Varathalekshmi Shanmuganathan: Mwanamke wa miaka 87 wa Sri Lanka aliyetunikiwa Shahada ya uzamili

Chanzo cha picha, YORK UNIVERSITY
Katika umri wa miaka 87, Varadaletsumi Shanmuganathan kutoka nchiji Sri Lanka amefanikiwa kumaliza masomo yake ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu nchini Canada.
Ni mwanamke ambaye huzungumza taratibu neno moja baada ya jingine na ana uwezo wa kujumuisha mawazo yake kwa urahisi na anajivunia kuwa mhitimu mwenye umri mkubwa zaidi wa Chuo kikuu cha York nchini Canada.
Akiwa ni mzaliwa wa kijiji cha Velanai kilichopo katika wilaya ya Jaffna kusini mwa Sri Lanka, Varadaletsumi aliwafundish wanafunzi katika maabara nne duniani.
Maisha ya kusoma ya Varadaletsumi hayakuwa rahisi pamoja na kwamba ni mtu aliyependa sana elimu.
Ingawa alifaulu mtihani wa kati kwa alama nzuri, hakuweza kuendelea na elimu nchini Sri Lanka kwani kulikuwa na nafasi chache tu zilizotolewa kwa misingi ya jamii, jinsia na wanafunzi kutoka jamii za walio wachache.
Alikwenda Tamil Nadu kwa kuvuka bahari ili kuendelea na masomo yake.
"Mmoja wa waalimu wangu aliwashauri wazazi wangu kunipeleka katika chuo cha nchi ya ng'ambo. Kwahiyo wakanipeleka India ," anasema Varadaletsumi.
Alimaliza masomo yake ya shahada katika Chuo kikuu cha Chennai kilichopo katika jimbo la Tamil Nadu. Aliporejea Sri Lanka, aliwafundisha watoto historia ya India na Kiingereza katika shule moja ya kwao.
Alipokea stashahada ya elimu kutoka Chuo kikuu cha Ceylon, kulingana na taarifa ya Chuo kikuu cha York University
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Elimu ya mwanamke huyu ambaye alikuwa na shauku ya kufahamu ni nini atakachojifunza kwa siku zijazo, ilivurugwa na kuugua kwa baba yake.
Alilazimika kuchukua jukumu la kuitunza familia ya kwao. Baadaye akaolewa na mwalimu na kuondoka nchini Sri Lanka.
Aliwasili Canada mnamo mwaka 2004 baada ya kuishi katika nchi za Ethiopia, Sierra Leone, Nigeria na Uingereza.

Chanzo cha picha, YORK UNIVERSITY
Umri ulianza kumuandama, lakini nia ya kusoma ya Varadaletsumi haikuwahi kufifia. Aligundua kuwa kulikuwa na makubaliano kuhusu ada ya raia wenye umri mkubwa zaidi katika Chuo kikuu cha York.
Akiwa na umri wa miaka 85, alituma maombi ya kusoma shahada ya uzamili katika Chuo kikuu cha York, akisema, "Nilikuwa nikiwa na maslahi katika vita kuu vya II ya dunia katika Ceylon (baadaye iliitwa Sri Lanka) wakati nilipokuwa na umri wa miaka mitano.
Wakati Varathaletsumi alipoandika maombi alisajiliwa na Chuo kikuu cha York katika mwaka 2019. Alisimama darasani kama mwalimu, mjukuu wake wa kiume aliketi naye miaka 30 baadaye kusoma.
"Kwenda katika mazingira ya Chuo kikuu yalikuwa mabadiliko makubwa kwangu, kutembea kwenye mazingira ya chuo kikuu, kusoma katika maktaba, kutembea kama msichana mdogo mwenye umri wa kupevuka…nilipenda kila kitu ," anasema Varadaletsumi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Madereva wa teksi wanamchukulia kama profesa na huwa wanashangaa kufahamu kuwa ni mwanafunzi. "Najivunia sana kuwa mwanafunzi. Naamini katika maisha marefu ya kusoma.
''Wazee wanahitaji kusoma zaidi ya viwango vya ukomo vilivyowekwa na jamii kwao .", anasema.
Varadaletsumi alimaliza shahada yake ya uzamili akiwa na umri wa miaka 50 katika Chuo cha Birkbeck , London, iliyoitwa 'Mitizamo ya Watamili wa Sri Lanka katika Uingereza England kuhusu lugha'.
Aliamua kusoma katika Chuo kikuu cha York juu ya ujenzi wa amani na maridhiano bila ghasia katika Sri Lanka.
Varadaletsumi alitoa hotuba kuhusu (Sababu za vita vya kiraia, shuguli za amani, fursa ya amani nchini Sri Lanka) kwa njia ya video ya Zoom na kujibu maswali.
"Vita vinaweza kuwa vimeisha, lakini amani haitarudi hadi matatizo ya Watamil wa Sri Lanka yatakapotatuliwa, kugawana mamlaka na kugawana katiba italeta amani," alihitimisha.
Pia aliamua kuandika kitabu kwa misingi ya matokeo ya utafiti wake juu ya hali ya Sri Lanka baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na matarajio ya amani.
unaweza pia kusikiliza:













