Nasa imetuma chombo kuchunguza sampuli za sayari

Chanzo cha picha, NASA
Shirika la safari za anga za mbali la Marekani (Nasa) limetuma chombo ambacho kitachukua sampuli ya mchanga kwenye mwamba uliopo kwenye sayari ndogo( Asteroid) yenye upana wa mita 500 ijulikanayo kama Bennu.
Wanasayansi wanatumai sampuli hiyo itafichua maelezo ya kina juu ya taarifa za sayari zote ,na hivyo kuboresha uelewa wetu juu ya uwezekanohatari zinazoweza kusababishwa na vifaa vya angani vinavyotoka kwenye mfumo wa jua.
Chombo hicho kilichoitwa jina la Osiris-Rex, kiliondoka kuelekea anga za mbali kutoka Florida saa moja na dakika tano za asubuhi saa za Florida.
Itakichukua miaka saba kabla ya chombokurejea duniani.

Chanzo cha picha, LOCKHEED MARTIN
Sampuli hiyo itarejeshwa katika pipa likakaloshushwa kwenye jangwa la Utah tarehe 24 Septemba 2023.
Si sampuli itakayokuwa ya kwanza kurejeshwa duniani na chombo cha anga za mbali.
Wajapan walirejesha kiasi kidogo cha vumbi kutoka kwenye sayari ndogo (asteroid) katika eneo la Itokawa mwaka 2010.
Lakini Wamarekani wanatumai kupata sampuli hiyo kwa wingi zaidi, yenye uzito labda wa gramu mamia kadhaa.
Wahandisi wametengeneza kifaa cha kutunza sampuli hizo ambacho kitawekwa kwenye Osiris-Rex katika mkono wa roboti na kwenye eneo la juu la Bennu.












