Mzozo wa Msumbiji: Wanajeshi wa Rwanda wapata watumwa wa ngono na misikiti iliyoharibiwa

People in a crowd in Pemba hold up pictures of Rwanda's President Paul Kagame at an event to greet him during his two-day visit to Cabo Delgado in September
Maelezo ya picha, Raia wa Msumbiji wakisubiri kumsalimia rais wa Rwanda katika mji wa Cabo Delgado
    • Author, Anne Soy
    • Nafasi, Senior Africa correspondent, Mozambique

Chini ya miti mikubwa ya maembe, maembe yakiwa yameiva na mengine kuoza hakuna wa kuyaokota huko kaskazini mwa Msumbiji.

Zaidi ya miaka minne , vijiji vingi na miji ya Cabo Delgado imetelekezwa na wakazi wake -lakini mwezi uliopita wanamgambo wa kiislamu waliondolewa na wanajeshi wa Rwanda.

Majengo yamekuwa magofu tayari na kukiwa na ushahidi wa milipuko bado.

Katika kuta zilizoanguka , tayari magugu yameanza kuota katika maeneo ambayo yalikuwa makazi ya watu hapo awali.

Nilikuwa miongoni mwa kundi la waandishi wa habari walioona kwa mara ya kwanza , uharibifu ulioachwa na wanamgambo wanaofahamika duniani kama wanamgambo wa kiislamu.

Wakazi wa hapo wanawaita kwa jina la kiarabu la vijana - al-Shabab.

Ingawa hawana uhusiano na kundi ambalo lina jina kama hilo huko Somalia. Wanadaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Islamic State.

"Wana uhusiano wa kiitikadi zaidi," Msemaji wa jeshi la Rwanda kanali Ronald Rwivanga aliwaambia.

Jeshi la Rwanda lilitutembeza katika jimbo hilo , eneo ambalo mapigano yalitokea wiki chache zilizopita.

Map of Cabo Delgado

Kundi moja lilihama kutoka Palma kaskazini mwa eneo ambalo kulitokea shambulio katika hoteli na watu kadhaa kuuawa mnamo mwezi Machi, baadhi ya waathirika walikutwa wamekatwa vichwa, na wengine kufungwa mikono mgongoni.

Shambulio hilo liliilazimu kampuni kubwa ya nishati kutoka Ufaransa, kufunga mradi wake wa gesi .

Kundi la pili lilienda jimbo la magharibi wakiwa na wanajeshi wa Rwanda, kukiwa karibu na mji wenye bandari wa Mocímboa da Praia, eneo ambalo Agosti 8 jeshi la majini la Msumbiji lilisitisha huduma ya ufikaji wa baharini.

Walikutana na uvamizi na mapigano wakati wanamgambo wakiwa wanakimbilia kusini eneo la msituni katika hifadhi ya taifa ya Quirimbas wakiwa na mateka wao na waliojeruhiwa, kanali Rwivanga alisema.

Wapiganaji wapatao 100 waliuawa na Rwanda kupoteza wanajeshi wake wanne, alisema.

Ngome kuu ya wapiganaji wa kiislamu ya Mbau, nyumba nyingi zinaonekana kuwa zilitelekezwa kwa muda mrefu, na kubaki kuwa magofu.

Wanajeshi wanadai walikuta maficho yao huko.

'Misikiti iliteketezwa'

Katika kituo kimoja tu cha Quitunda, tulikuta sauti za watoto wakiwa wanacheza mpira bali mzee wa miaka 80, alikuwa amekaa katika gogo akiwa anaangalia mechi..

Children displaced by fighting walk past soldiers from the Rwandan security forces in a camp for the internally displaced, in the town of Quitunda, Mozambique - 22 September 2021

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mji wa Quitunda ni miongoni mwa miji ambayo ilikuwa na watu

"Hatujui waasi wanataka nini," aliniambia. "Waliteketeza misikiti yetu na kushambulia makanisa yetu."

Alihamia hapa aliposikia kuwa wapiganaji walikuwa wameondoka.

Angependa kurudi nyumbani kwake katika mji wa bandari wa Mocímboa da Praia - lakini kila kitu kimeharibiwa. Hakuna hata jengo moja,kote kumeharibika kutokana na mapigano ya miaka.

Katika mji huo , wanajeshi wa Rwanda walituonesha silaha walizozipata kutoka kwa wapiganaji.

Weapons captured from militants, Mocímboa da Praia, Mozambique - 22 September 2021

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baadhi ya silaha za wapiganaji

Silaha hizo nyingi zilikuwa ni AK-47, baadhi ya hizo zilikuwa zimeandikwa majina kwa rangi, inawezekana yalikuwa majina ya wapiganaji waliokuwa wanazimiliki.

Kulikuwa na silaha nyingine kama mabomu na silaha za kupambana katika anga.

Kulikuwa na mfungwa wa vita , alikuwa mvuvi mwenye miaka 18, aliniambia kuwa alichukuliwa na kulazimishwa kujiunga na kundi la wapiganaji.

Vitisho vya watumwa wa ngono

Baadhi ya wanawake waliookolewa walikuwa wanakaribia. Tulikutana nao Pemba, ambako wengi walikimbilia huko.

Mama wa watoto sita aliniambia walimchukua alipokuwa shambani na watoto wake wadogo watatu.

Iliwachukua karibu wiki nzima kuweza kupumzika. "Walikuwa wakiwapiga watoto kama wakilalamika kuwa wamechoka," alisema.

Wapiganaji walikuwa na yeye kama mtumwa wa ngono kwa zaidi ya mwaka. Wakati akinyonyesha, alipata mimba na kujifungua akiwa mateka.

A woman in Pemba who was kidnapped by al-Shabab and her children - Pemba, Mozambique, September 2021

"Hakukuwa na chakula cha kutosha," alisema.

Yeye na wanawake wengine waliweza kutoroka wakati helkopta ilipokuja wiki chache zilizopita ambayo iliwalazimisha wapiganaji kukimbia.

Mwanamke mwingine aliyekuwa mateka mwenye miaka 24 alisema alishuhudia wanawake wawili wakiuawa walipojaribu kutoroka.

Wapiganaji walipandikiza hofu na kutoaminiana sisi wenywe. Baadhi ya mateka walikuwa walikuwa wanatoa taarifa kuhusu mipango ya kutoroka.

Wapiganaji walikuwa hawalali usiku na waliwalazimisha kulala mchana, alisema.

Walikuwa wakilazimisha wanawake kwenda vijijini kuvuna chakula kama miogo.

Lakini chakula kilikuwa hakitoshi kwa ajili yao na mateka wao.

Maelezo ya video, Africa Eye: Watu wanaotekeleza vitendo vya kigaidi ni nani, wanataka nini Msumbiji?

"Tafadhali wasaidieni wale ambao bado ni mateka," aliomba.

Anataka kurudi nyumbani kwa mume wake na watoto wake, lakini hajui watampokeaje. Maisha yake hayawezi kuwa sawa tena.

Jeshi la Msumbiji liko sasa katika eneo ambalo lilikuwa limethibiwa na wanamgambo.

Lakini utagundua tu kuwa wapiganaji hao walikuwa na silaha nzuri na ukilinganisha na jeshi la Rwanda.

Huko Pemba,nilimuuliza rais wa Rwanda Paul Kagame kuhusu gharama za operesheni na wafadhili na alijibu kuwa ni serikali ya Rwanda ndio imefadhili.

line
Mozambican soldiers patrol in front of a burned truck carrying the inscription "Shabaab Chinja" referring to the jihadist group in Mocímboa da Praia -22 September 2021

Chanzo cha picha, AFP

"Kiukweli ni gharama kubwa," alijibu, "hivyo tunahitaji kuungwa mkono."

Mara nyingi alikosolewa kwa hatua hiyo lakini Rwanda imekuwa shujaa wa Msumbiji.

Katika tukio lililoandaliwa na serikali , wananchi walipeperusha picha yake na bendera ya Rwanda.

Serikali ya Msumbiji inawataka watu kurudi majumbani kwao.

Wanajeshi wa Rwanda bado watabaki mji wa Cabo Delgado mpaka hali iwe shwari.

Wapiganaji wanaweza kuwa wameondoka lakini bado wakazi wana hofu.