Afghanistan: Fahamu kwanini Taliban inataka taifa hilo kuwa Emirati ya Kiislamu

Chanzo cha picha, Getty Images
Afghanistan imebadilika kabisa ndani ya siku chache tu.
Baada ya kuchukua hatamu za nchi, ni habari kidogo sana ambazo zimekuwa wazi juu ya aina ya utawala ambao Taliban inataka kuunda.
Vikosi vya Marekani vina haraka ya kuondoka katikati ya machafuko yote yanayotokea katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, lakini ni jambo moja tu linaonekana wazi, historia ya 'Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan'.
Awamu mpya ambayo Afghanistan inapitia, sehemu za kwanza za historia ya nchi hiyo tayari zimeandikwa kama vile kuondoka kwa Rais Ashraf Ghani, kuanguka kwa Kabul, amri iliyo mikononi mwa Taliban na hamu ya Taliban kuifanya Afghanistan iwe Emirati ya Kiislamu Emirate.
Kuna ukweli pia kwamba Taliban inajielezea kama 'Emirati ya Kiislamu ya Afghanistan'.
Makubaliano ya Mkataba wa Doha wa mwaka 2020 pia yalifikiwa kwa jina hilo
Hati hii ndio tangazo la kwanza la Marekani kuondoka Afghanistan.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasemaji wa Taliban wamerejelea mara kadhaa " Mkataba wa Doha" katika siku za hivi karibuni, na Zabihullah Mujahid ameiita Afghanistan kwa jina hilo hilo katika mikutano yake na waandishi wa habari.
Lakini hilo limeanza kupokelewa kwa mtazamo tofauti. Hii imekuwa wazi kutokana na maandamano katika miji kama Kabul, Jalalabad na Asadabad.
Hapa waandamanaji waliobeba bendera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan walifutwa kazi.
Taliban wameamua kuwa sasa watatumia bendera yao badala ya bendera hii.
Mabadiliko haya yanayofanywa kwa jina la Afghanistan yatakuwa na athari za kisiasa, kiitikadi na kidini.
Mabadiliko haya pia yataathiri uhusiano ambao Afghanistan na watu wake wanao na ulimwengu wa Kiislamu na jamii yote ya kimataifa kijumla.

Chanzo cha picha, Getty Images
Emirati 'Emirates' ni nini na inamaanisha nini?
Kuna nchi kama hizo katika eneo la Ghuba ya Uajemi kama Qatar na Kuwait.
Jina la Falme za Kiarabu linaonyesha kuwa ni shirikisho la emirati.
Javier Guirado, mtaalam wa maswala ya Mashariki ya Kati katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Georgia, anasema, "Katika jamhuri, rais sio kiongozi wa kidini, lakini kwa emirati, mkuu wa nchi ni kiongozi wa dini. Mamlaka ya kisiasa na kidini yamejikita kwa mtu mmoja , na kwamba Mtu huyo ni Aamir wa nchi.
"Ni kawaida katika nchi nyingi za Kiislamu kuwa madaraka ya kisiasa na kidini yamepewa mtu yule yule.
Thomas Barfield, mtaalam wa anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Boston, anasema kwamba "jina la Amir limeanza wakati wa Amir Alumminin. Maana yake ni "kamanda wa watu waaminifu". Wakati wa Mtume Muhammad (S.A.W) wakuu wengine wa jeshi walitumia jina hili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Thomas Barfield anasema kwamba kile Taliban wanachozungumzia ni tofauti na khalifa ya Kiislamu.
"Islamic State inasema mpango wake ni kuushinda ulimwengu kwa kuhakikisha kuwa utawala wa ukhalifa wake umeanzishwa kwa Waislamu wote, bila kujali wanapoishi. Wakati Taliban inajiona kama taasisi huru ya kisiasa ambayo upeo wake ni mdogo kwa watu wanaoishi katika ardhi ya Afghanistan", Javier Guirado anasema, "Dhana ya ukhalifa ilianzia kipindi cha makhalifa wanne, wakati ulimwengu wa Kiislam ulitawaliwa moja kwa moja na warithi wa Nabii Muhammad katika karne ya saba." Thomas Barfield anaelezea kwamba "wakati utawala wa ukhalifa unapoanza kudhoofika, utawala wa emirati na masultani huanza.
Kwa hivyo ni nani atakayeshinda emirati ya Taliban na ukhalifa wa Islamic State?
Thomas Barfield anajibu, "Vikundi vyote viwili vinaangaliana kama maadui. Itafurahisha kuona ikiwa Islamic State itaanzisha msururu wa mashambulizi ya mabomu huko Kabul.
Ilikuwa ni mwendelezo wa kile kilichotokea katika uwanja wa ndege wa Kabul Alhamisi.
Marekani inataka kuamini ahadi ya Taliban kwamba ardhi ya Afghanistan haitatumika dhidi ya masilahi ya nchi za Magharibi, lakini kundi lenye msimamo mkali, ambalo linajiita "Islamic State" lina mtazmo tofauti.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwanini Emirati?
Javier Guirado anasema, "Sababu ya kuchagua mfumo wa Emirati ni mizizi yake katika utamaduni wa siasa ya Taliban".
Marehemu Mullah Omar, ambaye alishikilia hatamu ya utawala wake hadi kuanguka kwa Taliban mnamo 2001, alikuwa akishikilia jina la Amir.
Xavier anasema kwamba wakati kundi jipya na familia tofauti inapoingia madarakani, inachukua jina la Amir kupata hadhi yake ya kisiasa.
Afghanistan hadi sasa imepitisha mifumo kadhaa ya kisiasa.
Pia ilikuwa na ufalme wa kikatiba wa Mohammad Zahir Shah, ambaye aliondolewa mamlakani mnamo 1973 baada ya uasi.
Jamhuri ya Kiislamu ilianzishwa baada ya kuwasili kwa Marekani mnamo mwaka 2001, lakini Taliban kila wakati ilitaka kurejesha mfumo wa zamani wa emirati.
Na sasa ni hakika kwamba watafaulu.
Hata hivyo, Waafghanistan wengi wanaogopa kwamba inaweza kumaanisha kurudi kwa serikali udhalimu na yenye vurugu ya miaka ya tisini.अफ़ग़ानिस्तान में तालिबान की जीत क्या 'पाकिस्तान की जीत' है?

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Emirati itakuwaje?
Watu wengi wanauliza swali hili kwamba serikali ya mfumo wa Emirati nchini Afghanistan itakuwaje?
Mnamo mwaka 2004, wakati Afghanistan ilikuwa chini ya ushawishi wa nchi za magharibi, katiba iliyotengenezwa wakati huo iliipa nchi hiyo hadhi ya kuwa Jamhuri ya Kiislamu.
Katika hili, mfumo wa serikali ya kidemokrasia, unaoendeshwa kwa kuzingatia matakwa ya watu maarufu, ulipangwa.
Lakini sasa katiba hii imekuwa hati iliyokufa.
Thomas Barfield anasema, "Ni hakika kwamba Taliban hawataandika katiba mpya kwasababu sheria za Uislamu yaani Sharia zinatosha kwao.
Hakutakuwa na uchaguzi tena nchini Afghanistan kwasababu uhalali wa utawala wa Taliban hautategemea dhamira ya watu.
Badala yake, mfumo huo utaendeshwa kwa madai kwamba ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu. "Yeyote atakayekuwa Amir wa serikali ya Taliban, atakuwa na nguvu za kisiasa na kimahakama, pia atakuwa na nguvu za kidini.
Lakini je! Atatawala milele? Thomas Barfield anasema, "Ikiwa utaangalia vile utawala ulivyokuwa zamani nchini Afghanistan, utawala wa viongozi wengi umeisha kwa kifo chao au kuhama nchi na kwenda kwengine."

Chanzo cha picha, Reuters
Je hali ya wanawake itakuwaje?
Je! kutakuwa na ushiriki wowote wa wanawake katika kujadiliana kweye suala la madaraka?
Kwa sasa, hili halionekani kutokea wala hakuna tumaini lolote juu yake.
Kuruhusu wasichana kusoma na kufanya kazi tu inamaanisha kuwa msimamo wa zamani wa Taliban umebadilika.
Lakini katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, kumekuwa na mabadiliko kadhaa nchini Afghanistan, ambayo yatachukua muda kuondoka na Taliban italazimika kushughulika hayo kuanzia sasa kuendelea.
Javier Guirado anaonya kuwa, "Uhuru wa sasa wa Afghanistan ni ule wa kujifunza zaidi kuliko hapo awali. Hasa katika miji, wanatumia mtandao. Wamekuwa wakipiga kura. Kwa hivyo, Taliban huenda ikakataa kutawala kama mara ya mwisho walivyokuwa madarakani."
"Ikiwa Taliban itaanza kukandamiza watu na kutumia nguvu, itakuwa na shida kupata kutambuliwa kimataifa na italazimika kukabiliwa na athari za kidiplomasia na kiuchumi".
Thomas Barfield anasema, ."Swali ni ikiwa Taliban wamejifunza somo kwamba watalazimika kufanya mapatano na maadui zao ili kutawala nchi."












