Kwanini binadamu wengi hawako tayari kula wadudu ingawa wanachukuliwa kama "chakula bora"

Chanzo cha picha, Getty Images
Inaweza kuchukua muda kidogo kuzoea kula vyakula vilivyochanganywa na panzi, nyenje, konokono au kuchanganya na nyungunyungu na minyoo wengine kwenye wali.
Hata hivyo, hata kama wazo la kula wadudu huenda kikafanya tumbo kunguruma kwa kufikiria tu, baadhi ya watafiti wanasema wanadudu wanastahili kuwa sehemu muhimu ya mlo wetu wa kila siku.
Ingawa bado uhalisia wa kula wadudu haujakubalika hasa katika mataifa mengi ya magharibi na Afrika, binadamu wamekuwa wa kila wadudu kwa miaka elfu kadhaa na kuna sehemu kadhaa duniani ambako huu umekuwa utamaduni wa kawaida.
Takriban spishi 20,000 za wadudu huliwa na mataifa kama ya Asia, Amerika Kusini na hata sehemu zingine za Afrika.
Mfano nchini Thailand, wachuuzi huuza panzi waliokaangwa masokoni.
Na nchini Japani, mabuu ya nyigu ni mlo mtamu sana na huliwa yakiwa mazima yaani hajapikwa.
Suluhu mara mbili
"Wadudu ni sehemu muhimu sana ya mlo unaokosekana kwenye mfumo wetu wa chakula," amesema Virginia Emery, mwanzilishi wa kampuni moja inayotengeneza chakula cha ng'ombe kutokana na minyoo.
"Kuna viritubisho vingi katika kiwango kidogo tu cha chakula," amesema.
Na kwasababu ya hili, kuanzisha mazoea ya kula wadudu kama chakula kunaweza kutatua matatizo mawili makubwa duniani: uhaba wa chakula na mabadiliko ya hali ya hewa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ufugaji pekee unachangia takriban asilimia 14.5 ya hewa chafuzi duniani, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO). Na hii ndio sababu 'lazima kufanyike mabadiliko, tena mabadiliko makubwa.'Umuhimu wa kuanzisha mazoea
Ukulima wa wadudu unatumia sehemu kidogo tu ya ardhi, nishati na maji vyote hivyo vikiwa na mchango kidogo tu katika uchafuzi wa hali hewa.
Wadudu nyenje wanatengeza hadi chini ya asilimia 80 ya kemikali ya methani ikilinganishwa na ng'ombe na chini ya mara 8 na 12 ya kemikali ya ammonia ikilinganishwa na nguruwe, kulingana na watafiti wa chuo kikuu cha Uholanzi.
Methani ni gesi chafuzi ya kiwango cha juu mno ingawa maisha yake ni mafupi na inaathiri mabadiliko ya hali ya hewa mara 84 zaidi ikilinganishwa na kaboni dioksidi kwa kipindi cha miaka 20.
Kwa pande mwingine, ammonia ni gesi yenye harufu kali sana na chafuzi kwa mazingira inayochafua mchanga, maji ya chini ardhi na mfumo wa ikolojia.
Ikiwa dunia nzima itakumbatia ufugaji wa wadudu, itakuwa kheri kwa kiasi kikubwa cha ardhi ambacho sasa hivi kinatumika kwa ufugaji wa wanyama, na uzalishaji wa chakula ama kwa binadamu au kwa wanyama.

Kuwa na mbadala wa nyama nusu ya kiwango cha sasa duniani na minyoo ambayo ni chakula na wadudu panzi, kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza sehemu kubwa inayotumika kwa kilimo.
Pia, Tilly Collins, mtafiti mwandamizi katika kituo kinachoangazia Sera ya Mazingira, amesema kuwa wadudu wanaweza kukidhi baadhi ya mahitaji ambayo ni vigumu kutimizika kwa kutegemea mimea.
Ameongeza kuwa "ni kheri kukuza wadudu kwa ukamilifu kwasababu lishe inayotegemea mazao mara nyingi huwa na kiwango kikubwa cha kaboni."

Kiwango cha wadudu kuzaliana na kufikia kiwango cha ukomavu ni siku kadhaa tu badala ya miezi au miaka kama ilivyo kwa mifugo na mimea na pia kiwango cha uzalianaji wao kinaweza kufika hata elfu kadhaa.
Kiwango cha lishe ya wadudu nyenje ni cha chini ya ng'ombe kwa mara sita, mara nne chini ikilinganishwa na kondoo na mara mbili chini ya nguruwe, kulingana na FAO.
Hii ni kwasababu wadudu wanatambulika kuwa na damu baridi na hivyo basi kiwango cha nishati wanachopoteza ni cha chini mno wakati wanadumisha joto la mwili, mtafiti Alexander amesema.
Pia ameongeza kuwa uchafu wao wanaotengeneza ni wa chini kabisa.
"Kwa wanyama, nyama nyingi zinatupwa, lakini kwa wadudu unakula kila kitu,"ameseama.
Pia, wadudu wanaweza kuishi kwa chakula na mimea ambayo ingetupwa na hivyo basi kuchangia kwenye mzunguko wa uchumi ambapo raslimali zitakuwa zinachakatwa upya na kutumika tena.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Tunashirikisha wadudu na kila kitu isipokuwa chakula pekee," amesema mtafiti Giovanni Sagari.
Mtaalamu huyo amesema kuwa mara nyingi wadudu huusishwa na uchafu, hatari, vitu vibaya au vile vinavyotufanya kuhisi vibaya.
Lakini kuna umuhimu wa tabia hii kuanza kubadilika.
Pia Sagari anasema, itakuwa vizuri zaidi ikiwa wadudu watakuwa wanasagwa na kuongezwa kwenye vyakula badala ya kuliwa wazima wazima kama vitafunwa.
Inaweza kuchukua muda kidogo kuzoea kula vyakula vilivyochanganywa na panzi, nyenje, konokono au kuchanganya na nyungunyungu na minyoo wengine kwenye wali.
Hata hivyo, hata kama wazo la kula wadudu huenda kikafanya tumbo kunguruma kwa kufikiria tu, baadhi ya watafiti wanasema wanadudu wanastahili kuwa sehemu muhimu ya mlo wetu wa kila siku.
Ingawa bado uhalisia wa kula wadudu haujakubalika hasa katika mataifa mengi ya magharibi na Afrika, binadamu wamekuwa wa kila wadudu kwa miaka elfu kadhaa na kuna sehemu kadhaa duniani ambako huu umekuwa utamaduni wa kawaida.
Takriban spishi 20,000 za wadudu huliwa na mataifa kama ya Asia, Amerika Kusini na hata sehemu zingine za Afrika.
Mfano nchini Thailand, wachuuzi huuza panzi waliokaangwa masokoni.
Na nchini Japani, mabuu ya nyigu ni mlo mtamu sana na huliwa yakiwa mazima yaani hajapikwa.
Umuhimu wa kuanzisha mazoea
Ukulima wa wadudu unatumia sehemu kidogo tu ya ardhi, nishati na maji vyote hivyo vikiwa na mchango kidogo tu katika uchafuzi wa hali hewa.
Wadudu nyenje wanatengeza hadi chini ya asilimia 80 ya kemikali ya methani ikilinganishwa na ng'ombe na chini ya mara 8 na 12 ya kemikali ya ammonia ikilinganishwa na nguruwe, kulingana na watafiti wa chuo kikuu cha Uholanzi.
Unaweza pia kusoma: