Je ni taifa gani lenye jeshi lenye uwezo mkubwa katika eneo la Uarabuni?

Chanzo cha picha, RT
Maeneo ya mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini yanachukuliwa kuwa miongoni mwa maeneo yaliyo imara zaidi duniani.
Hatahivyo tasisi ya Uchumi na Amani imeelezea eneo hilo kuwa moja ya maeneo yenye shida zaidi ulimwenguni.
Hili si jambo la kushangaza kwa kuzingatia hali ya migogoro nchini Iraq, Libya, Syria na Yemen, pamoja na mzozo wa Palestina na Israel na pia mzozo wa Saudia na Iran.
Mengi ya machafuko haya ni vita vinavyoanzishwa na baadhi ya nchi kwaa nchi kama njia ya kupima uwezo wao.
Katika ripoti hii, tunaangalia nchi 10 zenye nguvu zaidi katika Mashariki ya Kati, tukianza na nambari kumi.

Chanzo cha picha, AFP
10.Kuwait
Hapo awali iliripotiwa kuwa jeshi la anga la Kuwait lina ndege za kivita aina ya Hornets 39 zenye kiti kimoja na viti viwili, katika huduma yake tangu 1992. Ndege hizo hatahivyo zimeboreshwa kisasa.Kuwait inatarajiwa kupata ndege mpya 56 aina ya Typhoons 28 za Eurofighter na 28 Boeing F/A-18E/F Super Hornets.Kuwait pia ina makombora ya PAC-2 na PAC-3 Patriot ya ardhini.
9. Qatar
Jeshi la Qatar lilianzishwa mwaka 1971 baada ya nchi hiyo kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. Iikiwa na nguvu ya wanajeshi 11,800, vikosi vya jeshi vya Qatar ndio vya pili kwa udogo katika Mashariki ya Kati. Ufaransa imetoa takriban 80% ya orodha ya silaha za Qatar.Kikosi cha anga cha Qatar Emiri Air Force (QEAF) tayari kimenunu ndege 36 za Boeing F-15QA, na idadi sawa ya ndege za kijeshi za Dassault Aviation Raf. Kampuni ya BAE Systems mwishoni mwa mwezi wa Februari ilitangaza kuwa iliwasilisha ndege 10 za kivita aina ya Eurofighter kwa Qatar baada ya kulikabidhi aina hiyo ya ndege mwaka uliopita.
8. Syria
Jeshi la Syria la Junta limekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi.
Kwa sasa haijulikani litafanya nini baada ya kuacha majukumu hayo.
7. Umoja wa Falme za Kiarabu UAE
Umoja wa Falme za Kiarabu uko mbele zaidi ya mataifa mengi ya Ghuba kwa uwezo wa kijeshi.
UAE inaongozwa na Bahrain, Kuwait, Oman na Qatar.
Jeshi la UAE limetajwa kuwa na uzoefu mkubwa na limepigana katika maeneo mengi, ikiwa ni pamoja na Afghanistan, Yemen na Libya.
UAE ina wastani askari 63,000.
6. Algeria
Algeria ni moja ya nchi zenye nguvu zaidi barani Afrika na moja ya nchi zinazoongoza katika Mashariki ya Kati.

Chanzo cha picha, Getty Images
6. Iraq
Iraq inasemekana kuwa moja ya nchi zenye nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati.
Lakini Iraq, iliyokuwa nchi ya nne kwa nguvu zaidi duniani wakati wa utawala wa Saddam katika miaka ya 1990, sasa iko katika hali ya kuzorota.
Bajeti ya kijeshi ya Iraq inakaribia dola bilioni 7 na inakua mwaka baada ya mwaka.
Idadi ya wanajeshi wa Iraq inasemekana kuwa 64,000.
Bajeti ya kijeshi ya Algeria ni dola bilioni 10 na inakua mwaka baada ya mwaka.
Idadi ya wanajeshi wa Algeria inakadiriwa kuwa 130,000.
5. Saudi Arabia
Saudi Arabia ni moja ya nchi zenye nguvu zaidi katika Mashariki ya Kati.
Nchi hii ni miongoni mwa nchi zinazotumia pesa nyingi zaidi kwenye jeshi.
Matumizi makubwa ya kijeshi ya Saudi Arabia yameifanya nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zenye vifaa bora zaidi katika eneo hilo.
Saudi Arabia inatumia dola bilioni 46 mwaka huu kwa jeshi. Idadi ya wanajeshi wake ni 227,000.
4. Israeli
Kwa vile Israel inazingirwa na nchi adui, haina budi kuboresha vikosi na zana zake.
Jeshi la Israel limetajwa kuwa mojawapo ya vikosi vilivyo na mafunzo bora na vyenye vifaa vya kutosha katika eneo hilo.
Idadi ya wanajeshi wa Israel ni 176,500 huku bajeti ya kijeshi ikiwa ni dola bilioni 18.5.
3. Misri
Jeshi la nchi kavu limesajiliwa na Wizara ya Ulinzi ya Misri kama la wanajeshi 920,000, wakati kikosi cha sasa ni 440,000.
Serikali ya Misri pia ina kikosi cha akiba cha askari 480,000, ambacho kinaweza kupigana usiku na mchana ikibidi.
Jeshi la wanamaji la Misri lina wastani vyombo 316 vya kivita.
2. Iran

Wanajeshi wa Iran wanakadiriwa kufikia 523,000 wakiwa na vitengo mbalimbali, kulingana na Taasisi ya Mafunzo ya Kimkakati yenye makao yake makuu nchini Uingereza.
Hiyo inajumuisha wanajeshi 350,000 wa kawaida, na angalau wanachama 150,000 wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi (IRGC).
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi wa Iran (IRGC) liliundwa miaka 40 iliyopita kwa ajili ya kutetea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
1. Uturuki
Uturuki, yenye wakazi milioni 82, inaajiri takriban watu milioni 42 na ina jumla ya wanajeshi 735,000.
Kwa mujibu wa The Global Fire Power, Uturuki ina takriban wanajeshi 355,000, huku kikosi cha akiba kikiwa na wanajeshi 380,000.
Kuna ndege 207 za kivita nchini Uturuki.
Vikosi vya ardhini vya Uturuki ni jeshi la saba lenye nguvu zaidi duniani.












