Wafahamu wanaharakati 5 wanaopinga mabadiliko ya hali ya hewa unaostahili kuwajua

Wakati mawaziri wanaohusika na mabadiliko ya hali ya hewa wanafanya mazungumzo yao ya mwisho kabla ya mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Glasgow, wanaharakati wachanga watano wanaeleza ni kwa nini uanaharakati wao una umuhimu, kile wamefanya kuleta mabadiliko na matarajio yao siku zinazokuja.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataiafa wa COP 26 unaondaliwa kupitia ushirikiano kati ya Uingereza na Italia utafanyika kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi 12 Novemba 2021.

Huu ni mwaka muhimu kwa mazungumzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP26 mwezi Novemba unatarajiwa kuwa wenye ushawishi kwa kuweka malengo ya muda mrefu kusuluhisha tatizo lililopo.

Waandamanaji watano wachanga wanaeleza ni kwa nini uanaharakati ni muhimu kwa kile wamefanya kuleta mabadiliko na matumaini yao siku zinazokuja.

'Ilinilazimu niandamane'

Shaama Sandooyea alifanya maandamano ya kwanza ya mabadiliko ya tabia nchi mara ya kwanza mwezi Machi kama sehemu ya vita vyake kulinda moja ya eneo kubwa zaidi duniani lenye nyasi za bahari.

Akishika bango lenye ujumbe "Vijana wagome kwa hali ya hewa", mwanaharakati huyo mwenye miaka 24 alipiga mbizi kwenda bahari hindi umbali wa kilomita 735 kutoka pwani ya Ushelisheli.

"Eneo hili lina bayo anuai nyingi lakini kwa sasa linakumbwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi," anasema Shaama, mwanasayansi wa masuala ya bahari. Tuligundua kuwa matumbawe yameanza kukua karibu na nyasi za bahari."

Nyasi za baharini ni kati ya mimea inaayopunguza kiwango cha kaboni baharini na ina uwezo wa kuchukua gesi ya Carbon kutoka hewani hata kuliko msitu wa Amazon. Wanasayansi wanasema ni muhimu kulinda maeneo hayo ikiwa tunataka kuzuia ongezeko la joto kwa zaidi nyusi 1.5C. Wanaharakati watano wanaopinga mabadiliko ya hali ya hewa unaostahili kuwajua

Mamia ya viumbe wa baharini walio kwenye hatari ya kuangamia wanategemea nyasi ya bahari kwa chakula na makao.

Lengo la mgomo wake ni kuwashawishi viongozi wa dunia kujitolea kulinda maeneo yanayotegemewa kwa takriban asilimia 30 ya bahari zetu.

' Ninazungumza kuhusu uharibifu ninao uona'

Bhagya Abeyratne aligonga vichwa vya habari nchini Sri Lanka wakati alifichua kuwa mfumo nchini humo wa nani anataka kuwa milionea, anaamini msitu wa Sinharaja unakumbwa na hatari kutokanana ukataji miti kwa miradi ya ujenzi.

Mwanaharakati huyo wa umri wa miaka 19 kutoka kijiji cha Rukwana kilicho karibu na eneo lililo chini ya hifadhi ya UNESCO alisema haya wakati wa kinyang'anyiro kwenye kipindi cha televisheni cha wanaharakati wa mazingira na tangu wakati huo amepongezwa sana kwa hatua zake.

Lakina serikali na mamlaka zimemlaumu kwa kutoa taarifa zisizo za ukweli. Polisi na idara ya misitu walifika nyumbani kwao na kumhoji.

Katie Hodjetts alikuwa na umri wa miaka 18 wakati aligundua kuwa tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa sio suala lililokuwa likifanyika mbali na nyumbani kwao huko Bristol Uingereza.

"Wakati nikiwa mdogo, picha ya dubu juu ya teluthi inayoyeyuka ilifanya nifikirie kuwa na hilo halikuwa na lolote na jinsi nilikuwa naishi," anasema.

Hiyo ilibadilika wakati alijiunga na chuo kikuu na kusomea kile kinachojulikana kama siasa na mabadiliko ya hali ya hewa.

"Ndipo nikaelewa kuwa tatizo la mabadiliko ya tabi nchi lilikuwa kubwa kuliko dubu wa milima ya theluji.

Mwaka 2019 akawa mmoja wa waandalizi wa kwanza wa kile kilichojulikana kama Bristol Youth Strike 4 Climate movement na kuwaleta pamoja maelfu ya vijana kupinga kupanuliwa kwa uwanja wa ngege wa mji na kuhutubia umati wa hadi karibu watu 30,000.

'Ilikuwa hatari kwa afya zao'

Sophia Kianni alifahamu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa wakati akiwa dasara la sita wakati alifanya safari kwenda Tehran akiwa na umiri wa miaka 12 au 13 na akiwa na uraia wa Iran na Marekani na kugundua jinsi tatizo lilikuwa kubwa. Siku moja aliangalia angani na hakuona nyota kwa sababu ya uchafuzi.

Uchafuzi ulikuwa mbaya lakini niligundua kuwa ndugu zangu hawakuelewa chochote kuhusu hilo.

Walisema Tehran ni mji mkubwa na hivyo ndivyo hali ya hewa ilivyo kutokana na viwanda. Hawakuelewa hatari iliyokubwa kwa afya zao.

Sophia akaunda vikundi vya vijana kuwaelimisha watu kote duniani kuhusu athari za mabadiliko ya tabia nchi . Badala ya kusambaza habari kwa Kiingereza, aligundua kuwa ni vyema kile kinachochapishwa kiwe katika lugha asili.

'Viongoizi wa dunia hawajajitolea'

Sarah Goody alikuwa na umri wa miaka 12 wakati somo la sayansi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa lilichangia mabadiliko makubwa katika maisha yake.

"Siku hiyo niligundua umuhimu wa mabadiliko ya tabia nchi ," anasema. Darasa kisha likachukua mwezi mzima kusoma kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kwa wanyamapori na wanadamu.

"Ndio mara ya kwanza nilianza kuelewa kuhusu ukubwa wa tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.

Nikaanza kutazama makala, kusoma na kufanya utafiti wangu binafsi."

Akiwa na miaka 14 akazindua shirika la Climate Now, shirika la kimataifa la vijana linalojikita katika kuwaelimisha vijana kuchukua hatua za kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa. Lina vijana 30 wa kujitolea kutoka kote duniani na limewaelimisha hadi wanafunzi 10,000.

Mwaka uliopita Sarah alikuwa mmoja wa wale waliopokea tuzo ya Princess Diana, inayowatambua wanaharakati wa kibinadamu wachanga.