Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ethiopia: Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
Mzozo katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia umegeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinatishia kusambaratisha nchi hiyo na kuyumbisha eneo lote.
Waasi wameanzisha mashambulizi eneo la kusini kuelekea mji mkuu wa shirikisho, Addis Ababa, na kumfanya Waziri Mkuu Abiy Ahmed - mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na kanali wa zamani wa Luteni - kuliongoza jeshi la taifa kwenda vitani.
Ongezeko hilo la ghasia limesababisha raia wa mataifa ya magharibi na wafanyakazi wa kigeni wasio wa lazima wa Umoja wa Mataifa (UN) kuondoka nchini, bbaada ya usalama kuwa mbaya.
Baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1970 na 1980, Ethiopia ilikuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi barani Afrika na nguzo ya utulivu wa kikanda.
Lakini ghasia zimesambaa kutoka ngome ya waasi ya Tigray ambako mapigano yalizuka, hadi maeneo jirani ya Amhara kaskazini -magharibi na Afarkaskazini -mashariki.
Ushindi wa hivi majuzi wa vikosi vya muungano katika uwanja wa vita haujafanya chochote kuzima hofu ya kuongezeka kwa mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya watu na maelfu ya wengine kuyahama makazi yao.
TPLF 'kurejea mara ya pili'
Waasi wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) wanasema uvamizi wao kuelekea kusini unalenga kushinikiza serikali kuondoa vikosi vyake eneo Tigray ambako mawasiliano na misaada ya kibinadamu imedhibitiwa.
Hata hivyo, utawala wa Abiy umewashtumu waasi kwa kueneza vurugu na kutaka mabadiliko ya utawal kwa nguvu, na hivyo kuzua hofu kwamba TPLF ina nia ya kurejea madarakani.
Chama cha TPLF kilitawala ngome ya kisiasa ya Ethiopia kwa miaka 27 baada ya kuanzisha uasi kama huo mwaka 1991 dhidi ya serikali ya wakati huo ya kikomunisti.
Utawala wao ulisababisha uwekezaji mkubwa katika miundombinu, ambayo ilikuza uchumi wa Ethiopia, lakini ilikumbwa na ukandamizaji wa kijamii na kisiasa.
Hali ambayo ilitibua maandamano makubwa dhidi ya serikali na kumweka madarakani Bw. Abiy mnamo Aprili 2018, ambapo alianzisha mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiusalama.
Katika mapambano yake dhidi ya serikali, TPLF imeunda miungano ili kuongeza nguvu zake za mapigano na kuongeza sifa zake baada ya kuungwa mkono na vyama kadhaa vyenye mfungamano wa kikabila vinavyompinga waziri mkuu.
Kuongezeka kwa wito wa silaha
Vita hivyo awali vilikuwa kati yawapiganaji wa TPLF na jeshi la muungano, likisaidiwa na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali kutoka Amhara na vikosi vya Eritrea.
Viongozi wa TPLF walifurushwa ndani ya wiki kadhaa, lakini uvamizi uliendelea katika vijijin vya Tigray,kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu tayari.
Zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wa eneo hilo - takriban watu milioni 5.2 - wanahitaji msaada wa dharura, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.
Maelfu wametorokea nchi ya Sudan - yenyewe inakabiliwa na mapinduzi ya kijeshi.
Waasi waliweka wakati wa kuuteka tena mji mkuu wa Tigray Mekelle mwezi Juni, wakati Ethiopia ilipokuwa ikisubiri matokeo ya uchaguzi, ili kudhoofisha uhalali wa Abiy.
Wakati wapiganaji wa waasi wakivamia maeneo ya nje ya Tigray, wanamgambo kutoka majimbo yenye ufungamano wa kabila la Ethiopia, zikiwemo Somalia na Oromia, waliingizwa kwenye mapigano.
Wito wa mara kwa mara wa Waziri Mkuu Abiy kwa umma kuchukua silaha ili kuzuia waasi kusonga mbele ulihalalisha zaidi matumizi ya nguvu.
"Ni jukumu letu kwa pamoja kufa kwa maslahi ya Ethiopia. Kwa hiyo, watu wetu lazima waache mambo yao binafsi kwa sasa na wajipange kwa njia halali na watoke wakiwa na silaha na uwezo wowote wa kuwafukuza na kuwazika magaidi wa TPLF, dhamira ya uharibifu," Abiy alisema katika taarifa ambayo ilifutwa na Facebook tarehe 4 Novemba kwa madai ya uchochezi.
Nyuso za zamani, miungano mipya new alliances
Matarajio ya Bw Abiy ya utaifa yamejaribu mfumo wa utawala wenye utata wa kikabila wa Ethiopia, ambao uliwekwa katika katiba ya 1994. Licha ya kutaka kuyapa makumi ya makabila uhuru zaidi, baadhi ya jamii za wachache zimeendelea kushinikiza uhuru tangu Abiy aingie madarakani.
Mwezi Agosti, TPLF ilianzisha muungano wa kijeshi na waasi wa Oromo Liberation Army (OLA) kutoka kabila lenye watu wengi zaidi la Ethiopia ambalo lilikuwa limetengwa kwa muda mrefu na serikali zilizopita.
Bw Abiy alikuwa mwanachama wa kwanza wa jamii ya Oromo kushikilia wadhifa wa waziri mkuu.
Lakini baada ya serikali kuwazuilia wapinzani wakuu wa kisiasa kutoka kwa jamii ya Oromo, OLA imekuwa mpinzani mkubwa wa waziri mkuu.
Muungano wa OLA na TPLF ulichochea kuendelea kwa wapiganaji wa waasi kuteka miji muhimu ya Amhara - ikiwa ni pamoja na Kemise, Dessie na Kombolcha - walipokuwa wakielekea mji mkuu.
Mapambano hayo yaliendelea kwa kasi zaidi na kuungwa mkono na mirengo saba ya upinzani ya kisiasa na waasi, ambao wengi wao wanaishi ugenini na kutoka makabila madogo, ambao wametishia kumuondoa waziri mkuu madarakani.
Serikali ya Ethiopia imetangaza kukomboa tena baadhi ya miji iliyochukuliwa na waasi.
Wito wa majadiliano
Mnamo tarehe 7 Novemba, mjumbe wa Umoja wa Afrika (AU), Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, alielezea matumaini kwamba pande zinazozozana ziko tayari kwa mazungumzo.
Lakini waasi na Waziri Mkuu Abiy wanaendelea kuzozana wao kwa wao.
Kwa sasa, shinikizo la kikanda limepungua na simu za mazungumzo ya kimataifa zimepuuzwa kwa kuingilia masuala ya ndani.
Kutoegemea upande wa AU, yenye makao yake makuu nchini Ethiopia, yenyewe kumehojiwa, baada ya ujumbe kwenye akaunti yake rasmi ya Twitter mwezi Agosti,, kukosoa wito wa Marekani wa mazungumzo. Ujumbe huo ulifutwa.
Maandamano dhidi ya Marekani na mataifa mengine ya magharibi na vyombo vya habari vya kigeni yamekuwa yakiongezeka mjini Addis Ababa na miongoni mwa jamii za Waethiopia wanaoishi nje ya nchi.
"Vikosi vinavyojaribu kuamuru nchi yetu na kutuongoza kupitia propaganda za kiuchumi, kidiplomasia na vyombo vya habari au vita vya kisaikolojia vitashindwa kwa nguvu moja ya Waethiopia," Bw Abiy alisema mnamo Novemba.