Mabadiliko ya tabia nchi: Nchi masikini zaidi duniani zinataka nini kutoka katika mkutano wa mabadiliko yatabia nchi wa Glasgow ?

Nchi zinazoendelea zinakabiliwa zaidi na athari mbaya za tabia nchi kama vile mafuriko, ukame na mioto ya nyikani.

Kufikia mahitaji ya matakwa ya mataifa tajiri ni muhimu wakati wa mazungumzo yanayofanyika mkutano wa hali ya hewa COP26 mjini Glasgow, ambako viongozi wataombwa kukubali ahadi mpya za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Nchi zinazoendelea zinataka nini ?

Nchi zinazoendelea duniani zimetengeneza oridha ya vipaumbele vyake, huku zikitaka nchi tajiri na zile zinazoendelea kufanya mambo yafuatayo:

  • Kutimiza ahadi yake ya kutoa dola bilioni 100 (takriban pauni bilioni 73 ) kila mwaka ili kuzisaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
  • Kukubali kukamilisha usitishwaji wa utoaji wa gesi chafu kabla ya mwaka 2050, kwasababu kuna malengo mahsusi kwa nchi zinazowajibika na utoaji wa kiwango kikubwa cha utoaji wa hewa chafu, kama vile Marekani, Australia na baadhi ya nchi za Muungano wa Ulaya .
  • Kutambuliwa uharibifu usliosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile athari ya kuongezeka kwa viwango vya maji ya bahari au mafuriko ya mara kwa mara.
  • Kukamilisha sheria za ufuatiliaji wa utekelezwaji wa makubaliano yaliyofikiwa awali
  • Katika taarifa yake kabla ya mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi kikundi cha nchi zinazoendelea ilisema " Kuongezwa kwa malengo ya dunia na kuongeza ufadhili wa fedha katika kupambana na athari mabadiliko ya hali ya hewa ni muhimu katika kunusurika kwetu ."

Mwenyekiti wa kikundi cha nchi zinazoendelea, Sonam Wangde, alisema: "Mzozo haujashugulikiwa kama mzozo na hali hiyo lazima ibadilike hapa katika Glasgow."

Ni nchi gani ambazo zinakabiliwa zaidi na athari za mabadiliko ya tabia nchi?

Nchi zinazoendelea kihistoria zimekuwa zikichangia asilimia ndogo tu ya utoaji wa hewa zenye madhara zilizosababisha mabadiliko ya tabia nchi , na 1% ya watu wanaoishi katika nchi tajiri zaidi duniani wanawajibika kwa zaidi ya mara mbili ya kiwango cha uzalishaji wa hewa chafu zinazozalishwa na asilimia 50 ya wakazi wan chi masikini duniani leo.

Nchi masikini pia zinakabiliwa na athari zenye madhara za hali mbaya ya hewam kwasababu zinategenea zaidi zaidi mazingira asilia kwa ajili ya chakula na ajira, na hazina pesa za kutumia kuweza kukabiliana na adhari hizo.

Zaidi ya miaka 50 iliyopita, zaidi ya vifo viwili kati ya vitatu , vilivyotokana na hali mbaya ya hewa, ikiwa ni pamoja na ukame, mioto ya nyikani na vimekuwa vikitokea katika walau nchi 47 masikini zaidi duniani.

Nchi tajiri zinafanya nini kukabiliana na tatizo ?

Katika mwaka 2009, nchi tajiri zaidi duniani ziliahidi kutoa dola bilioni 100 Kila mwaka kutoka kwa sekta za umma na za kibinafsi kufikia mwaka 2020 ili kitimiza haja za nchi zinazoendelea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Fedha hizo zililenga katika kufadhili kupunguzwa kwa utoaji mbaya wa hali ya hewa na kuzilinda nchi zinazoendelea dhidi ya athari za hali mbaya zaidi za hewa kama vile kuboresha mifumo ya kuzilinda na mafuriko na kuwekeza katika vyanzo vya nishati safi.

Hatahivyo, ahadi hizo zilikuwa ni jumla ya bilioni 80 tu kufikia mwaka 2019, na lengo hilo huenda lisifikiwe kabla ya 2023.

Nchi zinazoendelea zinajadiliana vipi katika mikutano ya mabadiliko ya tabia nchi ?

Nchi zinazoendelea kwa kawaida huwa hazina sauti katika jukwaa la kimataifa, kwahiyo ni muhimu kwao kuunda kikundi ili kuwezesha sauti yao kusikika.

Kikundi cha nchi zinazoendelea kinajumuisha nchi 46, ikiwa ni pamoja na Senegal, Bangladesh na Yemen, na zinawakilisha watu bilioni moja.

Nchi hizo zinaweza kuimarisha msimamo wa majadiliano yao wakati "vipaumbele na maslahi yanapokuwa sawa ,"anasema Sonam Wangde, mwenyekiti wa sasa wis kutoka Bhuta.

Nchi hizi zimefanya kazi pamoja kwa kipindi cha mwaka uliopita na watakutana katika mji wa Glasgow.

Iwapo makubaliano ya mwisho yatafikiwa, nchi zote 197 zilizosaini Makubaliano ya Umoja wa Mtaifa ya mfumo unaohusu mabadiliko ya tabia nchi zitatakiwa kuyasaini.

Hii inamaanisha kuwa makubaliano hayo lazima yakubaliwe na nchi masikini na tajiri kwa pamoja.

Ni muhimu kukumbuka kuwa viongozi wa dunian walishindwa kufikia makubaliano ya kisheria ya Copenhagen katika mwaka 2009, kwa sehemu moja kwasababu nchi chache zinazoendelea zikiwemo Sudan na Tuvalu, zilipinga toleo la mwisho la makubaliano ya mwisho hayo.

Unaweza pia kusoma: