Genge la Clan del Golfo lina nguvu gani na kwanini Otoniel anafananishwa na wakati wa Pablo Escobar

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwishoni mwa wiki iliyopita, miongoni mwa habari kubwa katika masuala ya usalama hivi karibuni nchini Colombia: ni kumkamata Dairo Antonio Úsuga David, anayejulikana kama Otoniel, Mfanyabiashara mashuhuri wa dawa za kulevya na kiongozi wa genge kubwa la uhalifu linaloitwa Clan del Golfo, huko kusini mwa Amerika.
Vyombo vya habari vya ndani na nje vilipokea taarifa za kukamatwa kwake, katika eneo la magharibi mwa Colombia, na kusema kuwa Otoniel ndiye "mtu anayetafutwa zaidi" ambaye analiongoza shirika linaloundwa na wanaume 6,000.
Kwa kuongezea, mamlaka ya ndani imebainisha kuwa genge hilo la Clan del Golfo - pia waliliita Autodefensas Gaitanistas , Los urabeños au Clan Ú suga - alikuwa na udhibiti wa ulanguzi wa dawa za kulevya kupitia Ghuba ya Urabá, eneo lililoko kaskazini-magharibi mwa Colombia.
Huko pia kwa mujibu wa polisi nchini humo , walikuwa wanahusika na usafirishaji wahamiaji katika mpaka wa Colombia na Panama wakati wakipitia Darien Gap.
Hata hivyo , rais wa Colombia, Iván Duque, alifanya ulinganisho uliovuta hisia za wachambuzi wa kisiasa na mwanahistoria: "Kukamatwa kwa Otoniel anafananishwa na anguko la Pablo Escobar," alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Kukuza jambo
"Huko ni kukuza mambo, ingawa haipingiki kuwa Otoniel ni muhalifu aliyekuwa anatafutwa sana Colombia kwa wakati huu, katika wakati wa Pablo Escobar aliweza kukabiliwa kwa vita" , anasema Hernando Zuleta, mchambuzi wa siasa kutoka chuo kikuu .
Zuleta na watu wengine ambao walizungumza na BBC Mundo waliainisha ukweli kuwa: mwaka 1990, ulikuwa wakati mbaya zaidi wa vita dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya nchini Colombia, kulikuwa na mashambulio 180 ya magari , ambayo yalisababisha maelfu ya watu kuuawa katika miji mbalimbali.
"Mambo yamebadilika tangu kifo cha Pablo Escobar. Ingawa dawa za kulevya aina ya cocaine zinatengenezwa zaidi ya wakati wa Escobar, nguvu ya walanguzi wa dawa za kulevya Colombia imepunguzwa, "alisema.
Nguvu ya genge la Golfo Clan
Ingawa wachambuzi wengi wanasema kuwa Otoniel hawezi kufananishwa na Pablo Escobar, ukweli ni kuwa nguvu ya genge ambalo alikuwa analiongoza mpaka mwishoni mwa wiki haliwezi kulinganishwa hivyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya taasisi ya taifa ya polisi na amani na upatanishi (National Police and the Peace and Reconciliation Foundation), Genge la Clan del Golfo ni taasisi ya uhalifu ambayo imethibiti miji mingi nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti, Clan del Golfo ina manispaa 211 kati ya 1,103 nchini Colombia na inakadiria kuwa zaidi ya maelfu ya watu walikuwa chini ya uongozi huo wa alias Otoniel, wengi wao wakiwa wanachama wa zamani wa wapiganaji wa msituni wa Jeshi maarufu la Ukombozi maarufu (EPL) na vikundi vya kujilinda.
Na hayo yana ufafanuzi : Otoniel mwenyewe ni sehemu ya EPL na kundi hilo la wapiganaji wa msituni walipoondolewa mwaka 1991, aliamua kubadili uelekeo na kuwa mwanachma wa kundi la kujihami lililokuwa eneo la Urabá , kaskazini magharibi mwa Colombia.
Lilikuwa eneo hilo ambapo alijiunga na taasisi iliyoongozwa na, Daniel Rendón alifahamika zaidi kama Don Mario, mmoja kati ya watu hatari aliyejisogeza zaidi na kundi la wanamgambo ambap walimfanya aweze kuwa na uwezo wa kulidhibiti eneo ambalo lilihifadhi genge la uhalifu la Medellín, baada tu ya kifo cha Escobar mwaka 1993. Pia ndio eneo ambalo Clan del Golfo pamoja na Don Mario walikamatwa mwaka 2009.Huku mwenzao Otoniel, ndani ya kipindi cha muongo mmoja aliweza kuanzisha utawala wake. Na kutokana na uhusiano wake na wafanyabiashara kadhaa wa dawa za kulevya wa Mexico, pia alifanikiwa kupata tani nyingi za cocaine nchini humo.
Kwa mujibu wa mamlaka za wilaya huko Colombia, inakadiriwa kuwa nusu ya mauzo ya cocaine ambayo huondoka Colombia hadi nchi nyingine yalidhibitiwa na Clan del Golfo, kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ndiyo maana Otoniel, ambaye alikuwa mwanajeshi na mtu aliyejihusisha na ujambazi zamani (hakutaka kuwa sehemu ya mchakato wa kuwaondoa watu wenye silaha ambao ulitokea miaka ya nyuma), anachukuliwa kama mmoja wa walanguzi wakubwa wa sawa za Kulevya Marekani ya kusini.
Aidha ili kufikia watu wakubwa wa usalama walianzisha vita na mashirika ya usalama ya eneo hilo, hasa na polisi wanaofanya kazi katika eneo la Urabá. Taarifa zinasema kuwa askari wapatao 40 waliuawa na wanachama wa kundi hilo.
"Haiwezi kukanushwa kuwa Clan del Golfo ndio wanaohusika zaidi na uhalifu nchini Colombia, haswa kwa sababu limeweza kudhibiti eneo kubwa na hii ni kutokana na kujimilikisha eneo hilo hususani kwa biashara ya dawa za kulevya," José Guarnizo, mwandishi wa habari wa Colombia, aliambia BBC.
Mwandishi wa kitabu "La patrona de Pablo Escobar". Guarnizo anasema kuwa hii imemruhusu kudhibiti sio tu ulanguzi wa dawa za kulevya, lakini pia shughuli zingine haramu kama vile unyang'anyi wa biashara, usafirishaji wa binadamu na kuvuka mpaka kati ya Panama na Colombia bila ya kuwa na vibali.
"Wameweza kujua jinsi ya kudhibiti maeneo ambayo cocaine inazalishwa na kuisafirisha nchi zingine," anaongeza.
Mabadiliko makubwa: kutoka mji hadi nchi Ingawa maneno ambayo Rais Duque alimlinganisha Otoniel na Pablo Escobar yameonekana kama ukweli wake ulikuwa na ulakini kwa lengo la kujipatia umaarufu kwa watu wengi,
Kwa Gustavo Duncan, mtafiti na profesa wa serikali na sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Eafit cha Medellín, mojawapo ya mabadiliko makubwa yanahusiana na uwezo ambao walanguzi wa dawa za kulevya walikuwa nao juu ya raia nchini Kolombia.
"Si Otoniel, wala kundi la Ghuba au mashirika mengine ya sasa nchini Kolombia yaliweza kuwa na kile ambacho Pablo Escobar au Cali Cartel walikuwa nacho: udhibiti wa miji mikubwa ya nchi," anasema mtafiti.
Duncan anaonyesha kwamba Escobar na Rodríguez Orejuela, wakuu wa Cali Cartel, walikuwa na uwezo wa kiuchumi ambao uliwaruhusu kutawala maeneo makubwa ya mijini. Na katika hili liko kwake tofauti kuu na mashirika ya sasa.
"The Gulf Clan ni shirika linalofanya kazi pembezoni na vijijini na hii ni matokeo ya kupita kwa Escobar na Cali Cartel: ni vigumu sana kwa cartel au mfanyabiashara wa madawa ya kulevya kuwa na ushawishi huo tena katika jiji kubwa kama Medellín, Bogotá au Cali " .
"Hiyo ilikuwa maendeleo ya wazi ya Serikali na mapambano yake dhidi ya Escobar. Ndiyo maana kukamatwa kwa watu hao wawili si sawa," anaongeza.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na kwa maana hiyo, genge la Clan del Golfo lilithihirisha kuwa Otoniel ameweka himaya maeneo ya vijijini, wakishirikiana na mashirika yenye silaha ambayo yalifanya kazi msituni kama vile waasi au vikundi vya kujilinda.
Muelekeo mpya wa biashara
Kama Escobar au kaka zake Rodríguez Orejuela wangeongeza nguvu , ingewezekanaje kiasi chote cha dawa za kulevya aina ya cocaine kutengenezwa Colombia sasa kuliko wakati huo?
Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya dawa za kulevya na uhalifu , mazao ya coca nchini Colombia yameongezeka kutoka hekari 50,000 mwaka 1995 kufikia hekari 140,000 mwaka jana.
" Mgenge ya dawa za kulevya Colombia, kwa kuacha kushamiri maeneo ya mijini, yaliachana na kutafuta ushawishi wa kisiasa kama mwanzoni na kujikita katika kuzalisha na kuuza nje cocaine," anaongeza Duncan.
"Ndio maana cocaine nyingi zaidi zinazalishwa sasa kuliko wakati wa Escobar."
Kwa upande wake, mchambuzi Hernando Zuleta anaeleza BBC kwamba "biashara imebadilika."

Chanzo cha picha, Getty Images
Na pia imesababisha ukweli kwamba, katika miaka 30, uzalishaji wa cocaine na mazao ya jani ambayo yako chini ya udhibiti wake yameongezeka kwa kasi.
Kwa kuongezea, wakuu wapya wa magenge ya dawa za kulevya wa Colombia walijifunza somo la kutoonekana.
"Watendaji hawa wapya katika hatua ya usambazaji wa dawa za kulevya walijifunza kitu: hapo awali ilikuwa kuonekana na hali ya juu ya makampuni makubwa ambayo yaliwaangamiza."
"Sasa ni majambazi ambao hawaonekani kuwa majambazi," anasema Zuleta
Mwisho wa genge la Gulf Clan?
Je! inaweza kusema kwamba kuanguka kwa Otoniel kutasababisha mapambano mapya dhidi ya mashirika ya dawa za kulevya, kama ilivyotokea katika anguko la Escobar mnamo mwaka 1993?
Kwa Duncan, kuna mambo mawili muhimu yanayojibu swali hilo.
"Kwanza, kukamatwa kwa Otoniel, Gulf Cartel kama shirika la uhalifu halitaisha mara moja. Ni mchakato ambao utachukua muda," alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Pili, na haya ni matokeo yaliyotokea, mkakati wa serikali utakuwa muhimu kuzuia mkuu wa pili wa shirika hili kudumisha umoja na utawala ambao Otoniel aliweza kudumisha kwa miaka kadhaa," anasema.
Kwa upande wake, Zuleta anabainisha kuwa kwasababu hakuna operesheni ya kimataifa iliyoelezwa, kutakuwa na ugumu sana kupunguza biashara ya dawa za kulevya kutoka Colombia.
."Juhudi za miongo kadhaa za kuharibu mazao, kuwekea dawa na kuwa na bidhaa mbadala hakuna mafanikio tuliyoyapata , kwa sababu ni biashara na mahitaji, yanaendelea kuwepo," anasema mchambuzi huyo
Miongoni mwa mkakati mkubwa ambao amependekeza, kuwa mengi yanapaswa kutekelezwa bila ya yote kuwa na majibu kamili, ni kuunda miradi ya majaribio ya kuhalalisha ili kubaini kama inawezekana kwa kiwango kikubwa.
"Tumeona kuhalalishwa kwa bangi katika majimbokadhaa Marekani, kumepunguza uhalifu ukilinganisha na wakati ambao bangi ilikuwa haijakubaliwa kisheria. Jaribio linaweza kufanywa eneo ambalo tunaona wigo wa hatua kama hiyo inaweza kupunguza nguvu za mashirika ya dawa. dawa, "anafafanua.














