Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wanawake 100 wa BBC 2021: Nani yuko kwenye orodha mwaka huu?
BBC imefichua orodha yake ya wanawake 100 wenye hamasa na ushawishi kutoka kote ulimwenguni kwa mwaka wa 2021.
Mwaka huu Wanawake 100 inaangazia wale wanaogonga 'kuweka upya' - wanawake wanaotekeleza wajibu kuunda upya jamii yetu, utamaduni wetu na ulimwengu wetu.
Miongoni mwa walio kwenye orodha hiyo ni Malala Yousafzai, mshindi wa mwenye umri wa chini zaidi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa Samoa Fiamē Naomi Mata'afa, Prof Heidi J Larson, anayeongoza Mradi wa Vaccine Confidence Project, na mwandishi maarufu Chimamanda Ngozi Adichie.
Wanawake kutoka Afghanistan wanasheheni nusu ya orodha ya mwaka huu, baadhi yao wakionekana kwa majina bandia na bila picha kwa usalama wao wenyewe.
Kuibuka tena kwa Taliban mnamo Agosti 2021 kumebadilisha maisha ya mamilioni ya Waafghanistan - huku wasichana wakipigwa marufuku kupata elimu ya sekondari, wizara ya masuala ya wanawake ikivunjwa, na wanawake katika hali nyingi kuambiwa wasirudi kazini. Orodha ya mwaka huu inatambua upeo wa ushujaa wao na mafanikio yao wanapoweka upya maisha yao. BBC imefichua orodha yake ya wanawake 100 wenye hamasa na ushawishi kutoka kote ulimwenguni kwa mwaka wa 2021.
Je Wanawake 100 walichaguliwaje?
Timu ya BBC 100 Women ilitayarisha orodha fupi kulingana na majina waliyokusanya na kupendekezwa na mtandao wa BBC wa timu za lugha za Idhaa ya Dunia. Tulikuwa tunatafuta wagombeaji ambao walikuwa wamegonga vichwa vya habari au walioshawishi hadithi muhimu katika muda wa miezi 12 iliyopita, pamoja na wale ambao wana hadithi za kusisimua za kusimulia, walipata jambo muhimu au walioshawishi jamii zao kwa njia ambazo hazingegonga vichwa vya habari. Mkusanyiko wa majina ulitathminiwa dhidi ya kauli mbiu ya mwaka huu - wanawake ambao wanagonga 'kuweka upya', wakitelekeza jukumu lao kuunda tena ulimwengu wetu baada ya janga la Covid 19 kulazimisha wengi wetu kutathmini upya jinsi tunavyoishi. Pia ilipimwa kwa uwakilishi wa kikanda na kutopendelea, kabla ya majina ya mwisho kuchaguliwa.
Mwaka huu BBC 100 Women walifanya uamuzi ambao haujawahi kushuhudiwa wa kutenga nusu ya orodha hiyo kwa wanawake kutoka nchi moja - Afghanistan. Matukio ya hivi majuzi nchini humo yamegonga vichwa vya habari na kuwaacha mamilioni ya Waafghanistan wakihoji mustakabali wao, huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakizungumza kwa hofu kwamba uhuru wa wanawake unaweza kuminywa kwa mustakabali unaoonekana chini ya Taliban. Kwa kutoa nusu ya orodha hiyo kwa wanawake wanaotoka au kufanya kazi nchini, tulitaka kuangazia ni wangapi kati ya wanawake hao wamelazimika kutoweka katika maeneo ya maisha ya umma, na pia kuzitoa sauti za wale ambao wanazidi kunyamazishwa au ambao ni sehemu ya mpya ya raia wa Afghanistan walio nje ya nchi .
Mnamo tarehe 3 Disemba, Taliban walitoa amri kwa jina la kiongozi wao mkuu kuziagiza wizara "kuchukua hatua kali" juu ya haki za wanawake. Amri hiyo inaweka sheria zinazosimamia ndoa na mali kwa wanawake, ikisema kwamba wanawake hawapaswi kulazimishwa kuolewa na wasionekane kama "mali". Lakini tamko hili limekosolewa kwani linashindwa kutaja elimu ya sekondari ya wasichana na kupunguzwa haki za wanawake za kuajiriwa.
Baadhi ya wanawake wa Afghanistan katika orodha hiyo hawajajulikana majina yao ili kuwalinda wao na familia zao, kwa ridhaa yao na kufuata Sera ya Uhariri ya BBC na miongozo ya usalama.
Waliochangia
Imeandaliwa na kuhaririwa na Valeria Perasso, Amelia Butterly, Lara Owen, Georgina Pearce, Kawoon Khamoosh, Haniya Ali, Mark Shea. BBC 100 Women editor: Claire Williams. Production by Paul Sargeant, Philippa Joy, Ana Lucía González. Development by Ayu Widyaningsih Idjaja, Alexander Ivanov. Design by Debie Loizou, Zoe Bartholemew. Illustrations by Jilla Dastmalchi.
.
Haki Miliki za Picha : Fadil Berisha, Gerwin Polu/Talamua Media, Gregg DeGuire/Getty Images, Netflix, Manny Jefferson, University College London (UCL), Zuno Photography, Brian Mwando, S.H. Raihan, CAMGEW, Ferhat Elik, Chloé Desnoyers, Reuters, Boudewijn Bollmann, Imran Karim Khattak/RedOn Films, Patrick Dowse, Kate Warren, Sherridon Poyer, Fondo Semillas, Magnificent Lenses Limited, Darcy Hemley, Ray Ryan Photography Tuam, Carla Policella/Ministry of Women, Gender and Diversity (Argentina), Matías Salazar, Acumen Pictures, Mercia Windwaai, Carlos Orsi/Questão de Ciência, Yuriy Ogarkov, Setiz/@setiz, Made Antarawan, Peter Hurley, Jason Bell, University of Sheffield Hallam, Caroline Mardok, Emad Mankusa, David M. Benett/Getty, East West Institute Flickr Gallery, Rashed Lovaan, Abdullah Rafiq, RFH, Jenny Lewis, Ram Parkash Studio, Oslo Freedom Forum, Kiana Hayeri/Malala Fund, Fatima Hasani, Nasrin Raofi, Mohammad Anwar Danishyar, Sophie Sheinwald, Payez Jahanbeen, James Batten.
Wanawake 100 ni nini?
BBC 100 Women huwataja wanawake 100 wenye ushawishi na kutia moyo kila mwaka duniani kote. Tunatengeneza filamu za hali halisi, makala na mahojiano kuhusu maisha yao - hadithi zinazowaweka wanawake katikati.
Fuata BBC 100 Women kwenye Instagram, Facebook ana Twitter. Jiunge na mazungumzo ukitumia #BBC100Women.