Unaweza kuugua au kufa ukila vyakula hivi

Baadhi ya vyakula vinaweza kuonekana kuwa sio hatari lakini vina madhara makubwa kwa mwili wa binadamu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya vyakula vinaweza kuonekana kuwa sio hatari lakini vina madhara makubwa kwa mwili wa binadamu

Vyakula huwa vinaonekana kuwa havidhuru lakini ukweli ni kwamba sio kila kitu kinaweza kulika bila kuchukua tahadhari kama ya kuchagua chakula, upishi au maandalizi ya chakula - jinsi ya kutoa sehemu ya sumu iliyopo kwenye chakula.

Bila kuzingatia hatua hizi, baadhi ya vyakula ukila vinaweza kukufanya uugue sana, dalili zake huanzia kwenye kupata kichefuchefu , kujisikia vibaya na hata kifo.

Katika hali mbaya au chakula ambacho hakijatunzwa vizuri au kupikwa vizuri, mtu anaweza kupata kichefuchefu, kushindwa kupumua vizuri, au hata kufa.

Vyakula ambavyo mtu unapaswa kuwa makini kuvila

Kama huna uhakika kuwa ni sehemu gani ya chakula hicho inabidi uiondoe basi ni bora kuacha kuvila kabisa.

Samaki aina ya 'Puffer'

Samaki huyu ni chakula kinachopendwa kuliwa nchini Japan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Samaki huyu ni chakula kinachopendwa kuliwa nchini Japan

Samaki huyu ni hatari na anaua.

Hii ni kutokana kuwa na sumu ambayo inaogopeka kuwa inaweza kumdhuru mtu haraka sana.

Licha ya samaki huyo kuwa hatari, 'puffers' bado kuna baadhi ya mataifa wanaona kuwa ni chakula cha kipekee.

Nchini Japan, samaki huyu huwa analiwa katika supu.

Mpishi wa samaki huyu anapaswa kuwa amepata mafunzo kwa miaka kadhaa kabla ya kuruhusiwa kupika samaki wa aina hii kwa ajili ya wateja.

Kitu cha muhimu ni kuwa lazima kuhakikisha kuwa wakati samaki huyu anaandaliwa mezani, sehemu yote ya sumu imeondolewa ikiwa pamoja na ubongo, ngozi, macho,ini na utumbo vimeondolewa.

Sehemu ya ndani ya samaki ambazo zinahitajika kutolewa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mpishi wa samaki huyo anapata kupata mafunzo ya muda mrefu ili kuwa na utaalamu wa kuondoa viungo vyenye sumu kwenye samaki

Jibini inayofahamika kama 'Casu Marzu'

Kitu kinachoshangaza katika chakula hiki ni minyoo iliyo ndani yake.

Inaweza kutokupa hamu ya kukila lakini jibini ya aina hii kutoka Sardinia nchini Italia, watu wengi wanaipenda.

Casu marzu imetengenezwa na wadudu,ambao wana ladha ya jibini.

Baada ya muda, funza waliowekwa ndani ya jibini huilainisha kwa ajili ya kutumika.

Jibini hiyo inadaiwa kuwa na ladha sawa na jibini inayotengenezwa kaskazini mwa Italia inayofahamika kama 'gorgonzola'.

Casu marzu ina ladha nzuri na yenye nguvu zaidi.

Ladha yake ndio kitu ambacho wengi wanavutiwa nacho na hata namna ya kuwa mwepesi wa kula wadudu hao maana wanaweza kuruka wakati unakula.

Casu marzu cheese

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jibini ya Casu marzu

Vilevile jibini hii haipatikani kwa urahisi.

Jibini aina ya Casu marzu haijaorodheshwa katika orodha za vyakula ambavyo vimethibishwa kwa kula barani ulaya na hakiwezi kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi.

Jibini hiyo pia inatajwa kuwa hatari zaidi kiafya.

Labda kama funza hao wamekufa kutokana na baridi la jokofu.

Jibini hiyo isipotunzwa vizuri inaweza kuvuruga tumbo na kumfanya mtu kutapika na kuharisha.

Casu marzu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Casu Marzu inadaiwa kuwa jibini hatari zaidi duniani

4. Maharage mekundu

Maharage mekundu pia ni hatari kwa afya

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maharage mekundu pia ni hatari kwa afya

Kwa ujumla huwa tunasema kuwa maharage ni mazuri kwa afya, lakini kuna aina ya maharage kama hayataandaliwa vizuri yanaweza kukufanya uugue ukila.

Maharage mekundu ndio aina ya maharage ambayo yanatajwa kuwa na ladha nzuri, yenye virutubishi, protini, vitamini na madini.

Lakini kwa upande mwingine aina hiyohiyo ya maharage ina sehemu inayojulikana kama 'phytohaemagglutinin' ambayo huwa sio rahisi kuyeyuka.

Kama ukijaribu baada ya muda, jiandae kutapika na maumivu ya tumbo.

Habari njema ni kuwa kama maharage hayo yakipikwa vizuri , madhara kama hayo yanaweza yasikupate.

Kama ilivyo kwenye maharage mekundu, maharage ya soya pia yana protini lakini ya sumu asili ambayo mtu unapaswa kuwa makini kuyaandaa.

Ni vyema maharage hayo yakalowekwa kwenye maji walau saa 12 kabla ya kuchemshwa.

Karanga zinazojulikana kama'Kungu'

Kungu zinaweza kukusababishia madhara ukila kupita kiasi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kungu zinaweza kukusababishia madhara ukila kupita kiasi

Kiungo hiki ni maarufu zaidi nchini Indonesia.

Karanga hiyo huwa inatumika kama kingo katika baadhi ya vyakula ili kuongeza ladha.

Huwa ni zao la msimu ambalo linaweza kuwekwa kwenye viazi, mboga za majani, nyama na hata baadhi ya vinywaji.

Ingawa zikitumika kwa wingi huwa zinasababisha mtu kuwa na kichefuchefu, kushindwa kupumua vizuri, maumivu na mara chache madhara yake huwa yanasababisha vifo.

Lakini kwa nini mtu anaweza kuamua kula kiungo hicho kwa wingi?

Ni kwa sababu ya ladha yake kuwa nzuri na kuwavutia wengi.