Chombo cha Nasa chanasa sauti zake za ya miamba ya sayari ya Mars

“Máaz”

Chanzo cha picha, NASA/JPL-Caltech/LANL/CNES/CNRS

Kwahiyo, sasa tunafahamu milio ya sauti za upasuaji wa miamba zinavyosikika katika dunia nyingine.

Chombo cha Shirika la anga za mbali la Marekani kinachofahamika kama Perseverance rover kimepeleka kifaa chake kinachoitwa SuperCam kwenye sayari ya Mars kwa mara ya kwanza.

Chombo hiki chenye mwangaza mkubwa kinaweza kutambua miamba iliyopo mbali.

Ni mbinu ambayo ilitumiwa na chombo cha awali cha Nasa kinachoitwa, Curiosity.

Lakini chombo hiki cha Perseverance kimeimarishwa zaidi kiuwezo, ikiwa ni pamoja na kuwekewa kinasa sauti(microphone) ambayo inatuwezesha kusikiliza sauti za mashine yake ya uvumbuzi jinsi inavyofanya kazi.

Hili halikufanyika kwa misingi ya kupata picha bora tu za sayari ya Mars, wala kwa lengo pia la kujinadi, bali inalenga kutoa taarifa za ziada ambazo ni muhimu kwa wanasayansi.

Sauti za mashine hiyo ikigonga mwamba inafichua ujuzi kama vile ugumu wa maeneo yanayolengwa kuchunguzwa katika sayari hiyo ya Mars.

"Kama tukigusa sakafu ambayo ni ngumu, hatutasikia sauti sawa na hiyo tunapogusa eneo ambalo laini ," alifafanua Naomi Murdoch, kutoka katika Taasisi ya ngazi ya juu ya wataalamu wa anga za mbali na masuala ya anga za mbali na ya Ufaransa , mjini Toulouse.

"Chukua kwa mfano chaki au mwamba.Vitu hivi vinamchanganyiko wa kemikali unaofanana (calcium carbonate), lakini vina mchanganyiko tofauti kabisa wa kifizikia ."

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano, Dkt Murdoch alicheza sauti tatu tofautizilizorekodiwa na kinasa sauti cha SuperCam katika sayari ya Mars. Sauti moja ilikuwa ni sauti ya jumla ya kawaida ya Mars, ya pili ilikuwa ya upepo, na ya tatu ilikuwa ni ya aina fulani ya mapigo iliyosikika wakati wa upasuaji wa mwamba.

Chombo hicho-Perseverance kilitua kwenye shimo la maji la Mars- Jezero Crator tarehe 18 Februari kwa ajili ya kutafuta ushahidi wa maisha ya nyakati zilizopita.

Shimo hilo lenye kina kirefu linachukuliwa kama mahali pazuri zaidi kwa ajili ya utafiti huo kwasababu limekuwa na ziwa kwa miaka mabilioni iliyopita , na inaaminiwa kuwa mahala penye maji huenda kumekuwa na maisha, pia.

Mast head

Chanzo cha picha, NASA/JPL-CALTECH

Maelezo ya picha, Kifaa cha SuperCam kilitengenezwa kwa ushirikiano wa timu ya watafiti wa Ufaransa na Wamarekani.

Kifaa cha SuperCam kilitengenezwa kwa ushirikiano wa timu ya watafiti wa Ufaransa na Wamarekani.

Kifaa cha kwanza kilicholenga utafiti wa miamba kilipewa jina "Máaz", ikimaanisha Mars kwa lugha ya Navajo inayozungumzwana Wamarekani wazawa wanaoishi maeneo ya kusini magharibi mwa Marekani.

Máaz kilipatikana, na haikumshangaza yeyote, kwamba Mars ilikuwa na asili ya miamba.

Miamba ni kitu cha kawaida katika sayari Mars.

Ni mwamba ambao una kiwango kikubwa cha madini ya magnesium na iron, na madini haya hutokana na lava inayopoa kwa haraka.

"Hatujafahamu bado kama miamba hii yenyewe iko hai, mfano volcano, au labda ni miamba iliyoundwa na mimea iliyosombwa na mito hadi kwenye maji ya ziwa Jezero na kujikusanya pamoja ," alisema mkuu wa uchunguzi wa SuperCam Roger Wiens, Kutoka maabara ya kitaifa ya Los Alamos iliyopo katika New Mexico.

"Tutahitajika kutumia mbinu zetu zaidi na kujifunza kuhusu maeneo yanayozingira eneo hilo ili kuelewa mambo zaidi ."

Perseverance kimetumkia muda mwingi wa wiki zake tatu za kwanza katika sayari ya Mars kikichunguza maeno matatu ya kutua. Hata hivyo kimeanza kujiendesha kuelekea maeneo ya kaskazini-mashariki ya Mars.

Lengo la moja kwa moja ni uzoefu wa helikopta.

Chombo hicho kiliwekewa helikota ndogo kutoka duniani.

Gari hilo linaangalia eneo la tambarale linalofaa ambako helikopta hiyo yenye uzito wa kilo mbili, inayoitwa 'Ingenuity', inaweza kuwekwa kwa usalama ardhini.

Kwa sasa helikota hiyo ndogo imeshikizwa kwenye sehemu ya chini ya Perseverance.