Wafungwa sita wa Palestina watoroka gereza la Israel kupitia handaki

Gereza la Gilboa

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Gereza la Gilboa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Maafisa nchini Israeli wameanzisha msako mkali baada ya wafungwa sita wa Kipalestina kutoroka kutoka kwenye moja ya magereza yenye ulinzi mkali usiku.

Wanaume hao wanaaminiwa kuwa walichimba handaki hilo kuanzia kwenye mahabusu yao kwa miezi kadhaa na kuweza kufikia barabara iliyopo nje ya kuta za gereza la Gilboa.

Maafisa walifahamishwa na wakulima ambao waliwaona wafungwa hao wakikimbia shambani.

Wafungwa waliotoroka ni pamoja na kiongozi wa kikundi cha wanamgambo wa Brigedi ya mashahidi wa Al-Aqsa na wajumbe watano wa kikundi cha Jihadi cha Kiislamu.

Afisa wa magereza nchini Israeli alielezea kutoroka kwa wafungwa hao kama " kushindwa vibaya kwa usalama na ujasusi "; na makundi ya wanamgambo wa Palestina yamesifu kitendo hicho kama cha "ushujaa".

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Kengele ya dharura ililia kwenye gereza la Gilboa, ambalo ni gereza lenye uslama mkubwa lililopo kaskazini mwa Israeli likifaamika kama "the Safe", wakati maafisa walipopokea taarifa kutoka kwa wakulima wa eneo hilo kuhusu "watu wasiojulikana " walioonekana katika mashamba yao.

Wakati wahudumu wa gereza walipowahesabu majira ya saa kumi alfajiri , walibaini kuwa wafungwa sita hawapo.

Wapalestina hao wanaaminiwa kutengeneza njia ambayo waliitumia kutokea nje kwa kuchimba shimo la handaki kwenye sakafu ya bafu lao. Handaki hilo lilitokea nje ya gereza lao.

Picha za video zinaonesha maafisa wakikagua shimo dogo lililochimbwa chini ya sinki na shimo jingine katikati ya barabata chafu inayopita kando ya kuta za gereza hilo.

Jarida la The Jerusalem Post limeripoti kuwa wafungwa hao walitumia koleo ambalo walikuwa wamelificha nyuma ya bango.

Huduma za usalama za Shin Bet, wakati huo huo zimesema kuwa zinaamini kuwa wamekuwa wakiwasiliana na watu nje ya gereza kwa kutumia simu iliyoibiwa na kwamba walichukuliwa na gari baada ya kutoroka gerezani.

Handaki lilitokea katika eneo lililopo karibu kuta za gereza

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Handaki lilitokea katika eneo lililopo karibu kuta za gereza

Wafungwa hao watoro sita ni pamoja na Zakaria Zubeidi, kamanda wa zamani wa kikundi cha Wapalestina cha Brigedi ya Mashahidi wa Al-Aqsa kilichopo katika mji wa West Bank wa Jenin, pamoja na wajumbe watano wa kikundi cha Kiislam cha Jihad.

Gazeti la The Times la Israel lilisema kuwa watano kati ya wafungwa hao sita walikuwa wanatumikia kifungo cha maisha baada ya kuhusishwa na mashambulio yaliyosababisha vifo ndani ya Israeli. Zubeidi alikuwa gerezani wakati kesi dhidi yake ya makosa ishirini na nne ya uhalifu ikiendelea, ikiwa ni pamoja na kujaribu kutekeleza mauaji.

Polisi wa mpaka wa Israeli na wanajeshi wanaofanya msako wanasemekana kuweka vizuizi ili kuwazuia wanaume hao kufika karibu na eneo lililotwaliwa la West Bank au Jordan, ambalo liko takriban kilomita 14 (maili tisa) mashariki mwa jimbo la Gilboa.

Waziri mkuu wa Israeli Naftali Bennett alizungumza na Waziri wa usalama wa umma Omer Bar-Lev na "kusisitiza kwamba hili ni tukio baya ambalo linahitaji juhudi za ushirikiano wa vikosi vyote vya usalama'' kuwapata watoro.

Kikundi cha Jihad cha kiislam kimeeleza kutoka kwa wafungwa hao kutoka jela ni "ushujaa" na kimesema kitendo hicho "kitaushitua mfumo wa ulinzi wa Israeli'' , huku msemaji wa Hamas Fawzi Barhoum akisema ni "ushindi mzuri" ambao unathibitisha "utashi na juhudi za wanajeshi wetu jasiri ndani ya magereza ya adui hauwezi kushindwa".

Ramani ya Israel