Kwa nini wananchi wa Gambia hawataacha kupiga kura kwa kutumia gololi

A voter in Gambia holding up a marble used to vote - archive shot

Chanzo cha picha, AFP

Katika mfululizo wa makala kutoka kwa waandishi wa Afrika, mwanahabari mwenye asili ya Sierra Leon-Gambia Ade Daramy anasema Gambia imeshuhudia kushamiri kwa demokrasia lakini mfumo wake wa ajabu wa uchaguzi bado haujabadilika..

Short presentational grey line

Wananchi wengi wa Gambia ninaowajua wanajivunia mfumo wao wa kipekee wa kupiga kura.

Watakapopiga kura Jumamosi tarehe 4 Desemba kumchagua rais, karatasi za kupigia kura hazitatumika.

Badala yake, akifika katika kituo cha kupigia kura, na baada ya kitambulisho chake kuthibitishwa, mpiga kura ataelekezwa kwenye safu ya ngoma zilizopakwa rangi za vyama vya wagombea tofauti.

Kinachochomoza kutoka juu ya kila ngoma ni bomba ambalo mpiga kura atapenyeza gololi aliyokabidhiwa na afisa wa uchaguzi.

Maafisa wa upigaji kura wakiangalia mihuri kwenye ngoma za kupigia kura katika kituo cha kupigia kura huko Banjul tarehe 1 Desemba 2016.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Katika chaguzi zilizopita, kama ule wa 2016, kulikuwa na ngoma tatu katika kila kituo cha kupigia kura ili kuwakilisha wagombea watatu.

Inatoa mlio wa kengele ili viongozi waweze kusikia kama kuna mtu yeyote atajaribu kupiga kura zaidi ya mara moja.

Wakati shughuli ya kupiga kura inapokamilishwa, gololi kutoka kwa kila pipa zinahesabiwa na kujumuishwa - kama inavyofanywa karatasi za kupiga kura.

Njia hii ya upigaji kura ilianzishwa baada ya uhuru mwaka 1965 kwa sababu ya kiwango cha juu cha watu wasiojua kusoma na kuandika nchini Gambia.

Marekebisho kadhaa yamefanywa tangu Yayha Jammeh kuondoka madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa rais mwaka 2016.

Hali ngumu ingeepukwa

Baadhi ya maafisa wa uchaguzi kisiri walikuwa na matumaini kwamba mfumo wa upigaji kura kupitia gololi ungelikuwa moja ya mabadiliko hayo.

Walikuwa wanahoji kwa misingi ya kupanuka kwa nafasi ya kidemokrasia na uwezekano wa wagombea wengi kushiriki katika chaguzi zijazo, hivyo basi mfumo wa kupiga kura kwa kutumia gololi na ngoma unaweza kuwa mgumu sana na wa kuchosha.

Zamani ni ngoma tatu tu zilihitajika katika kila kituo cha kupigia kura.

Wakati wa miaka 22 ya Bw Jammeh mamlakani ilionekana kuwa na umuhimu mdogo katika kugombea.

Kwa kweli Gambia imekuwa na marais watatu tu katika historia yake.

Bodi kama hizi hutumiwa kuhesabu marumaru

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bodi kama hizi hutumiwa kuhesabu gololi

Bw Jammeh aliingia mamlakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1994, na kumuondoa madarakani kiongozi wa uhuru Dawda Jawara.

Waangalizi wengi wanaafiki kuwa uchaguzi pekee ambao Bw Jammeh alishinda kwa haki ulikuwa wa mwaka wa 1996, wakati bado kulikuwa na kipindi cha fungate baada ya mapinduzi na kabla ya kuanza uongozi wake wa kimabavu.

Chaguzi zilizofuata zilichakachuliwa kwa maslahi yake, na kushindwa kwake 2016 kulionekana kumshangaza yeye na mrithi wake Adama Barrow.

Kwa kiasi kikubwa kinyang'anyiro kilikuwa mbio za farasi wawili, huku Bw Barrow akiwa mgombea wa maridhiano aliyechaguliwa na muungano wa vyama vya upinzani. Mgombea wa tatu, Mama Kandeh, alipata asilimia 17 ya kura.

Rais Barrow anagombea tena, wakati huu kwa tikiti ya chama chake kipya.

Wakati mmoja ilionekana kwamba angekabiliana na wagombea 22 - hali ya kutisha kwa tume ya uchaguzi kutokana na mfumo wa kupiga kura kwa kutumia gololi na ngoma bado ipo kwani hakukuwa na utashi wa kisiasa wa kuubadilisha.

Kwa bahati nzuri wagombea hao tangu wakati huo wamepunguzwa hadi sita - bado ni wengi kwa nchi yenye takriban watu milioni 2.2.

Kuondoka kwa Jammeh

Kujitokeza kwa wagombea wote hawa ni ushahidi wa jinsi nchi ilivyobadilika, na bado inabadilika.

Hapo zamani, watu walikuwa wakiogopa sana kushindana dhidi ya Bw Jammeh au waliona kuwa ni kupoteza muda.

Ade Daramy
A Daramy
A comedian called Wagan has a weekly TV show in which he pokes fun at all the main politicians, including the president - something unthinkable five years ago"
Ade Daramy
Journalist
1px transparent line

Siku hizi, katika kile kinachojulikana mara kwa mara kama "Gambia Mpya", hofu hiyo imepita na uhuru wa kujieleza umeshamiri.

Mchekeshaji kwa jina Wagan ana kipindi cha televisheni cha kila wiki ambapo huwakejeli wanasiasa wakuu akiwemo rais - jambo ambalo halikufanyika miaka mitano iliyopita.

Waandishi wa habari wanatoa maoni yao juu ya jambo lolote bila hofu ya kuchukuliwa hatua, kuteswa au kuuawa kama ilivyotokea chini ya Bw Jammeh.

Baadhi ya ukatili huu ulifichuliwa wakati wa Tume ya Ukweli, Maridhiano (TRRC), iliyosikiliza ushuhuda kutoka kwa karibu watu 400 kuanzia Januari 2019 hadi Mei 2021.

Iliwasilisha ripoti yake ya mwisho wiki iliyopita - rais sasa ana miezi sita kuijibu na mapendekezo yake.

Utawala wa miaka 22 wa Yahya Jammeh umechunguzwa na Tume ya Ukweli, Maridhiano (TRRC)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Utawala wa miaka 22 wa Yahya Jammeh umechunguzwa na Tume ya Ukweli, Maridhiano (TRRC)

Hii ina maana kwamba itaangukia kwa yeyote atakayeshinda tarehe 4 Desemba kuanza mchakato halisi wa kuponya majeraha yaliyoachwa nyuma na uongozi wa Bw Jammeh.

Hata kutoka uhamishoni nchini Equatorial Guinea, rais huyo wa zamani anajaribu kutumia ushawishi wake katika uchaguzi.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 56 anasalia kuwa kiungo cha migawanyiko - ilivyodhihirishwa na mzozo kati yake na chama alichoanzisha, Alliance for Patriotic Reorientation and Construction (APRC).

Imeingia katika muungano rasmi na chama cha Rais Barrow - kiasi cha kukerwa na Bw Jammeh, ambaye alitoa rekodi za sauti zinazomuunga mkono Bw Kandeh badala yake.

Lakini kivuli halisi ambacho kinagubika Gambia, kama ulimwengu wote, ni janga la Covid.

Nchi iliyo na fukwe zake nzuri na wanyamapori wengi hutegemea sana utalii na iliathiriwa sana na vizuizi vya kusafiri. Watu wengi walipoteza kazi.

Sasa watalii wameanza kuzuru nchi hiyo lakini mengi zaidi yanahitajika ili kurejea katika viwango vya kabla ya Covid.

Kukuza uchumi ni changamoto kubwa kwa yeyote atakayeshinda urais

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kukuza uchumi ni changamoto kubwa kwa yeyote atakayeshinda urais

Hata kabla ya viruis vya corona , nchi ilichangia idadi kubwa ya wahamiaji wanaotaka kuingia Ulaya ukilinganisha na ukubwa wake.

Mengi, ingawa si yote, yanatokana na ukosefu wa ajira.

Kwa yeyote atakayepata gololi nyingi zaidi tarehe 4 Disemba, kuendeleza na kubuni fursa nchini Gambia ili kuifanya ivutie zaidi kwa wakazi sio tu watalii itakuwa changamoto kubwa zaidi.

Presentational grey line

Wagombea sita katika kinyang'anyiro hicho:

  • Adama Barrow (National People's Party) - Rais aliye madarakani
  • Ousainou Darboe (United Democratic Party) - wakili ambaye alihudumu kwa muda mfupi kama makamu wa rais wa Bw Barrow. Alikuwa sehemu ya muungano uliomwangusha Bw Jammeh na anagombea kwa mara ya tano
  • Essa Mbye Faal (Mgombea Huru) -wakili na wakili kiongozi wa zamani katika TRRC iliyohitimishwa hivi karibuni. Anagombea urais kwa mara ya kwanza
  • Mama Kandeh (Gambia Democratic Congress) - Alikuwa wa tatu katika uchaguzi wa 2016, anaungwa mkono na Bw. Jammeh
  • Abdoulie Ebrima Jammeh (National Unity Party) - mwalimu wa zamani aliyewahi kuongoza mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo. Anagombea kwa mara ya kwanza
  • Halifa Sallah (People's Democratic Organisation for Independence and Socialism) - mbunge anagombea kwa mara ya tano
Presentational grey line