Kwanini Waislam wanaobadili jinsia huibua mzozo? Dini na dunia - Taarifa za Ulimwengu wa Kiislamu

Nur Sajat ana jinsia zote mbili na alikwenda Hija. Lakini serikali ya Malaysia inamtambua kama mwanaume na kulingana na Sheria ya Kiislam, wanaumer hawezi kuvaa mavazi ya mwanamke

Kukamatwa kwa Nur Sajot

Mwishoni mwa mwaka jana, Maafisa wa uhamiaji waliripotiwa kufanya msako usio wa kawaida mjini Bangkok.

Aliyekamatwa alikuwa ni Nur Sajot Kamaruzzaman, mfanyabiashara mwanaume, mchangamfu mwenye umri wa miaka 36, raia wa Malysia ambaye alikuwa na ufuasi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Serikali ya Malaysia ilimshutumu kwa kuutusi Uislamu katika mwezi Januari mwaka ule na kudai arejeshwe nchini mwake mara moja.

Mashitaka haya yalitangazwa dhidi yake wakati huo huo.

Mfanyabiashara huyo anaweza kukabiliwa na kifungo cha miak mitatu gerezani.

Uhalifu wa Nur Sajot ulikuwa ni kuvaa vazi la kitamaduni refu na la mikono mirefu lililovaliwa na wanawake wa Malaysia katika sherehe za kidini mwaka 2018.

Ni mwanamke aliyebadili jinsia, kwahiyo Thailand ilimpatia hadhi ya ukimbizi na haikumzuwia kuomba uhamiaji katika nchi ya Australia.

Kulingana na maafisa wa Australia, Nur Sajot ni mwanaume na kulingana na Sheria ya Kiislam, mwanaume hawezi kuvaa kama kama mwanamke.

Kutoroka

Katika mahojiano na BBC akiwa Sidney Australia, Bw Nur , alisema kuwa hakuwa na chaguo lolote bali kutoroka nchi yake baada ya kushambuliwa na Idara ya masuala ya kidini ya Selangor- Selangor Department of Religious Affairs (ISA).

"Ilibidi nitoroke. Mbele ya wazazi wangu na familia, nilidhihakiwa, kupigwa , kusukumwa, na kufungwa mikono. Niliaibika na kukasirika. Nilijisalimisha kwao, lakini bado walinifanyia ukatili."

"Labda walifikiria nimekamatwa, kupigwa na kupigwa mateke, kwasababu waliniona kama mtu aliyebadili jinsia. Kuna hisia miongoni mwa watu waliobadili jinsia pia. Tuna haki ya kuishi maisha yetu kama watu wa kawaida ."

"Mkanganyiko wa jinsia "

Nur Sajot ni mjasiliamali binafsi mwenye mafanikio

Anasema alianza kujinadi mwenyewe kwenye mitandao ya kijamii miaka saba iliyopita.

Pia alitengeneza vipodozi vya mwili wake na madawa mbadala ya afya yenye chapa yake.

Kutokana na muonekano wake na jumbe za kufurahisha kwenye mitandao ya kijamii, alipata maelfu ya wafuasi na akawa mtu maarufu katika taifa lake. Halafu maswali kuhusu jinsia yake yakaanza.

Siri ya wazi

Kusema kweli haikuwa siri hata kidogo. Katika mwaka 2013 Nur Sajot alishiriki katika mashindano maarufu ya urembo ya watu walibadili jinsia zao yaliyofanyika nchini Thailand na akashinda tuzo kwa densi yake.

Kile kinachoishangaza Malasyia ni kwamba pia ni Muislam aliyeshika dini na amekuwa akituma picha za Waislam waliovaa hijab.

Amekuwa akiwaambia wale waliomuuliza kwamba alizaliwa na jinsia mbili- ya kike na ya kiume.

Katika Uislam, wale waliozaliwa na hali ya kuwa na jinsia mbili wanavumiliwa kuliko watu waliobadili jinsia zao.

Katika mwaka 2017, Nur Sajot alitagaza kwamba ana maumbile ya mwanamke kamili, na ripoti ya daktari ilithibitisha hili.

Uchunguzi

Maafisa wameamua kuchunguza. Idara ya Maendeleo ya Dini ya Kiislam, JAKIM, ilisema ilihitaji kuhakikisha kwamba alizaliwa na jinsia mbili.

Waliamua kumsaidia Nur Sajot kwa "mkanganyiko wa jinsia ."

Mwaka jana, picha za Nur Sajot akiwa amevalia gauni la sala wakati wa hija Macca akiwa pamoja na watu wa familia yake ziliibua utata hata zaidi, ambao umekosolewa na Waislam mahafidhina.

Baadaye aliomba msamaha kwa sakata hiyo, lakini mwaka mmoja baadye kesi imefunguliwa dhidi yake.

"Nilipokuwa katika Ardhi Takatifu, nilitaka kujiuliza binafsi swali…Labda haikuwa bure kwamba nilizaliwa hivyo? " Alisema Nur Sajot. "

Maafisa walisema nini?

BBC iliitaka Wizara ya masuala ya Kidini ya Malasyia kutoa kauli yake juu ya kesi ya Nur Sajot , lakini haijapata jibu.

Mwezi Septema, Waziri wa wizara ya Masuala ya kisini wa Malaysia Idris Ahmad alisema , "Kama anataka kuja kwetu, wacha akiri kwamba anafanya kitu fulani ambacho ni kosa. Kama yuko tayari kurejea katika hali yake halisi ya maumbile yake, sio tatizo. Hatutaki kumuadhibu, tunataka kumuelimisha ."

Tulimuuliza Muhammad Asri Zainul Obidin, mshauri mkuu wa masuala ya Uislam katika Perlis, iwapo Waislam wa Malasyia wanaweza kuwakubali watu waliobadili jinsia

"Kwangu mimi, sula la Sajat ni la kipekee," alisema, na huwezi kwenda kwenye maliwato ya wanawake. "

Malaysia ina mfumo wa aina mbili ambapo familia na na maadili ya Waislam, ambao ni asilimia 60 ya wakazi wake katika majimbo 13 na maeneo matatu ya shirikisho, yanatawaliwa kwa sheria ya Kiislamu (Sharia).

Hii inasababisha kuendelea kwa tatizo kwa wapenzi wa jinsia moja, waliobadili jinsia na wanaohisi kutokuwa na jinsia zinazoendena na muonekano wao wa - LGBT

"Sharia huwalenga watu LGBT kila jimbo," alisema Nisha Ayub, mwanaharakati aliyebadili jinsia ambaye wakati mmoja alifungwa gerezani kwa kuvaa nguo za wanawake.

"Na kwasababu ya Sharia, kuna wanasiasa, viongozi, taasisi za kidini ambao hutoa kauli hasi kuhusu jamii yetu. Na hilo linasababisha mazingira hatari san ana yasiyo ya amnani kuishi kwetu."

"Mchakato wa kumuingiza mtu katika Uislamu" ni vugu vugu.

Lakini hili halijawa hivi mara kwa mara.

"Malaysia wakati mmoja iliwavumilia sana, watu waliobadili jinsia,"

"Mchakato wa kumuingiza mtu katika Uislamu" ni vugu vugu.

"Wakati ule, ungeweza kuona wazi jinsi walivyoishi miongoni mwa familia zetu, katika maeneo yetu, na katika maisha ya kijamii. Lakini kwa zaidi ya miaka 30, tumekuwa tukitaka sera ya Uislamu . "

Alisema Rozana Isa, muasisi Kikundi cha Madada wa Kiislamu- Sisters of Islam, kikundi kinachofanya kazi katika Uislamu na kinachomuunga mkono Nur Sajot.

"Wakati ule, ungeweza kuona wazi jinsi walivyoishi miongoni mwa familia zetu, katika maeneo yetu, na katika maisha ya kijamii. Lakini kwa zaidi ya miaka 30, tumekuwa tukitaka sera ya Uislamu . "

Uislamu sio dini rasmi la Shirikisho la Malaysia, lakini inaonekana kama ni ishara muhimu ya Malaysia, kikundi kikubwa zaidi cha kikundi cha kijamii.

Ili kushinda uchaguzi , vyama vya kisiasa, vinahitaji kupata uungaji mkono zaidi katika wilaya za Malaysia.

Katika maeneo hayo, hatahivyo, watu bado wana mawazo ya kidini ya kihafidhina.

Vyama vinatoa ahadi hapa kwamba vitalinda sana maadili ya Kiislamu. Hatahivyo, Nisha Ayub alisisitiza kuwa licha ya maoni ya Kiislamu, bado ni wajibu wa serikali kulinda haki za watu waliobadili jinsia.

Nur Sajot anawakosa sana watoto wake wawili, wakiume na wa kike aliowaasili ambao sasa wanatunzwa na wazazi wao nchini Malaysia.

Lakini sasa ana fursa ya kuushirikisha umma uzoefu wa maisha yake na watu wengine waliobadili jinsia nchini Australia.

Rosana Isa,Muaisisi wa Kikundi cha Madada katika Uislamu, anatoa wito kwa Wamalasyia ''kuwa wazi zaidi na wenye akili katika mitandao ya kijamii."

"Ni kwanini tunamlaumu Sajjad sana? Hajamdhuru yeyote kwa jumbe zake au akiwa Macc. Tunahitaji kujidhibiti wenyewe kuliko kuwadhibiti watu wengine."