Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 21.11.2021: Solskjaer, Sterling, Zidane, Dembele, Lingard, Lampard, Vlahovic, De Ligt

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wameimarisha juhudi za kumsaka kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane. United inaonekana wameongeza ofa yao ya kifedha kwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 49 ili kumrithi Ole Gunnar Solskjaer uwanjani Old Trafford. (Times - subscription required
Winga wa Manchester City na England Raheem Sterling ameiambia klabu hiyo kuwa nataka kuhamia Barcelona kwa mkopo ifikapo Januari mwakani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameanza mechi tatu pekee msimu huu na ameiomba City kuidhinisha uhamisho huo. (90 min)
Manchester City hawako tayari kumruhusu Sterling kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo na watapokea tu ofa za mshambuliaji huyo iwapo wanaweza kusajili mbadala wake.(Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa England Mason Mount, ambaye anafanya mazungumzo na Chelsea kuhusu mkataba mpya, hahisi kama "anathaminiwa" kwani nyota wa klabu hiyo na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wanaweza kuwa tayari kuondoka iwapo hali haitabadilika. (Star)
Arsenal wanataka kumsajili mchezaji wa RB Salzburg Karim Adeyemi. Mshambuliaji huyo wa miaka 19 wa Ujerumani huenda akachukua nafasi ya Alexandre Lacazette, lakini Gunners wameambiwa wasubiri hadi msimu wa joto kumnunua. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanataka kumsaini winga wa Barcelona Ousmane Dembele. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa wa miaka 24, anaingia miezi sita ya mwisho ya mkataba wake wiki chache zijazo wakati United imeonesha ishara ya kutaka kumnunua. (Mundo Deportivo, in Spanish)
Lakini mkurugenzi wa soka wa Barcelona Mateu Alemany anasema klabu hiyo imekuwa kwenye mazungumzo na Dembele kuhusu mkataba mpya na kwamba fowadi huyo anataka kusalia na klabu hiyo ya Nou Camp.(Sport, in Spanish)
Jesse Lingard anataka kuondoka Old Trafford kwa mkopo wa muda mfupi mwezi Januari kwa nia ya kuhama kabisa katika majira ya joto. Mazungumzo ya mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Manchester United na England mwenye umri wa miaka 28 na klabu hiyo yalivunjika hivi majuzi . (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wamemfanya mlinzi wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, kuwa mmoja wa walengwa wao wakuu Januari huku mkurugenzi wa soka Fabio Paratici na bosi Antonio Conte wakitambua hitaji la Spurs kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Football Insider)
Mkufunzi wa Chelsea Thomas Tuchel anapanga kufanya mazungumzo na kiungo wa Crystal Palace Conor Gallagher kuhusu mustakabali wake. Kiungo huyo wa Palace na England mwenye umri wa miaka 21 amefunga mabao manne na kusaidia ufungaji wa mabao mawili katika mechi 10 za Ligi ya Primia msimu huu. (Four Four Two)
Paris St-Germain wameachana na nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, na badala yake watafuatilia usajili wa mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic, 21, kutoka Fiorentina.(El Nacional - in Catalan)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aaron Ramsey, 30, atajaribu kupata muda zaidi wa kucheza Juventus lakini kiungo huyo wa Wales atajaribu kurejea Ligi Kuu ya Uingereza iwapo atashindwa kufanya hivyo. (Kioo)
Mahasimu wa Serie A Roma na Juventus wanatafakari uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Paris St-Germain na Argentina Leandro Paredes, 27 ifikapo Januari. (Calciomercato - in Italian).













