Chuo kikuu baada ya kustaafu: Mhitimu mkongwe anayeonyesha kuwa umri sio kikwazo kwa elimu

Dr Ruth Wilson, 88, with her husband Dr David Wilson (L) and Chancellor Dr Barry Catchlove who presented the graduation certificates

Chanzo cha picha, University of Sydney

Maelezo ya picha, "Kila kitu kilikuwa kipya kabisa kwangu , kwani mara ya mwisho nilipokuwa mwanafunzi ilikuwa mwaka 1979, nilipohitimu kwa mara ya kwanza " - Dkt Ruth (katikati)

Unapofikiria kuhusu chuo Kikuu, oicha unayoifiria akilini mwako huenda ni ya vijana wenye miaka ishirini na ushee au umri kama huo, ambao wanafuatilia kwa urahisi masomo ya Mhadhiri wao , au vijana ambao wamestarehe na kuchangamana katika maisha ya ujana.

Watu wenye umri wa uzee mahali kama Chuo kikuu mara nyingi huwa ni wahadhiri , maprofesa au waalalimu , na sio wanafunzi.

Lakini huku umri wa kuishi ukiongezeka kote duniani, baadhi ya wanafunzi watu wazima pamoja na wazee wanaamua kutumia miaka yao ya ziada kusoma katika chuo kikuu baada ya kustaafu.

Katika siku ya kimataifa ya Elimu ya Umoja wa Mataifa (24 Januari), BBC ilizungumza na wahitimu wanne wakongwe kutoka Indonesia, Canada, Brazil na Australia kufahamu ni kwanini wanaona elimu ni kitu cha kutafuta maisha yote.

Brazil: 'Tunaweza kusaidia bado kuifanya jamii kuwa bora zaidi'

Antonia Landgraf at the university

Chanzo cha picha, Antonia Landgraf

Maelezo ya picha, "Baada ya kustaafu na kuacha kazi katika Benki ya Brazil kwa miaka 10, sikukaa nyumbani ," anasema Antonia

Antonia Landgraf ana umri wa miaka 70 , na ni mwanafunzi.

Mstaafu kutoka Nova Xavantina katika eneo la kati la Brazil kwa sasa anasoma katia Chuo kikuu cha Mato Grosso.

"Baada ya kustaafu kazi katika Benki ya Brazil miaka,sikuweza kukaa nyumbani ,"aliiambia BBC.

"Mume wangu hufuga mifugo katika shamba na nilitaka kumsaidia. Lakini kujifunza mambo kunaufanya ubongo wangu ujishughulishe.

"Kwahiyo, kwanza , alisoma Jeografia na uhasibu," alisema.

Hiyo ilikuwa ni miaka 10 iliyopita. Tangu wakati huo alibadili na kusoma Kilimo.

Antonia Landgraf at the university

Chanzo cha picha, Antonia Landgraf

Maelezo ya picha, Marafiki wa Antonia walifikiri amechanganyikiwa wakati alipowaambia kwa mara ya kwanza kwamba anarudi kusoma chuo kikuu.

Wakati alipowaambia marafiki zake kwamba anataka kurudi chuo kikuu kusoma , walidhani amechanganyikiwa.

"Baadhi yao walisema ni kupoteza wakati, lakini nadhani watu wa rika langu bado wana mengi ya kutoa na wanaweza kusaidia kufanya jamii iwe bora kwa ujumla."

Lakini kurejea darasani kwa umri wake ilikuwa changamoto, na sio ajabu , alikuwa ndiye mwanafunzi mwenye umri mkubwa zaidi katika darasa lake.

Unaweza pia kusoma:

Australia: 'Elimu hukufanya uwe mdogo zaidi kwa umri'

Dr Ruth Wilson with her granddaughter, Dr Jessica Genauer

Chanzo cha picha, Dr Ruth Wilson

Maelezo ya picha, Mmoja wa mabinti wa Dkt Ruth na mjukuu wake wa kike Dkt Jessica Genauer, pia walipata PhD

Ruth Wilson, 88,alimaliza masomo yake ya shahada ya uzamifu- PhD mwezi Februari katika chuo kikuu cha Sydney, nchini Australia.

Kwa upande wake anasema "ulikuwa ni uzoefu wa kufurahisha sana", na wenye faida nzuri.

"Elimu inakufanya uwe mdogo zaidi kwa umri," Dkt Ruth anasema.

"Yunajifunza mengi sana ambayo ni mapya na ya kusisimua na unapata njia ambazo unaungana nazo katika maisha ya dunia ya sasa. Kwangu mimi ni kama nimepunguziwa miaka 20 ya maisha yangu."

Mama huyo wa watoto wanee ana wajukuu watano na vitukuu wanane, wenye umri wa kati ya miaka sita na 12 .

Canada: 'Hadithi za maisha bado zinaendelea kuandikwa'

Lois Kamenitz, 70

Chanzo cha picha, York University

Maelezo ya picha, "Mimi ni mtu wa kwanza katika familia yangu kwenda Chuo kikuu," " anasema Dkt Lois

Mapema mwaka huu alimaliza masomo yake ya shahada ya udaktari kutoka chuo kikuu cha Yoek nchini Canada, aifanya utafiti kuhusu wanafunzi wenye umri mkubwa .

Aliwafanyia utafiti wanawake kati ya 50 na 60, na kubaini kuwa wengi wao, walikuwa wamerudi shuleni kwa sehemu moja kwasabau Chuo kikuu kilikuwa kimepunguza ada ya mazomo kwa wanafunzi wenye umri mkubwa zaidi.

Laikini kwa Lois, kulikuwa na sababu nyingine muhimu:

"Mimi ni mtu wa kwanza katika familia yangu kwenda Chuo kikuu," aliiambia BBC.

Lois Kamenitz

Chanzo cha picha, York University

Maelezo ya picha, Wazazi wa Lois wambao walikuwa wahamiaji hawakuwa na uwezo wa kifedha wa kumsaidia kupata elimu ya juu, lakini alipata uwezo huo baadaye maishani mwake

Mtoto wa wahamiaji waliofanya kazi katika viwanda, wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kifedha wa kumsomesha , lakini baadaye fursa ilijitokeza katika maisha yake ya baadaye.

Lois anahisi kwamba kuwa mwanamke kulifanya mambo kuwa magumu zaidi kwake.

"Maisha na matarajio ya taaluma kwa mwanamke huwa sio ya uhakika kwasabau ya ujauzito, kuwatunza watoto, na majukumu ya kifamilia.

Nilidhani labda nilipowafanyia utafiti wanawake , ningepata baadhi ya majibu ya maswali yangu binafsi. Kwahiyo ndio maana nilifanya utafiti huu."

Lengo la utafiti wake , anasema lilikuwa ni kuvunja mwiko kwamba watu hawawezi au hawapaswi kwenda shuleni baadaye katika maisha yao.

'Kama tunaweza bado kusoma, hatupaswi kuacha'

La Ode with his teacher and a granddaughter

Chanzo cha picha, La Ode Muhammad Sidik

Maelezo ya picha, mmoja wa wanafunzi wa zamani wa La Ode Nadir La Djamudi (kushoto)alikuwa mwalimu wake na kumsaidia kufanya utafiti wake wa kukamilisha masomo yake.

Miaka miwili iliyopita, La Ode Muhammad Sidik, 87, alihitimu kutoka Chuo kikuu cha Muhammadiyah cha Buton, kilichopo katika kisiwa cha Indonesia cha Sulawesi.

Ilikuwa ni ndoto iliyotimia kwake, na bado anahamu ya kuendelea kupata elimu.

Mwalimu wa zamani wa shule alikuwa wakati wote maishani mwake akitaka kusoma Chuo kikuu, lakini kwa kuwa alikuwa na watoto tisa, ilibidi aweke ndoto zake kando kwanza.

Lakini mwaka 2012, mtoto wake mkubwa wa kiume alimhamasisha kurejea chuoni kusoma.

Alikuwa na umri wa miaka 78 ,alipojisajili masomo ya chuo kikuu. Lakini miaka miwili akiwa chuoni , aliugua. "Niliugua kwa mwaka mmoja na nusu na nilifanyiwa upasuaji wa tezi ," La Ode aliiambia BBC.

La Ode with family

Chanzo cha picha, La Ode Muhammad Sidik

Maelezo ya picha, "Kama tunaweza bado kusoma, hatupaswi kuzuiwa. Kama nina muda na fedha, ninataka bado kuendelea kumalisha shashada ya uzamili ,"anasema La Ode.

Lala, mmoja wa wajukuu wa La Ode ambaye alimsindikiza babu yake katika sherehe za kuhitimu, aliviambia vyombo vya habari kuwa babu yake hakuwahi kulalamika hata mara moja kuhusu masomo.

"Kila mara alihudhuria masomo, hata kama wakati mwingine alikuwa anaugua, alijitahidi kila mara kuendela kwenda chuoni ," Lala alisema.

Baada ya miaka saba, hatimaye, La Ode alipata Shahada yake ya kwanza kwa usaidizi wa mmoja wa wanafunzi wake, Nadir La Djamudi, ambaye alikuwa mhadhiri wake na alimsaidia kuandika utafiti wake wa mwisho. "Ninawashukuru sana-Niliwafundisha kuwa watu wema, na sasa ujuzi ule ulinirudia ," aliendelea kusema La Ode.

Fernando Duarte na Darul Amri wamechangia katika taarifa hii .