Makumbusho ya Historia ya Asili nchini Uingereza yathibitisha kuwa mdudu jamii ya panzi (stick ) ni dume na jike

Stick insect

Chanzo cha picha, Paul Brock/NHM

Maelezo ya picha, Sehemu yenye rangi ya kijani ya mdudu ni jinsia ya kiume na nusu nyingine ya rangi ya kahawia ni jinsia ya kike

Mdudu mmoja alishangaza mmiliki wake alipogundua kuwa alikuwa ni nusu dume na nusu jike - akijulikana kama gynandromorph.

Charlie, mdudu wa jamii ya panzi mwenye rangi ya kijani kibichi, alionyesha rangi yake halisi baada ya kutoa ngozi yake nyumbani huko Suffolk ili kufichua mwili wa kijani kibichi wa mbawa za kike na kahawia za dume.

Wataalamu katika Makumbusho ya Historia ya Asili walithibitisha kuwa ilikuwa "gynandromorph ya kwanza iliyoripotiwa katika spishi hiyo.

Mmiliki Lauren Garfield ametoa mdudu huyo kwa jumba la makumbusho la London kwa ajili ya utafiti wa kisayansi.

Charlie, au Diapherodes gigantea, awali alionekana kama wadudu wengine wa kijiti Bi Garfield anafuga nyumbani kwake huko Waldringfield.

Stick insect

Chanzo cha picha, Lauren Garfield

Maelezo ya picha, Mmiliki wake alituma picha kadhaa za Charlie kwenye ukurasa wake wa Facebook

Wadudu hawa wanaofahamika kama (stick) huota mara kadhaa na Charlie alipotoa ngozi yake, kila mtu alianza kugundua kiumbe huyo asiye wa kawaida.

Picha za mdudu huyo wa Bi Garfield, na mwili wake wa kike nusu kijani kibichi, pamoja na mbawa za kahawia za dume, zilionwa na Felixstowe Radio baada ya kuandika "tahadhari ya ajabu" kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu wadudu wake hawa wa jamii ya panzi.

"Kawaida sina tabia ya kuwafuatilia sana wadudu , lakini Charlie ni tofauti." aliiambia BBC

Alisema mwanae alifurahi sana, alichukua mdudu shuleni ili kuwaonyesha watoto wengine.

Male and female stick insects

Chanzo cha picha, Lauren Garfield

Maelezo ya picha, Lauren Garfield alipiga picha ya shehemu ya jinsia ya kiume (kushoto) na kike (kulia) ya mdudu kuonyesha utofauti wa ukubwa na rangi zake

Kisha Bi Garfield aliwasiliana na Paul Brock, mtaalamu wa wadudu katika Jumba la Makumbusho la Historia ya Asili, na baada ya kubadilishana picha, alikubali kumtuma Charlie kwa uchunguzi.

Bw Brock alielezea wadudu wa vijiti wa Bi Garfield kama "wa kukumbukwa".

"Wafugaji wengi wa wadudu hawa hawakutani na gynandromorph," alisema.

"Mnamo mwaka wa 1958, mwandishi alionyesha uwezekano wa asiilimia 0.05 ya kutokea kwa gynandromorphs kwa wadudu wa jamii ya panzi(stick) katika maabara ya Carausius morosus, iliyohifadhiwa katika utamaduni huko Ulaya na kwingineko tangu mwaka 1901.

Mdudu wa aina ya panzi(stick) mwenye rangi ya kijani

  • Diapherodes gigantea anajulikana sana kama mdudu mkubwa wa kijiti wa chokaa au wadudu wa kijiti cha kijani kibichi.
  • Aina hiyo ina asili ya visiwa vitatu vya Caribbean - St Vincent, Grenada na St Lucia
  • Katika pori hula majani ya mimea na miti katika maeneo ya misitu ya mvua
  • Katika sehemu zinazolimwa zaidi za visiwa hivyo hula mipera, miti ya mdalasini, mikorosho na mimea asilia.
  • Wakiwa kizuizini, wanachukuliwa kuwa rahisi kutunza, kulisha majani ya miiba, eucalyptus au mwaloni.
  • Urefu wa mwili wa dume ni kawaida kati ya sentimita 9 (3.5in) na sentimita 13 (inchi 5), wakati wanawake hukua hadi kati ya sentimita 14 (5.5in) na sentimita 18 (7in)
  • Muda wa kuishi wa kizuizini ni hadi mwaka mmoja

Chanzo: Paul Brock - mshirika wa kisayansi aliyebobea wa wadudu katika Idara ya Sayansi ya Maisha, katika Jumba la Makumbusho la Historia ya Asili, London

Judith Marshall, kutoka idara ya Sayansi ya Maisha ya jumba la makumbusho, alisema: "Huu ni mfano wa kuvutia sana.

"Ingawa anaonekana kama mwanamke mzima wa kawaida katika ukubwa wa mguu na mwili, ana upande wake wa kulia mbawa ndefu za dume mzima."

Unaweza pia kusoma:

Bibi Garfield alisema kwa bahati mbaya Charlie atalazimika kuuawa ili wadudu hao wachunguzwe ipasavyo katika siku zijazo, kwani mara tu wanapokufa kawaida, "husinyaa na kupoteza rangi yao".

Bw Brock alisema wadudu hao wataongezwa kwenye mkusanyiko wa jumba hilo la makumbusho "ambapo watawavutia watafiti".

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Kwanini watu wengi wanaogopa kula wadudu wakati zaidi ya watu bilioni mbili wanakula?