Homa isiyojulikana inavyowauwa watoto wa India

Kwa zaidi ya wiki moja sasa, watoto katika baadhi ya wilaya za jimbo la kaskazini mwa India la Uttar Pradesh wamekuwa wakiamshwa na homa kali na kujipata wameloa kwa jasho.
Wengi wao wanalalamika kuwa na maumivu ya viungo, kichwa, kuishiwa maji mwilini na kuhisi kizunguzungu.
Baadhi yao wameripotiwa kupata upele mdogo ambao husambaa kwenye mikono na miguu.
Takriban watu 50, wengi wao wakiwa ni watoto wamekufa kwa homa hiyo, na mamia kadhaa wamelazwa hospitalini katia wilaya sita ambazo ni sehemu ya jimbo hilo lililopo kaskazini mwa nchi . Hakuna hata mmoja miongoni mwa waliokufa aliyepimwa Covid-19.
Wakati ambapo India inaonekana kuondokana taratibu na wimbi la pili la virusi vya corona, vifo katika Uttar Pradesh vimeibua wasi wasi huku vichwa vya habari vya vyombo vya habari kote nchini vilivyoandikwa ndikwa kuhusu "homa isiyojulikana " kote katika jimbo hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini India.
Madaktari katika wilya chache zilizoathiriwa - Agra, Mathura, Mainpuri, Etah, Kasganj na Firozabad - wanaamini dengue, ambayo ni maradhi yanayotokana na maambukizi ya mbu, huenda ikawa sababu kuuu ya vifo.
Wanasema wengi miongoni mwa wagonjwa walipelekw hospitalini wakiwa wamepungukiwa damu - sawa na inavyotokea kwa wagonjwa wa dengue.
"Wagonjwa, hususan watoto, katika hospitali wanakufa haraka sana ," anasema Dkt Neeta Kulshrestha, afisa wa ngazi ya juu zaidi wa afya wa wilaya ya Firozabad, ambako watu 40, wakiwemo watoto 32 wamekufa katika kipindi cha wiki moja iliyopita.
Ukiwambukizwa kwa njia ya mbu jike, ugonjwa wa dengue ambao zaidi ni ugonjwa wa maeneo ya joto umekuwa ukizunguka nchini India kwa miaka mamia kadhaa. Ni ugonjwa unaopatikana mara kwa mara katika zaidi ya nchi 100, lakini 70% ya wagonjwa huripotiwa katika bara la Asia. Kuna virusi vinne vya dengue, na watoto wanakabiliwa na uwezekano wa kufa mara tano wanapopata maambukizi ya pili ya dengue kuliko watu wazima.

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Karibu wagonjwa milioni 100 waliougua sana dengue - hupatwa na tatizo la kutokwa damu nyingi, kuharibika kwa viungo vya mwili huripotiwa kutoka maeneo mbali mbali kote dunia.
"Athari za majanga ya Covid-19 na dengue kwa pamoja zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa idadi ya watu `," kulingana na Shirika la afya duniani (WHO).
Hatahivyo bado haijawa wazi iwapo janga la dengue pekee ndilo linalosababisha vifo vinavyotokana na homa katika Uttar Pradesh.
Jimbo la Uttar Pradesh lenye idadi ya watu milioni 200 na lenye viwango duni vya usafi, viwango vya juu vya utapiamlo miongoni mwa watoto na ripoti za wagonjwa wa "homa ya ajabu " huripotiwa kila mwaka baada ya msimu wa mvua kila mwaka.
Mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na mbu -Japanese encephalitis - ambo kwa mara ya kwanza uligundulika katika jimbo la Uttar Pradesh katika mwaka 1978 - umesababisha vifo vya zaidi ya watu 6,500 tangu ugundulike.
Ugonjwa huu husambaa zaidi kupitia Gorakhpur na wilaya zinazopakana ambazo zinapatikana kwenye mpaka wa India na Nepal kwenye maeneo ya vilima vya Himalayas. Maeneo yote haya huathiriwa na mafuriko na hivyo kutoa eneo la mazalio ya mbu ambao husambaza virusi.
Kampeni ya chanjo, iliyoanza mwaka 2013, ilipelekea kushuka kwa idadi ya wagonjwa, lakini watoto bado wanaendelea kufa . Watoto 17 wamekufa kutokana na Japanese encephalitis katika jimbo la Gorakhpur mwaka huu na visa 428 vimerekodiwa.
Mwaka 2014, wansayansi waliwachunguza watoto 250 walioathiriwa na maambukizi ya encephalitis na myocarditis - magonjwa yanayosababisha vidonda kwenye mishipa ya moyo katika jimbo la Gorakhpur, baada ya watoto wengi kufa kutokana na maradhi hayo.
Walibaini kuwa 160 kati yao walikuwa na kingamwili dhidi ya kakteria ambayo ilisababisha maradhi ya Orientia Tsutsugamushi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maradhi ya Scrub typhus, ambayo pia yanafahamika kama bush typhus, ni maambukizi ya bakteria yanayosambaa kwa kuumwa na virusi vyenye maambukizi.
Mapema, katika mwaka 2006, wanasayansi walifanya uchunguzi kuhusu ''mlipuko mwingine wa ajabu'' wa homa-iliyohusishwa na vifo vya watu miongoni mwao watoto katika jimbo la Uttar Pradesh. TWakati huo waligundua kuwa watoto walikufa baada ya kula mbegu za mmea wa Kasia, ambao humea kwa wingi katika eneo la magharibi mwa jimbo.
Ulaji wa sumu hii ulitokana na "umasikini, njaa, ukosefu wa uangalizi wa wazazi, ujinga, watoto wanaoheza wenyewe, ukosefu wa vifaa vya watoto vya kuchezea na na urahisi wa watoto wa kufikia mimea hiyo",walisema wanasayansi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni wazi kuwa, ni uchunuzi zaidi ya mmoja na tathmini zaidi ndivyo vitakavyofichu ugonjwa wa sasa wa "homa ya ajabu" nchini India unasababishwa na dengue pekee, au imesababishwa na magonjwa mengine . Hii itamaanisha kliniki na hospitali zitatakiwa kufundishwa jinsi ya kukusanya sampuli za watu wanaoumwa homa na kuzituma katika maabara zinazopima na kubaini tabia za virusi.
Watu huvuta sigara na kutoa moshi ili kuwafukuza mbu katika jimbo la Allahabad., na pia hakuna rekodi ya wazi kuhusu jinsi homa zinavyoanza na kuendelea, na iwapo hali ya mgonjwa huwa mbaya kutokana na kuchelewa kwa mgonjwa kufika hospitalini.
Haijulikani pia iwapo watoto wenye homa hioyo waliugua zaidi kutokana na matatizo mengine ya kiafya waliyokuwa nayo kama vile kifua kikuu.
Kama sababu ya vifo vya ajabu ni dengue pekee, itaonesha ktokuwa na ufanisi kwa mipango ya serikali ya udhibiti wa mbu.
Kuongezeka kwa maambukizi, kulingana na Dkt Halstead, kunaweza tu kubainika kwa vipimo vya kingamwili - vinavyoitwa sero surveys - kwa kuzingatia makundi ya miaka.
"Kama hatutachunguza vyema na mara kwa mara, magonjwa mengi yataendelea kuwa ya ajabu," anasema mtaalamu wa virusi wa India ambaye hakupend jina lake litajwe.












