Mzozo wa Msumbiji: Wanajeshi wa Rwanda waongoza vita dhidi ya wapiganaji Msumbiji

Rwanda yaongoza majeshi yake kukabiliana na wapiganaji Msumbiji

Chanzo cha picha, Reuters

Wanajeshi 1000 wa Rwanda wameanza kazi nchini Mozambique tangu wapelekwe nchini humo kukabiliana na wapiganaji ambao wamefanya mashambulizi ya uharibifu kaskazini mwa taifa hilo.

Katika kipindi cha wiki mbili - kundi la kwanza la wanajeshi wa kigeni kuwasili nchini humo dhidi ya wapiganaji hao , limeteka eneo muhimu lenye barabara ya makutano , ambalo lilikuwa likishikiliwa na wapiganaji hao kwa zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja uliopita , na wamefika katika mji muhimu wa Mocimboa da Praia.

Katika kipindi cha miaka minne wapiganaji hao walichukua udhibiti wa wilaya tano muhimu katika mkoa wa Cabo Delgado katika eneo la mashariki la Msumbiji. Kufikia sasa takriban watu 3,100 wameuawa na wengine 820, 000 kuwachwa bila makao.Katika kipindi cha miaka minne tangu makundi ya uasi yalichukua udhibiti wa maeneo mengi ya wilaya tano katika jimbo la Cabo Delgado kaskazini mashariki mwa Msumbiji

Hadi sasa watu 3,100 wameuawa na wengine zaidi ya 820,000 wamekimbia makazi yao -ikiwa ni zaidi ya idadi yote ya watu wa wilaya tano,

Wakati makundi ya uasi yalipoteka mji wa Palma mwezi Machi, mji wenye utajiri wa gesi ambako kunatengenezwa kiwanda chenye thamani ya dola bilioni 20 (£14bn) kikiwa ni kiwanda cha pili kwa ukubwa barani Afrika, Kampuni ya Ufaransa ya mafuta ililazimika kuacha ujenzi mkubwa katika eneo hilo.

Jeshi la ulinzi la Msumbiji linafahamika kwa kiasi kikubwa kuwa ni lenye ufisadi , lenye mafunzo ya kiwango cha chini na lenye ukosefu wa vifaa na kwamba wasingeweza kukabiliana na mashambulio ya wapiganaji.

Licha ya kupingwa na ndani ya chama chake, Rais Filipe Nyusi aliita usaidizi wa nje.

Kuna mapatano mengi mwamko wa uasi ulianzishwa na vijana wasio na ajira wanaopinga kuongezeka kwa umasikini na ukosefu wa usawa, pamoja na ukosefu wa faida zitokanazo na raslimali ikiwa ni pamoja na gesi na mawe ya thamani ya rubi.

Fariba Maurabu mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikimbia mapigano ameketi na familia nyingine zilizopo tarehe 8, Disemba, 2020 ambazo zilikimbia mapigano miezi mitatu iliyopita kwenye ufukwe wa Paquitequete katika mji wa Pemba, baada ya wanamgambo wenye silaha kuuteka mji wa Mocimboa da Praia.

Mzozo katika eneo la Kaskazini mwa Msumbiji uliwalazimisha zaidi ya watu 800,000 kuyakimbia makazi yao

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mzozo katika eneo la Kaskazini mwa Msumbiji uliwalazimisha zaidi ya watu 800,000 kuyakimbia makazi yao

Hii imezingirwa na udhalimu wa kijamii-ukosefu wa sauti na unyanyasaji wa maafisa wa serikali, polisi na wanajeshi.

Mzozo ulianza na shambulio dhidi ya Mocímboa da Praia mwaka 2017 na mzozo huo ukaendelea kuwa mbaya huku vijana wakiteka silaha kutoka kwa wanajeshi na kupata uungaji mkono wa wenyeji.

Uhusiano 'dhaifu' na IS

Waasi wanaitwa "al-Shabab", jina ambalo kwa kienyeji linamaanisha "vijana" na halina uhusiano na kundi lenye jina sawa na hilo nchini Somalia.

Eneo lenye mzozo linakaliwa na Waislamu wengi, na kufikia mwaka 2019 waasi walikuwa wamewasiliana na kundi la Islamic State (IS).

Marekani imewapatia jina la "Isis Mozambique" na kuwataja kama shirika la kigeni la ugaidi.

Vijana wavuvi wa Msumbiji walirejea kwenye mwambao baada ya siku kadhaa za uvuvi katika Palma, ambako hifadhi kubwa ya gesi asilia ilipatikana kwenye mwambao, tarehe 16 Februari, 2017

Watu wengi hutegemea uvuvi kujikimu kimaisha kaskazini mwa Msumbiji.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Watu wengi hutegemea uvuvi kujikimu kimaisha kaskazini mwa Msumbiji.

Lakini wapiganaji hawana ujumbe halisi wa kidini na badala yake wanasema wanapigana na taifa.

Na bado wanapigana kwa kutumia silaha na vifaru vya jeshi walivyoviteka kutoka kwa vikosi vya usalama vya Msumbiji.

Kikundi cha kimataifa cha masuala ya mizozo( IGC) hivi karibuni kilisema kuwa wapiganaji wana "uhusiano dhaifu" na kwamba "sababu halisi inaochochea mzozo huu ni kuhusu malalamiko ya wenyeji ".

Hakuna mtu atakayetuma wanajeshi Msumbiji kusaidia kupigana na raia wenye njaa, lakini wengi watasaidia kupambana na IS.

Ureno, ambayo ni koloni la zamani, pamoja na Marekani tayari wana wanajeshi wao nchini Msumbiji wanaotoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji ili kupigana na makundi ya uasi.

Jirani mkubwa wa Msumbiji, Afrika Kusini, alishawishi sana atume wanajeshi wake kupitia jumuiya ya kikanda, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika (Sadc).

Lakini Msumbiji ina mchanganyiko wa kihistoria na hao watatu na inataka kuwaweka mbali na silaha.

Ilifanya makubaliano na Rwanda, ambayo ina jeshi lenye ujuzi wa hali ya juu wa kijeshi.

Ramani ya Msumbiji

Siku 10 tu baada ya Rais Nyusi kusafiri Rwanda kukutana na mwenzake wa Rwanda kwa mazungumzo mwezi Aprili -kikosi cha kuchunguza hali ya mzozo na kuweka mkakati cha maafisa wa Rwanda kilikuwa tayari Cabo Delgado.

Vyanzo vya kidiplomasia vinasema Marekani iliidhinisha kupelekwa kwa vikosi vya Rwanda nchini Msumbiji.

Rwanda imejenga mahusiano na Israeli, ambayo bila shaka ingeunga mkono harakati dhidi ya IS.

Mara vikosi vya Rwanda kufika nchini Msumbiji na kupigana, vikosi vya Sadc viliruhusiwa kuingia.

Meli za Afrika Kusini na ndege ziliwasili mwishoni mwa juma karibu na eneo la vita na msafara wa magari wa kikosi cha kwanza na wanajeshi 1,500 wa Afrika Kusini wakaingia ndani ya Msumbiji.

Wanajumuisha kikosi maalumu cha Brigedi ya 43. Vifaru vya kijeshi vya Botswana na wanajeshi 300 ambao walivuka na kuingia ndani ya Msumbiji.

Hofu ya washambuliaji wa kuvizia

Rwanda inasema vikosi vyake viko pale kwa wakati wowote itakapokuwa muhimu, na hatimaye wanatarajiwa kubuni eneo salama karibu na mji wa Palma viwanda vya gesi.

Matumaini ni kwamba kampuni ya mafuta ya Total itahisi kuwa salama kwa kutosha kuweza kurejea kufanya kazi zake mwaka ujao.

Mwanzo vikosi vya Afrika Kusini viko Msumbiji kwa miezi mitatu pekee. Na karibu wanajeshi 3,000 pamoja na uwepo wa vikosi vya anga na majini bila shaka itaharakisha kazi ya kuikomboa tena miji , barabara na bandari ya Mocímboa da Praia.

Msafara wa kijeshi wa Kikosi cha ulinzi cha Afrika Kusini husafiri kwenye barabara ya vumbi katika wilaya ya Maringanha katika wilaya ya Pemba tarehe 5 Agosti 2021

Vikosi vya Afrika Kusini vimeanza sasa kutumwa maeneo ya vita

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Vikosi vya Afrika Kusini vimeanza sasa kutumwa maeneo ya vita

Lakini waasi wameanza tayari kuzikimbia ngome zao na kugawanyika katika makundi madogo madogo, kama wanavyofanya wapiganaji wa msituni wanapokabiliwa na shinikizo la mashambulio .

Baadhi ya maeneo ya vita yana misitu mikubwa ambayo ni maeneo bora zaidi ya kujifika ya wapiganaji.