Tutawahi kupata haki?-Raia wa Gambia

Maelezo ya video, Tutawahi kupata haki?-Raia wa Gambia

Wananchi wa Gambia bado wanasubiri haki itende dhidi ya madhila waliotendewa wakati wa utawala uliopita.

Ni miaka minne sasa tangu Yahya Jammeh ,kiongozi aliyetawala Gambia kwa miaka 22 kukimbia nchi yake.

Utawala wa rais aliyepita unashutumiwa kufanya mauji , kuwatesa watu na kuwaweka vizuizini au mateka.

Ingawa Jammeh alikanusha kuhusika katika madai hayo na kukataa kutoa ushirikiano katika tume ya maridhiano iliyoundwa ambayo inafanya uchunguzi wa unyanyasaji huo.

Hii ni mara ya pili kwa tume hiyo kuchelewa kutoa ripoti kuhusu kesi hiyo , jambo linalowapa hofu wahanga wa mateso hayo