David Dunbar Buick: Mvumbuzi maarufu wa magari ambaye alifilisika na kusahaulika

Chanzo cha picha, AFP
Wavumbuzi wanapojitokeza na kuondoka, David Dunbar Buick anaendelea kujulikana kwa uvumbuzi wake wa ajabu.
Enzi za uhai wake, Buick alivumbua mfumo wa kunyunyizia lawn, bomba la vyoo, na njia ya kupaka masinki na mabafu kwa kutumia Cast Iron, mchakato ambao unatumika hadi leo.
Hatahivyo, umaarufu wa Buick haukutegemea matokeo haya. Umaarufu wake uliongezeka kwa kuunda magari ambayo yalikuja kuwa msingi wa kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza magari, General Motors.
Zaidi ya magari milioni 50 chini ya jina la Buick yameuzwa sana zaidi ya karne iliyopita.
Ingawa uvumbuzi wake ulimfanya kuwa tajiri, mwisho wa maisha yake, hakuwa na senti.
"Alikunywa kikombe kikubwa kupita kiasi, kisha akamwaga kila kitu," alisema mfanyabiashara wa kisasa wa Marekani na mfadhili akitoa maoni yake kuhusu hadithi ya Buick.
Ilikuwaje?
Hadithi ya Buick inaonesha kwamba alikuwa na akili ya uvumbuzi lakini hakuwa na maarifa ya biashara.
Akiwa mtoto mdogo, Buick alihama kutoka Arbroath huko Scotland hadi Marekani mwaka wa 1856. Alipokuwa akikua alianzisha biashara ya mabomba.
Biashara hiyo ilithibitisha mafanikio yake ya pekee, hatimaye alitumia fursa akawa mvumbuzi.
Hatahivyo, Buick hakuridhika bado. Mwishoni mwa karne ya 19, aligundua jambo lingine, ambalo ni sehemu ya ndani ya injini inayopeleka umeme kwa kuchoma mafuta ya petroli.
Aliuza hisa zake katika biashara ya mabomba kwa $100,000 na kuanzisha kampuni yake ya magari.
Wakati huo, Buck Auto Vim, iliunda injini ya valve ya juu, ambayo bado inatumika leo. Hatahivyo, mnamo 1902, alitengeneza gari moja tu na pesa zikaisha.
Alipata fedha kutoka kwa William Crapo Durant, ambaye baadaye aliichukua biashara ya Detroit. Wakati huo Durant alianzisha kampuni ya General Motors (GM), ambayo mpaka sasa ndiyo kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza magari duniani.
GM 'imemtambua' Buick, ikisema kwamba "jukumu lake muhimu kwa chapa ya kisasa ya Buick na kwa General Motors haliwezi kupuuzwa".
Msemaji alisema: "Ingawa hadithi ya David Buick yenyewe ni ngumu sana, lakini kama sio yeye, kusingekuwa na gari la Buick."

Chanzo cha picha, GENERAL MOTORS
Buick aliondolewa kwenye kampuni hiyo miaka michache baadaye kwa kubadilishana na $100,000 nyingine, kiasi kidogo kuliko ambacho angepata ikiwa angeweka hisa yake katika biashara hiyo.
Hatimaye, alijaribu bahati yake ya pili kwa kuwekeza katika biashara za mafuta huko California na ardhi huko Florida.
Mnamo mwaka1924, akiwa na umri wa miaka 69, alirudi Detroit bila kazi na karibu bila senti. Hakuweza hata kununua simu nyumbani kwake.
Hatimaye alifanikiwa kupata kazi ya ualimu katika Shule ya Detroit ya Trades, lakini afya yake ilidhoofika.
'Mzee mwenye kinyongo'
Mwandishi wa habari mstaafu anayeishi Arbroath, Ian Lamb, ambaye alikuja na wazo la kusimamisha sanamu ya Buick katika jiji hilo alielezea: "Kadiri alivyokuwa dhaifu, alipata majukumu zaidi ya chini kwenye dawati la habari, ambapo anakumbukwa kama mtu mwembamba. , mzee aliyeinama, ambaye huwatazama wageni kupitia miwani yake nzito."
Mnamo Machi 1929, Buick aliaga dunia kwa homa ya mapafu katika Hospitali ya Harper huko Detroit baada ya kuondoa uvimbe kwenye utumbo wake.
Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 74.
Katika mahojiano kabla ya kwenda hospitali, Buick alisema: "Sina wasiwasi, kinachoshindikana ni mtu anayekaa chini wakati anapoanguka, mtu anayekaa tu na kuwaza nini kilichotokea jana, badala ya kunyanyuka na kufikiria kuhusu kilichotokea, atakachofanya leo na kesho.
''Hayo ni mafanikio , kutazama mbele, simshutumu yoyote kwa kunidanganya. Nimepoteza kampuni niliyoiunda mwenyewe.

Chanzo cha picha, IAN LAMB
Mnamo Juni 1994, bango lilibandikwa kwenye ukuta wa Jumba la zamani la Masonic huko Arbroath, jengo pekee ambalo bado limesimama kwenye barabara ambayo alizaliwa.
Wakati bango hilo lilipozinduliwa, Robert Coletta, mtendaji mkuu wa General Motors, alisema: "Buick imekuwa mojawapo ya majina makubwa katika watengenezaji magari wa Marekani kwa karibu karne nzima ya 20.
"Kwa hakika inafaa kwetu kumheshimu, sio tu kwa sababu jina lake linatambulisha gari letu, lakini kwa sababu ujuzi wake na bidii yake iliunda mwanzo wa hadithi ya mafanikio ya magari ambayo bado yanaandikwa hadi leo."
Tangu wakati huo, nyota ya Buick imefifia na amekuwa mwana aliyesahaulika wa Arbroath.
Miaka miwili iliyopita, gazeti la New York Times liliripoti kwamba jina la Buick halikupigwa muhuri tena nyuma ya aina za magari huko Amerika Kaskazini.
Huko China, ambapo Buick nyingi zinauzwa leo, beji ya Buick imetoweka.
Licha ya juhudi za Ian Lamb na wengine, hakuna mpango wa kuweka muhuri wa jina la Buick katika vitabu vya historia na sanamu katika mji wake wa asili.
'Maendeleo makubwa'
Yote yaliyosalia ya urithi wa David Buick huko Arbroath ni ubao wa ukumbusho kando ya ukuta ambao wenyeji wengi hawaoni.
Ian Lamb alisema sanamu itakuwa heshima inayofaa kwa waanzilishi wa gari.
"Katika David Buick tulikuwa na mtu ambaye aliwajibika kwa maendeleo makubwa katika maendeleo ya gari, maendeleo ambayo bado yanafaa duniani kote leo.
"Lakini ni watu wangapi wanajua kuwa mvumbuzi huyo mahiri alizaliwa hapa Arbroath?"
"Ndiyo, tuna bango linaloashiria jengo la mwisho lililosalia kutoka mtaani alikozaliwa.
Lakini, hata watu wengi wanaoishi mjini wangekuwa na wakati mgumu kuipata."Buick anastahili kukumbukwa."













