Ole Gunnar Solskjaer: Man Utd yamfuta kazi mkufunzi wake

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameondoka katika klabu hiyo baada ya kushindwa kwa mabao 4-1 na Watford Jumamosi.
Matokeo hayo yanaifanya United kuwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza - pointi 12 nyuma ya vinara Chelsea wakiwa wamecheza michezo 12.
Kocha wa kikosi cha kwanza Michael Carrick ameteuliwa kwa muda kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Villarreal Jumanne.
"Ni kwa masikitiko kwamba tumefikia uamuzi huu mgumu," United ilisema.
"Wakati wiki chache zilizopita zimekuwa za kukatisha tamaa, hazipaswi kuficha kazi zote alizofanya katika kipindi cha miaka mitatu ya kujenga upya misingi ya mafanikio ya muda mrefu.
"Ole anaondoka na shukrani zetu za dhati kwa juhudi zake za kutokata tamm kama meneja na tunamtakia heri njema.
"Nafasi yake katika historia ya klabu itakuwa salama, sio tu kwa historia yake kama mchezaji, lakini kama mtu mashuhuri na meneja ambaye alitupa wakati mzuri sana. Atakaribishwa milele Old Trafford kama sehemu ya Manchester. Familia ya umoja.
"Michael Carrick sasa atachukua jukumu la kuiongoza timu kwa michezo ijayo, huku klabu ikitarajia kuteua meneja wa muda hadi mwisho wa msimu."
Baada ya safari ya Villarreal, United wanakabiliwa na mechi za ligi dhidi ya Chelsea na Arsenal.
Olskjaer, 48, alichukua nafasi ya Jose Mourinho kwa muda mnamo Desemba 2018.
Raia huyo wa Norway alipewa kazi hiyo kwa muda wote wa Machi 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu na, Julai, alisaini mkataba mpya na klabu hadi 2024.














