Tiba ya kubadili maumbo inavyoathiri warembo mashuhuri kimwili na kisaikolojia

Cryolipolysis hugandisha mafuta kama njia ya kuyapunguza

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanamitindo Linda Evangelista, mmoja wa walimbwende mashuhuri wa miaka ya 90, alitangaza wiki hii kwamba katika miaka mitano iliyopita alitengwa kwa sababu ya shida wakati wa matibabu ya urembo ambayo yalimwacha akiwa "ameharibika umbo lake kabisa."

"Nimetengeneza, hatari ambayo sikuifikiria kabla ya kufanyiwa taratibu," alisema Jumatano katika barua kwenye ukurasa wa Instagram.

Huko pia aliweka wazi kwamba ataishtaki kampuni iliyofanya matibabu hayo, utaratibu wa kupunguza mwili uitwao cryolipolysis kwa kitaalamu ambao, na kwa mujibu wake, "ulikuwa na matokeo kinyume na vile alivyoahidiwa" na kumwacha akiwa "ameharibika sana."

Cryolipolysis

L a Paradoxical Adipose hyperplasia (pia inajulikana kwa kifupi HAP) ni shida mara chache inaweza kutokea wakati wa matibabu utaratibu ambao ulifanywa na Evangelista.

Cryolipolysis ni mchakato wa kupunguza mwili, ambao ni sehemu ya kile kinachojulikana kama matibabu ya kutengeneza mwili.

Utaratibu huu unatafuta kugandisha mafuta ya mwili mahali ambapo ni ngumu kuyaondoa.

Ili kufanya hivyo, joto la chini sana huwekwa kwenye eneo linalopaswa kutibiwa, kwa muda maalum.

Lengo ni kutenganisha mafuta kutoka kwenye tishu na kuyaondoa, bila hitaji la upasuaji.

Kulingana na wataalamu wa matibabu haya, kipindi kimoja cha matibabu huharibu kati ya 20% na 25% ya seli za mafuta katika eneo lililotibiwa, ingawa matokeo hayaonekani mara moja.

Cryolipolysis hugandisha mafuta kama njia ya kuyapunguza

Chanzo cha picha, Getty Images

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) inatambua utaratibu huu kuwa tiba salama, kwa hivyo uliidhinisha, kwanza kutumika kwenye nyonga, mnamo mwaka 2008, na baadaye kwenye tumbo, mwaka 2011.

Hatahivyo, kikundi kidogo sana cha watu - hasa wanaume - wamepata athari mbaya baada ya kupata matibabu haya.

Kama ilivyotokea kwa Evangelista miaka mitano iliyopita, watu hawa walipata ugonjwa kitaalamu unaoitwa 'adipose hyperplasia', ambao husababisha seli za mafuta kuongezeka badala ya kupungua, na kutengeneza eneo gumu la mafuta ya ndani.

Shida hii adimu inaweza kuonekana kati ya wiki 8 na 24 baada ya tiba na hufanyika katika eneo ambalo tiba ilifanywa.

Tafiti zinasema nini?

Bado haijafahamika kwanini baadhi ya watu hupata athari baada ya tiba hii.

Utafiti uliochapishwa mwaka 2014 katika jarida la JAMA Dermatology, la Jumuia ya Madaktari Marekani, ulibainisha kuwa nafasi ya kutokea kwa madhara ni ndogo: kama 0.0051%.

Ilisisitiza pia kwamba "hakuna sababu ya hatari iliyotambuliwa" hasa kati ya wale wanaougua, ingawa hali hiyo "inaonekana kuwa ya kawaida kwa wagonjwa wa kiume wanaopitia tiba hiyo (cryolipolysis).

Hatahivyo, kikundi kidogo sana cha watu - hasa wanaume - wamepata athari mbaya baada ya kupata matibabu haya.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Kwa wakati huu, hakuna ushahidi wa utatuzi wa changamoto hiyo ," imeongeza.

Hatahivyo, utafiti wa baadaye, uliochapishwa mwaka 2018, ulihitimisha kuwa athari hiyo "inaweza kuwa ya kawaida zaidi kuliko ilivyofikiriwa hapo awali."

Maelezo ya video, Fahamu hatari ya kuongeza maziwa

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la ''Plastic and Reconstructive Surgery" wa Jumuiya ya wafanya upasuaji wa Marekani (ASPS), ilikadiriwa kuwa ilikuwa na matukio hayo kwa 0.025%.

Wanaume wako kwenye hatari zaidi baada ya tiba ya kurekebisha maumbo yao

Chanzo cha picha, Getty Images

"Watu wanafikiria kuwa matibabu yasiyo ya upasuaji ni salama, lakini sivyo ilivyo," Profesa Ash Mosahebi, daktari wa upasuaji wa urembo aliiambia BBC.

Kulingana na Mosahebi taratibu zote zina hatari.

Katika ujumbe wake, Evangelista alisema kwamba alikuwa amepata "upasuaji awamu mbili za kurekebisha mwili ambazo hazikufanikiwa."

Athari za kimwili na kisaikolojia

Katika chapisho lake la mitandao ya kijamii, mwanamitindo wa zamani wa Canada mwenye miaka 56 alieleza wazi athari ambayo alikumbana nayo kwenye maisha yake.

Alisema kuwa ilimwacha bila uwezekano wa kufanya kazi "wakati kazi za wenzangu zimefanikiwa."

Na akabainisha athari za kisaikolojia ambazo zilimfanya ahisi "kutotambulika."

''Ilinifanya niwe mwenye kunyong'onyea na huzuni kubwa, na kujichukia," alikiri.

Baadhi ya watu ambao walipata umaarufu pamoja naye katika miaka ya 1990 walijibu ujumbe wake wakimtia moyo na kumpongeza kwa ujasiri.