S-400: Ifahamu silaha inayozua hofu kati ya Marekani Uturuki na Marekani

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema katika mahojiano na runinga ya Marekani ya CBS kwamba serikali yake ina mpango wa kununua silaha nyengine aina ya S-400 kutoka kwa Urusi.

Lakini msemaji mmoja wa Idara ya serikali mara moja alijibu: Tunaionya Uturuki dhidi ya kununua silaha zaidi za kijeshi kutoka kwa Urusi.

Serikali ya Ankara inaonekana kupuuza onyo la Marekani kama ambavyo imekuwa ikifanya hapo awali.

Je Rais Erdogan alisema nini?

Akizungumza katika runinga hiyo ya CBS katika hotuba yake kwa taifa, mtangazaji Margeret Brennan alimuuliza swali hili .

"Inaonekana kana kwamba bado unataka kununua silaha nyengine aina ya S-400, je ni kweli?.

Akijibu Erdogan alisema: Tutanunua hivi karibuni . Hakuna mtu anaweza kuingilia masuala ya nchi nyengine .. "

Mtangazaji huyo alirejelea tena suali hilo akisema: Je unamaanisha ndio?. Erdogan alijibu mara moja: Unamaanisha nini? Ndio.

Jibu la Marekani

Kulingana na chombo cha habari cha Reuters , msemaji huyo wa idara ya masuala ya kigeni aliulizwa mara moja kuhusu jibu la serikali yake kufuatia matamshi hayo ya Erdogan.

"Tunaionya Uturuki, tunaonya kupitia viwango mbalimbali e kwamba kwasababu tayari anamiliki silaha hiyo hana haja ya kununua nyengine na hatutaki anunue silaha nyengine aina ya S-400 kutoka kwa Urusi.

Tutaweka vikwazo

"Tutaendelea kuiambia Uturuki kwa maelezo kwamba silaha yoyote itakayonunuliwa kutoka kwa Urusi itasababisha vikwazo zaidi mbali na vikwazo vilivyowekwa Disemba 2020'', alisema.

Msemaji huyo alisema kwamba Marekani inaichukulia Uturuki kama mshirika wake na kwamba inatazama njia za kuimarisha uhusiano wake zaidi na taifa hilo licha ya kwamba kuna tofauti ya maono.

Mwezi Disemba mwaka uliopita , wizara ya fedha nchini Marekani iliiwekea vikwazo Uturuki kuhusu hatua ya taifa hilo kununua silaha aina ya S-400 kutoka kwa Urusi.

Mwezi Aprili 2021, azimio la CAATSA lilianza kutumika na Uturuki ikapigwa marufuku kununua silaha kutoka Marekani.

Uturuki hutengeneza silaha za kisasa ambazo awali Ujerumani ilikuwa imezikataa.

Je ni aina gani ya silaha zilizonunuliwa na Uturuki ambazo zinahatarisha maisha ya Marekani?

Na ni kwanini Uturuki inataka kuongeza uwezo wake wa silaha za kijeshi?

Mataifa hayo mawili ni wanachama wa muungano wa NATO , ijapokuwa yana tofauti kubwa za kijeshi.

Uturuki kwa sasa ipo katika mazungumzo kununua silaha kutoka kwa Urusi , na inaonekana kwamba Ankara haitajali hatua ya Marekani kupinga uamuzi huo.

Erdogan alisema katika mahojiano na CBS kwamba alikuwa akituma ujumbe kwa rais Joe Biden.

"Namwambia Biden, hii ni muhimu. Tayari tumenunua ndege aina ya F35. Tuliwalipa Marekani $1.4b lakini haijaturudishia fedha hizo licha ya kuwalipa kununua ndege hizo. "

Siku ya Jumatano , rais Erdogan anatarajiwa kukutana na rais wa Urusi Vladmir Putin ambapo watazungumzia ununuzi wa silaha hizo pamoja na masuala mengine ikiwemo hali ilivyo kaskazini magharaibi mwa Syria.

Je silaha aina ya S-400 inafanya kazi vipi?

  • Rada ya uchunguzi wa mbali huangalia vilipuzi na ndege, na hupeleka habari kwa vifaa vya ulinzi, ambavyo hutathmini malengo yanayowezekana
  • Lengo linapogunduliwa linaamuru gari kurusha kombora
  • Takwimu za kurusha kombora zinatumwa kwa gari la kurusha kombora ambalo hurusha kombora hilo mara moja angani
  • Rada husaidia kuongoza kwa urahisi makombora kufikia malengo yake.

Mzigo wa kwanza wa silaha aina ya S-400 kutoka Urusi ziliingia nchini Uturuki katikati ya 2019.