Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afghaniastan: Ni vifaa gani vya kijeshi vilivyoachwa nyuma na vikosi vya Marekani?
Picha zimeibuka za wapiganaji wa Taliban wakiwa na vifaa vya kijeshi vilivyoachwa nyuma na vikosi vya Marekani katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kabul wa Hamid Karzai.
Jumla ya ndege 73, karibu magari 100 na vifaa vingine viliachwa na wanajeshi wa Marekani walipokuwa wakiondoka kabla ya tarehe ya mwisho ya wao kuondoka nchini humo Agosti, 31.
Lakini kamanda mkuu wa jeshi Marekani Jenerali Kenneth McKenzie alisema kuwa vifaa vyote vilivyoachwa vimelemazwa hivyobasi haviwezi kutumika tena.
"Ndege hizo hazitaweza kusafiri tena," alisema.
"Ndege zilizoachwa Kabul ni pamoja na:
- Helikopta aina ya MD-530, zilizotumika kwa uchunguzi na mashambulizi ya karibu
- Ndege aina ya A-29 za mashambulizi
Mnamo mwezi June, jeshi la Afghan lilikuwa linatumia:
- Ndege 43 aina ya MD-530, walizopewa na Marekani
- Ndege 23 aina ya A-29
Kujua gharama ya kila kilichoachwa sio rahisi - lakini gharama ya ndege moja aina ya A-29 imenukuliwa kama zaidi ya $ 10m (£ 7.3m).
Video iliyopigwa na mwandishi wa LA Times Nabih Bulos inaonyesha wapiganaji wa Taliban wakiwa na helikopta ya usafirishaji ya CH-46 Sea Knight.
Ikiwa zinatumiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuhamisha wafanyikazi kutoka ubalozi wao huko Kabul, ndege aina ya Seven Sea Knights zimeripotiwa kuachwa zikiwa haziwezi kutumika tena.
Ndege moja ya usafiri aina ya C-130 Hercules pia ilipigwa picha.
Kulingana na Jenerali McKenzie, magari 70 yanayotumika wakati wa uvamizi aina ya 'mine-resistant ambush-protected vehicles' (MRAP) pia yalitelekezwa, baada ya kulemezwa.
Gharama ya MRAP moja imenukuliwa kama $ 500,000- $ 1m.
Pia vifaa vingine vilivyoachwa Kabul ni pamoja na:
- Magari ya kijeshi ya kivita 27 aina ya 'Humvee'
- Na idadi isiyojulikana ya roketi na vifaa vya mfumo wa kujikinga dhidi ya uvamizi
Katika baadhi ya matukio, vilipuzi vilikuwa vinatumika kuharibu vifaa vinavyoachwa nyuma.
Hata hivyo, kwengineko, wanajeshi wa Afghanistan walitoroka wakifanya juhudi kidogo sana kuharibu vifaa wanavyoviacha nyuma.
Picha za setilaiti zinaonyesha kuwa baadhi ya ndege zilisafirishwa nje ya nchi hadi Uzbekistan, siku chache kabla ya serikali ya Afghanistan kuanguka.
Na wataalam wanasema kuwa ndege zingine zinaweza kuwa na matumizi kidogo sana kwa Taliban bila kuwa na marubani waliofunzwa, kujua namna ya kuzitunza na kuweza kupata vipuri.
Lakini, ingawa haiwezekani kujua idadi kamili, ndege nyingi kati ya 167, pamoja na helikopta 33 aina ya UH-60 Black Hawk, zilizokuwa chini ya udhibiti wa vikosi vya jeshi vya Afghanistan mwishoni mwa Juni, sasa zinafikiriwa kuwa mikononi mwa Taliban.
Je, jeshi la Afghan lilikuwa na ndege ngapi kufikia Juni 30, 2021?
Ni wazi kwamba Taliban tayari wanatumia baadhi ya vifaa vya Marekani vilivyoachwa nyuma.
Vikosi maalum vya jeshi la Taliban wamepigwa picha wakiwa katika mji wa Kabul na bunduki aina ya M4.
Na Marekani pia ilitoa zaidi ya magari ya kivita ya 'Humvees' 2,500, kutoka Desemba 2017 hadi Aprili 2020, kulingana na Mkaguzi Mkuu Maalum wa Marekani wa Ujenzi wa Afghanistan.
Gharama zake zinaweza kutofautiana - lakini bei ya moja imenukuliwa kama zaidi ya $ 250,000.
Wataalam wengine wa vifaa wanasema inaweza kuwa vifaa walivyonaswa na Taliban vikawa vya thamani kubwa ikiwa ni pamoja na miwani za macho zinazotumika usiku, 16,000 ambazo zilipewa wanajeshi wa Afghanistan kati ya mwaka 2003 na 2021.