Muammar Gaddafi: Familia yake ilishia wapi miaka 10 baada ya kifo chake?

Gaddafi na mke wake na watoto katika makazi yake ya Bab al-Aziziyah mwaka 1992

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gaddafi na mke wake na watoto katika makazi yake ya Bab al-Aziziyah mwaka 1992

Jumatano, ilikuwa maadhimisho ya kifo cha Muammar Gaddafi, aliyenyakua madaraka kwa mapinduzi kupitia mwaka 1969, na utawala wake kuendelea hadi alipopinduliwa na kuuawa Oktoba 20, 2011.

Kwa zaidi ya muongo mmoja, maandamano makubwa yaliibuka nchini Libya, ambayo yaligeuka na kuwa vilivyong'oa madarakani Kanali Muammar Gaddafi, ambaye aliiongoza Libya kwa mkon wa chuma kwa miongo minne na kuendesha utawala uliwekwa na wanae wa kiume na ndugu na kuidhibiti nchi :

Lakini je ni nini kilichotokea kwa wanafamilia wa Gaddafi waliobaki?.

Watoto watatu wa kiume wa Gaddafi walikufa katika matukio haya, ikiwa ni pamoja na mshauri wa zamani wa usalama, Mutassim Gaddafi, ambaye aliuliwa na watu wenye silaha siku moja na baba yake. Tangu tarehe ile, familia ya Gaddafi imegawanyika, na wamechukua njia tofauti za maisha

Gaddafi na familia yake

Gaddafi alizaliwa mwaka 1942 karibu na mji wa Sirte. Alikuwa maarufu kwa sare yake ya kipekee na walinzi wake wa kibinafsi ambao wengi walikuwa wanawake. Aliwakilisha mawazo yake katika "Green Book" kama mfumo mbadala kwa ujamaa na ubepari na kuuchanganya na mawazo ya Uislamu.

Gaddafi

Chanzo cha picha, Reuters

Agosti 2011, utawala wake ulianguka rasmi, baada ya vikosi vya baraza la mpito kuingia katika mji mkuuTripoli, takriban miezi sita baada ya muamko wa mageuzi makubwa dhidi dhidi yake na uingiliaji kati wa jeshi la magharibi.

Oktoba 2011, aliuawa katika mji wake wa nyumbani Sirte

Mke wa kwanza

Fathia Khaled ni mke wa kwanza wa Gaddafi na alikuwa ni mwalimu. Inasemekana kuwa wanandoa hao hawakuwahi kukutana kabla ya ndoa. Walikuwa na mtoto mmoja wa kiume , Muhammad, na wakaachana baada ya miezi sita.

Mke wa pili

Mke wa pili, Safiya Fargash, ni mama wa watoto wake saba . Wawili hao waliwaasili watoto watatu wa kiume na wa kike wawili , Milad Hana, na Safia ambao walikuwa wametoroka na binti yake Aisha na Muhammed bin Gaddafi kutoka kwa mke wa kwanza Fathia Khaled, kutoka mji mkuu , Tripoli, mwaka 2011 hadi katika nchi ya Algeria, ambayo iliwapatia hifadhi kama wakimbizi i kwa "sababu za kibinadamu" kabla hawajahamia katika Ufalme wa Oman.

AFP

Chanzo cha picha, AFP

Muhammed Gaddafi

AFP

Chanzo cha picha, AFP

Akizaliwa mwaka 1970, Muhammed Gaddafi alikuwa ni mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Libya, yenye makao yake Tripoli. Pia alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya mawasiliano ya posta ambayo ilisimamia mawasiliano ya simu za mkononi na setilaiti. Alihamia Oman baada ya kutoroka Libya na kwenda Algeria.

Hajashitakiwa bado na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, na haaminiwi kuhusika katika kujaribu kupinga muamko wa mageruzi mwaka 2011.

Saif al-Islam Gaddafi

Seif al-Islam, mwenye umri wa miaka 49, anazungumza vyema Kiingereza, ana Shahada ya uzamivu(PHD) kutoka katika chou kikuu cha Uingereza cha masuala ya uchumi - London's School of Economics, na yumo miongoni mwa watu waliotaka uchumi huru wa wa Libya.

Aliongoza Wakfu wa Gaddafi wa msaada na maendeleo, ambao ulifanya mazungumzo ya kuachiliwa kwa mateka walioshikiliwa na wanamgambo wa Kiislamu, hususan ni katika nchi ya Ufilipino.

Reuters

Chanzo cha picha, Reuters

Tarehe 19 Novemba, 2011, tume ya baraza la NTC lilitangaza kumkamata kusini magharibi mwa Libya.

Taarifa kumuhusu Saif al-Islam Gaddafi

  • Juni 1972: Alizaliwa Tripoli, Libya, mwana wa pili wa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi
  • Februari 2011: Upinzani dhidi ya serikali ya Gaddafi inaanza
  • Juni 2011: Mahakama ya Kimataifa yatoa kibali cha kukamatwa kwake kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu
  • Agosti 2011: Anaondoka mji mkuu baada ya Tripoli kudhibitiwa na vikosi vilivyopinga serikali; akakimbilia Bani Walid
  • Oktoba 2011: Baba na ndugu mdogo wauawa
  • Novemba 19, 2011: Alitekwa na wanamgambo alipokuwa akijaribu kukimbilia kusini mwa Niger. Akafungwa Zintan
  • Julai 2015: Alihukumiwa kifo na mahakama ya Tripoli
  • Juni 2017: Inasemekana aliachiliwa chini ya sheria ya msamaha iliyotolewa na mojawapo ya serikali mbili za mashindano nchini Libya
Saif al-Islam Gaddafi alihukumiwa kifo bila kuwepo na mahakama ya Tripoli

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Saif al-Islam Gaddafi alihukumiwa kifo bila kuwepo na mahakama ya Tripoli

Licha ya ukosoaji mkubwa ambao bado anakabiliana nao, bado kuna Walibya wengi wanaomuunga mkono Saif al-Islam, na nchi za magharibi bado zinamuona kama mrithi ajaye wa Ghaddafi kulingana na mwandishi wa BBC Orla Guerin.

Mwezi Julai mwaka jana gazeti la The New York Times lilisema kuwa lilifanya mahojiano na Saif al-Islam Gaddafi, kwani wafuasi wake wamesema kuwa atagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa Disemba 2022.

Saad Gaddafi

Al-Saadi ni mtoto wa tatu wa kiume wa Gaddafi, na kwa sasa ana umri wa miaka 48. Amemuoa binti wa kamanda wa zamani, na alikuwa mchezaji wa zamani wa soka, ambapo alicheza kwa muda mfupi katika Ligi ya Italia

Al-Mu'tasim

Chanzo cha picha, Al-Mu'tasim

Al-Saadi aligeuka kuwa mzalishaji wa filamu, akiwekeza dola milioni 100 katika kampuni ya uandaaji wa filamu.

Baada ya kuanguka kwa utawala wa baba yake, alikimbilia Niger, ambayo ilimpatia hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa, lakini mwaka 2014 , alirejeshwa Libya kwa ajili ya kesi dhidi yake.

Tarehe 5 Septemba, chanzo rasmi cha Libya kilisema mamlaka za Libya zilimuuachilia huru, na kwamba kuachiliwa kwake kulifuatia mazungumzo ambayo yalihusisha viongozi wa kikabila na waziri mkuu Abdel Hamid al-Dabaiba, na hapo ndipo alipoondoka mara moja kwenda Instanbul

Mutassim Gaddafi

Al-Mu'tasim alizaliwa mwaka 1975 na alikuwa Kanali katika jeshi la Libya . Alitorokea Misri baada ya kudaiwa kupanga mapinduzi dhidi ya utawala wa Gaddafi.

Khamisi

Chanzo cha picha, Getty Images

Hatahivyo, baadaye alisamehewa na akaruhusiwa kurudi nyumbani, ambako alihudumu kama Mshauri mkuu wa usalama wa taifa na akaongoza kikosi chake kibnafsi cha kijeshi. Aliuliwa na watu wenye silaha katika siku ambayo baba yake aliuawa.

Hannibal Gaddafi

Alikuwa akifanya kazi katika Kampuni ya taifa ya safari za majini, ambayo ilishugulika na usafirishaji wa Mafuta, na alidaiwa kuhusika katika matukio kadhaa ya ghasia.

AFP

Chanzo cha picha, AFP

Baada ya kuanguka kwa utawala wa baba yake, aliondoka na kuelekea nchini Algeria na kutoka pale alikwenda Oman ambako alipata ukimbizi . Alitekwa nyara na kikundi chenye silaha kisichojulikana nchini Lebanon mwishoni mwa mwaka 2015 kwa kipindi kifupi na baadaye aliachiliwa.

Kwa sasa anaishi Lebanon na mke wake, mwanamitindo wa zamani , Aline Skaf, katika mji mkuu wa Syria Damascus, ambako utata uliibuka hivi karibuni kwamba mke wake aliwagonga wapiti njia kadhaa wakiwemo polisi, katikati ya jiji.

Unaweza pia kusoma:

Saif Al-Arab Gaddafi

Ni mtoto wa kiume wa sita wa Gaddafi, aliyezaliwa mwaka 1980, ni taarifa chache zinazojulikana kumuhusu.

AFP

Chanzo cha picha, AFP

Mwaka 2008, gazeti la Uingereza The Daily Telegraph liliripoti kwamba polisi Ujerumani walilichukua gari lake aina ya Ferrari, kutokana na kwamba gari hilo lilikuwa linatoa kelele.

Anasemekana alikuwa mwanafunzi katika Chuo kikuu cha Munich wakati wa utawala wa baba yake. Saif al-Arab na watoto wake wawili waliuliwa katika mojawapo ya uvamizi wa vikosi vya muungano wa NATO mjini Tripoli.

Matokeo yake, wafuasi wa Gaddafi walichoma ubalozi wa Uingereza mjini Tripoli, ana majengo na mali nyigine za nchi za magharibi, kujibu kisasi kwa kumuua mtoto huyu wa kiume wa Gaddafi na wajukuu wake wawili.

Khamis Gaddafi

Ni mtoto mdogo zaidi wa Gaddafi wa kiume. Alizaliwa mwaka 1983. Alikuwa ni afisa wa polisi na alikuwa akiongoza kikosi maalumu. Alipata mafunzo ya kijeshi nchini Urusi. Iliripotiwa kuwa alikubali kuwajibika kwa kuwazuwia waandamanaji mjini Benghazi.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Khamis Gaddafi aliuawa Agosti 2011 pamoja na mtoto wa kiume wa Abdullah Al-Senussi, mkuu wa huduma za ujasusi katika utawala wa Gaddafi, katika mapigano na vikosi vya Baraza la mpito katika mji wa Tarhuna, ulipo takriban kilomita 90 kusini mashariki mwa mji wa Tripoli, kwa mujibu wa kituo cha televisheni kilichomuunga mkono Gaddafi.

Vyanzo vya kijeshi na kiraia vilisema kuwa mtot wa Khamis Gaddafi bado anaishi lakini duru binafsi ziliithibitishia BBC kifo chake.

Aisha Gaddafi

Aisha ana umri wa miaka 44 na anafanya kazi kama wakili. Pia alikuwa amejiunga na kundi la mawakili waliokuwa watetezi wa rais wa zamani wa Iraq hayati Saddam Hussein.

Aisha

Chanzo cha picha, AFP

Aliolewa na mmoja wa mabinamu wa Gaddafi mwaka 2006. Ndiye binti pekee wa Ghaddafi na alipewa ukimbizi nchini Algeria pamoja na mama yake, na baadaye alihamia Oman.

Vyombo vya habari vya Libya viliripoti kuwa Aisha, alipokuwa Algeria, aliunga mkono timu ya taifa ya soka dhidi ya timu ya Libya, akisema kuwa ''upande wa Libya'' haumuwakilishi.''

Hana Gaddafi

Kanali Gaddafi kwa muda mrefu alidai kwamba binti yake aliyemuasili kwa jina Hana aliuawa katika shambulio la anga la Marekani mwaka 1986, wakati alipokuwa na umri wa miezi 18 tu.

Hatahivyo, tangu mwaka 2011, Ushahidi ulijitokeza kwamba Hana alikuwa bado yuo hai, video ilitokea ya Hana akicheza na baba yake na ndugu zake miaka kadhaa baada ya mashambulio hayo ya makombora yaliyotekelezwa na Marekani.

AL-ARABIYA WEBSITE

Chanzo cha picha, AL-ARABIYA WEBSITE

Nyaraka zilipatikana katika makazi ya Gaddafi ya Bab al-Aziziya zikionyesha nyaraka za Matibabu , pamoja na Ushahidi wa Baraza la Uingereza kumuhusu Hana Muammar Gaddafi.

Kulingana na vyanzo vya habari nchini Libya, Hana ni daktari, na alifanya kazi katika kituo cha matibabu mjini Tripoli kwa miaka kadhaa.