Uislam: Msichana aliyetengeza nakala nzuri ya Qur'an katika kipindi cha miezi 14

Chanzo cha picha, Fatimha Shahaba
"Nilikuwa napenda kuandika nakala ya mwandiko ya Qur'an niliyoipenda.
"Mwaka jana nilinakili sura ya Qur'an na kuwaonyesha wazazi wangu na marafiki. Walifurahi sana. Niliwaambia ninataka kunakili Qur'an yote kwa kutumia mwandiko.
"Ilinitia moyo sana. Lakini walisema haitakuwa salama ."
Msichana huyu mwenye umri wa miaka kumi na tisa anayependa mchezo wa badminton-mwenye aibu Fatima Sahaba alieleza hadhithi yake hiyo ya mafanikio.
Lakini katika kipndi cha miezi 14 tu , alimshangaza kila mtu kwa kuweza kunakili Qur'an. Sio tu ndugu na marafiki lakini pia watu wengine wamempongeza kwa mafaniko yake.
Kuanza kuchora

Chanzo cha picha, Fathima Shahba
Fatima anaishi katika wilaya ya Kannur katika jimbo la kusini la India Kerala. Kutoka alipkuwa na umri mdogo alikuwa anapenda kuchora na kuandika.
Mara kwa mara alichora picha na kuwaonyesha wazazi wake. Pia walimtia moyo.
Alipokuwa anasoma darasa la tisa, alianza kupenda sana kuandika kwa michoro ya kiusanii. Alikuwa akiandika muda mwingi wa siku kwa anachosema '' kupenda sayansi ya kipekee''
"Nilikuwa ninaanza kuchora na wengine baada ya kurejea nyumbani nikitoka shule," alisema.
Alisema kwamba aya za Qur'an kila mara zimekuwa zikimfurahisha. Kwahiyo alitaka kunakili Qur'an kwa mwandiko bora.

Chanzo cha picha, Fatima Sahaba
"Mwanzoani, nilikuwa ninanakili sura moja au mbili ," anasema Fatima. "Wazazi wangu walishukuru sana.
"Baada ya muda mfupi, niliona marafiki zangu wakinunua picha zote hizo. Na nilifurahi kuchora kwa ajili yao.
"Iliinua kujiamini kwangu. Nimeanza kuamini kuwa chochote nachofanya ni muhimu kwa maisha yangu ."
Fatima Sahaba aliishi Oman na familia yake alipokuwa darasa la kumi.

Chanzo cha picha, Fathima Shahba
Wakati mmoja familia yake ilirejea nchini India. Waliishi katika mji wa Kodaparamba katika wilaya ya Kannur.
Baada ya kuamaliza shule, Fatima alitaka kujifunza uchoraji katika chou. Kwahiyo akaanza kusomea ubunifu wa ndani ya nyumba.
Kwa sasa anasomea ubunifu wa ndani ya nyuma katika chuo cha Kannur.
Kunakili Qur'an na ruhusa

Chanzo cha picha, fathima Shahba
Anasema iwapo kuna fursa, kila mtu angechagua gazi anayoipenda, na kufanya kazi hiyo kwa bidi. Kabla ya kuiandika Qur'an, baba yake Fatima alizungumza na Maulana. Alitaka kujua iwapo Fatimaanaweza kunakili Qur'an. Hatahivyo, hakuna masharti ya kidini yanayozuwia. Matokeo yake, Fatima aliruhusiwa.
"Nilimuomba baba yangu aninunulie kalamu ya wino mweusi na karatasi ya kuchora. Alinunua kila kitu kutoka katika duka lililopo jirani na kwao.
"Kila siku baada ya kurejea kutoka shule, Nilikuwa nachukua muda wa mapumziko. Baada ya sala ya Maghrib, nilikuwa naanza kunakili Qur'an.
"Nilianza kushugulikia mwandiko mwezi Agosti mwaka jana na Septemba 2021 nilimaliza kunakili Qur'an."

Chanzo cha picha, Fathima Shahba
"Nina madada wadogo na makaka. Nilidhani wangenisumbua wakati ninaandika nakala, lakini nilishangazwa sana kuona kwamba hawakunisumbua, bali walinisaidia kwa njia mbali mbali."
Fatima alijua kazi nzuri anayoifanya. Kwahiyo alitaka kumaliza kazi hiyo vyema.
"Nilikuwa nahofia kuwa huenda nikafanya makosa katika kunakili Qur'an," alisema.

Chanzo cha picha, Fathima Shahba
Fatima kwanza alibuni mwandiko kwa kalamu ya risasi ili asifanye makosa yoyote.
"Wakati nilipokuwa na uhakika kwamba hakuna kosa ndipo nilipoandika kwa kalamu ya wino," anasema.

Chanzo cha picha, Fathima Shahba
Katika kunakili Qur'an, Fatima alitengeneza kurasa 604.
"Mwanzoni kazi ilikuwa nzuri. Lakini baadaye kazi ikawa. Kadri tunavyoandika kazi ya uandishi huwa nzuri zaid ," anasema.
'Tunajivunia sana Fatima'
Wazazi wa Fatima Sahaba wanajivunia sana binti yao . Na wanasema wanajivunia sana mafanikio ya binti yao.
Mama Nadia Rauf alisema, " Kwa baraka ya Mungu, Fatima amemaliza kazi yake. Sote tunajivunia kazi yake. Tunajivunia kuwa naye. Ni msichana mchapakazi sana. Hufanya kila afanyacho kwa moyo wake wote."
"Namshukuru Allah kwamba amenipatia msichana mzuri na mchqa Mungu ," anasema Abdur Rauf, baba yake Fatima.
Fatima anasema wazazi wake hawakuwajawahi kuacha kumuunga mkono kutimiza ndoto zake. Baba anafurahia sana wakati watu wanapoipenda na kuishukuru kazi yangu.
Unaweza pia kusoma:
Ninataka kuwa mwalimu wa maandishi ya kiusanii
Fatima Sahaba anasema anapenda kuchora na kupamba nyumba kuifanya iwe yenye muonekano mzuri .
"Ninataka kuwa mwalimu wa michoro ya Sanaa," - haya ndio matumaini yake
Anasema alipokuwa mdogo, alikuwa akipaka rangi ya henna pamoja na marafiki zake. Marafiki waliupenda sana ubunifu wake.
"Sababu ni kwamba henna niliyokuwa ninaitumia kubuni michoro ilikuwa tofauti kabisa. Hivyo ndivyo nilivyovutiwa na uchoraji wa maandishi. Kuna mitindo mingi mingi katika lugha ya Kiarabu ambayo inavutia kwa msanii ."
Fatima kwa sasa hutumia muda wake mwingi katika elimu na uchoraji wa maandishi. Na pia hupenda kuwa na marafiki zake na kufurahi.
"Ni vizuri sana kuwa na marafiki. Ninafurahi sana kuongea nao ," anasema.
"Mimi ni mtu mwenye aibu kidogo. Lakini kwa sasa ninafurahi jinsi mambo yanavyozungumziwa kunihusu. Nadhani ninapata thamani ya bidii ya kazi yangu, Wakati watu wanaposema mambo mazuri kunihusu, ni nani asiyependa kusemwa vizuri?"












