Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini Ford iliharibu gari lake lililotengenezwa mwaka 1941?
'Ford-Tee' ndilo gari la kwanza lililotengenezwa kwa wingi duniani. Magari haya yalitengenezwa na Henry Ford. Linashikilia rekodi ya magari mengi zaidi duniani.
Kiwanda kilichoanzishwa na raia wa Marekani Henry Ford kilileta mageuzi makubwa katika uzalishaji wa magari dunia nzima.
Mapema karne ya ishirini Henry Ford aliifanya sekta ya usafiri kuwa soko kubwa.
Miaka 100 baadaye magari haya yaliyokuwa yakitumia mafuta na kutoa gesi ya kaboni, yanadhaniwa kuchangiaongezeko la joto duniani na mabadiliko ya hali ya hewa.
Lakini pia ni watu wachache wanafahamu kuwa mtu aliyesababisha kuwepo mbio za kunudwa magari pia ndiye muasisi katika masuala ya mazingira.
Gari la Soya
Kwa sababu miaka ya 1930, Ford ndiyo ilikuwa ya kwanza kuzalisha na kutumia bioplastki.
Bioplastic ni aina ya plastiki inayoundwa kutokana na mimea na haidrokaboni. Kando na hilo ni kwanba yaweza kuharibiwa.
Kando na kuunda bioplastiki, Ford alikuwa mtu kwa kwanza kutengeneza gari kutokana nayo.
Gari likapewa jina 'Soybean car' au 'Soybean Auto'. Ford akalitambulisha kwa umma mnamo mwaka 1941.
Ford anadai kuwa plastiki ina nguvu mara kumi zaidi kuliko chuma. Kila kifaa alichokitengeneza kilifanyiwa majaribio ya kutumia shoka.
Mkulima, mjasiriamali
Henry Ford alitaka kutengeneza maelfu ya sehemu za magari kwa kutumia nyenzo hii, lakini hakufanikiwa kufanya hivyo.
Kwa kweli, gari la soybean halikufanikaiwa kufika sokoni. Gari moja lililoundwa pia liliharibiwa. Hakuna gari lingine kama hilo.
Swahili sasa ni kwa nini gari safi la Henry Ford halikuundwa na ni kwa nini halikufanikiwa?
Kulingana na kituo cha utafiti cha Benson, mfanyabiashara Henry Ford alikua kwenye shamba moja huko Michigan, Alikuwa kila mara anafikiri jinsi ya kuzijumuisha setka za viwanda na kilimo.
Gari la paneli ya plastiki
Ford ikaanzisha mahabara za kujaribu kugundua matumizi ya mazao ya kilimo katika viwanda kama vile soya, mahindi, ngano na katani.
Wazo la kuunda gari kutoka kwa plastiki iliyotengenezwa kutokana na mimea haikutimiza lengo la Ford la kuunganisha sekta za viwanda na kilimo bali pia manufaa mengine.
Kulingana na kituo cha utafiti cha Benson, Ford anaamini gari lililotengenezwa kwa paneli za plastiki liko salama kuliko lile linalotengenezwa kutokana na chuma.
Sababu nyingine ya kulinda gari hili ni kwamba badala ya gari hili kuharibiwa wakati wa ajali, linaweza kupinduka. Vita vya pili vya dunia vilianza mwaka 1939 na kulikuwa na uhaba wa chuma wa dunia nzima.
Tunafahamu kipi kuhusu gari la soya?
Wakati wa mahojiano na New York Times mwaka 1941, wakati akilitambulisha gari lake, Henry Ford alisema gari lililoundwa kutoka kwa plastiki litapunguza mahitaji ya chuma nchini Marekani kwa asilimia 10.
Kulingana na kituo cha utafiti cha Benson, taarifa kidogo kuhusu ugunduzi huu zimehifadhiwa.
Hasa wakati huu umuhimu mkubwa unapewa mazingira, watu wengi bado wanapendezwa nayo.
Kilichotumika kuliunda gari hili bado ni siri. Kulingana na kituo cha utafiti cha Benson hakuna taarifa kamili iliyopo kuhusu ni vifaa vipi vilitumika kweye paneli kwa sababu famula yake haijahifadhiwa.
Kulinganna na nakala ya New York Times iliyochapishwa kuhusu gari hili ni kwamba wataalamu wa Ford walitumia asilimia 70 ya cellulose na alisilimia 30 ya risin binder kutengeza plastiki.
Kulingana na nakala hiyo cellulose fiber ilikuwa na asilimia 50 ya cedar Fiber, asilimia 30 ya nyasi, asilimia 10 ya bangi na asilimia 10 ya remy.
Hata hivyo Lowell, ambaye alisimamia kundi la gari hilo alitoa taarifa tofauti.
Wakati wa mahojiano alisema plastiki hiyo ilitengenezwa kutokana na soy fiber, phenolic resin na formaldehyde.
Rahisi sana
Hata hivyo kuna ujumbe wa maandishi kuhusu muundo wa gari hilo la soya.
Gari hilo lina muundo wa bomba la chuma na paneli 14 za plastiki. Faida moja ya plastiki ni kwamba ni nyepesi zaidi kuliko chuma.
Gari la soya lilikuwa tu na uzani wa kilo 907. Lina upungufu wa kilo 450 kuliko gari la kawada.
Wakati Ford ilitambulisha gari hili Agosti 13 mwaka 1941, pia ilisisitiza kuhusu ubora wake.
Licha kuwa Ford walikuwa na nia ya kutengeza plastiki kutoka kwa mimea, mradi huo haukuzaa matunda.
Gari hilo lilitengenezwa kwa muundo mmoja na liliharibiwa. Mipango ya kujenda gari lingine nayo imekwama.
Sababu ni gani?
Kwa sababu ya Marekani kuhusika kwenye vita vya pili vya dunia, mradi huo ulikwama na magari yakapigwa marufuku nchini Marekani.
Kulingana na kutuo cha ufafiti cha Benson, wazo la kuunda gari kutoka kwa plastiki halikutumia baada ya vita.
Serikali ikajikita katia kuongoza nchi baada ya vita na kurejea kwenye barabara ya maendeleo.
Wakati huohuo, hukukuwa na nia ya kutumia bioplastiki kutona na mafuta kupatikana kwa njia rahisi baada ya vita va pili vya dunia.
Haijalishi sababu ni ipi, ujenzi wa gari la soya na kutopatikana muundo wake ni kitu cha kuvutia hadi leo.