote duniani iliongezea mara mbili mnamo 2021.

Hilo ni jambo ambalo wafanyikazi wengi wanataka kuona likitokea pia.

Katika uchunguzi wa kimataifa wa watu zaidi ya 200,000 katika nchi 190, Boston Consulting iligundua kuwa 89% ya watu walitarajiwa kuwa na uwezo wa kufanya kazi nyumbani wakati fulani.

4. Jangala corona liliwaathiri watu walio hatarini zaidi katika jamii

Ulimwengu ni mahali pasipo usawa na, cha kusikitisha, mlipuko wa Covid-19 umeonyesha kuwa janga kama hilo linaweza kuifanya kuwa mbaya zaidi.

Huko Uingereza, utafiti uliofanywa na watafiti katika Benki ya Biobank ya Uingereza uligundua kuwa sehemu iliyoathiriwa zaidi ya nchi 11.4% ya watu walikuwa wameambukizwa Covid wakati katika maeneo duni kiwango kilikuwa cha chini (7.8%).

Utafiti huo pia ulibaini kuwa watu kutoka jamii za walio wachache ziliathiriwa, jambo ambalo pia limetokea nchini Marekani.

Huko New York, data ya mwaka 2020 ilionyesha kuwa Wahipania na Wamarekani weusi walijumuisha 34% na 28% ya vifo vya Covid, mtawaliwa, lakini ni 29% na 22% tu ya idadi ya watu nchini Marekani. .

Katika nchi nyingi, data sahihi kuhusu madhara ya Covid haipo, lakini kote duniani mojawapo ya tofauti kubwa zaidi iliyojitokeza ni viwango vya chanjo.

5. Hatuna uhakika wa jinsi, au kama, janga la Covid-19 litaisha

Neno ''herd immunity'' (idadi kubwa ya watu kupata chanjo ili kudhibiti maambukizi) lilipata umaarufu mwanzoni mwa janga hilo - wazo likiwa kwamba ikiwa watu wa kutosha watapata usugu dhidi ya Covid, ama kwa kuambukizwa ugonjwa huo au chanjo, virusi vitakuwa tishio kidogo.

Hilo huenda likawa vigumu kufikia. Imebainika kuwa mwitikio wa mifumo yetu ya kinga hupungua kadiri muda unavyosonga, ndiyo maana nchi zinazoweza zinazindua mpango wa chanjo ya nyongeza.

Kulingana na Shabir A Madhi, Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya na profesa wa chanjo katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Afrika Kusini, mwitikio wa kinga baada ya kuambukizwa au chanjo huchukua takriban miezi sita hadi tisa.

Ingawa chanjo ni kinga dhidi ya ugonjwa mbaya, hata zile bora zaidi hazionekani kuwazuia watu kuambukizwa Covid (ingawa watu walioambukizwa huenda wasionyeshe dalili zozote) na kuwaambukiza wengine.

"Kwa chanjo tulizo nazo, hata kama zinapunguza maambukizi, dhana ya watu wengi kupata chanjo haina maana," Dk Salvador Peiró, wa taasisi ya utafiti ya FISABIO huko Valencia nchini Uhispania, aliiambia BBC Mundo.

Hii ni kwa sababu virusi vimebadilika kwa haraka na aina nyingine ya corona, ambayo inaweza kuambukizwa kuibuka na huenda ikawa vigumu kudhibitiwa kwa chanjo.