Uhalisia: Sauti ya nyoka-kayamba inapumbaza masikio ya mwanadamu

Nyoka kayamba au 'Rattlesnake' wamekuwa werevu na kubadilisha njia ya kuwashawishi binadamu kuwa hatari iko karibu kuliko vile wanavyofikiria, wanasayansi wanasema.

Sauti za mkia wao unaotikisika huongezeka zaidi mtu anapokaribia lakini ghafla hubadilika na kuwa katika mzunguko wa haraka sana.

Katika majaribio, mabadiliko ya haraka ya sauti yalifanya washiriki waamini nyoka alikuwa karibu sana kuliko ilivyokuwa katika hali halisi.

Watafiti wanasema tabia hiyo ilibadilika kusaidia nyoka kuepuka kukanyagwa.

Sauti ya kelele ya kuchatachata ya mkia wa nyoka aina hiyo kwa muda mrefu imekuwa ikioneshwa kwenye sinema.

Hadithi ya nyoka huyo inatokana na kutingisha kwa haraka kwa pete ngumu za keratin kwenye ncha ya mikia ya wanyama wanaotambaa.

Keratin ni protini sawa ambayo hutengeneza kucha na nywele zetu.

Cha msingi katika kelele hizo ni uwezo wa nyoka kutikisa misuli yake ya mkia hadi mara 90 kwa sekunde.

Kutetemesha mkia namna hiyo kunatumika kuonya wanyama wengine na wanadamu juu ya uwepo wao.

Pamoja na hayo, nyoka aina ya kayamba 'rattlesnakes' bado ndio wanaowajibika kwa kuuma watu wengi kama 8,000 au zaidi kila mwaka nchini Marekani.

Watafiti wamejua kwa miongo kadhaa kwamba haraka hiyo inaweza kubadilika lakini kumekuwa na utafiti mdogo juu ya umuhimu wa mabadiliko ya sauti.

Katika utafiti huu, wanasayansi walijaribu kwa kusongesha kitu mfano wa sehemu ya juu ya mwanadamu karibu na nyoka wa magharibi na kurekodi kilichotokea.

Wakati kitu hicho kilipokaribia nyoka, kutingishika kuliongezeka kwa masafa ya hadi karibu 40Hz.

Hii ilifuatiwa na kuongezeka ghafla kwa sauti iliyobadilika na kuwa ya masafa ya juu kati ya 60-100Hz.

Ili kujua mabadiliko hayo ya ghafla yalimaanisha nini, watafiti walishirikiana zaidi na binadamu kwenye majaribio ya nyoka ambaye hakuwa halisi.

Kiwango cha kuongezeka kwa kutingisha mkia kiligunduliwa na washiriki wakati sauti inaongezeka kila wanapoendelea kusongea karibu.

Wanasayansi waligundua kuwa wakati mabadiliko ya ghafla ya masafa yalitokea kwa umbali wa mita 4, watu katika jaribio hilo waliamini ilikuwa karibu zaidi, karibu umbali wa mita moja.

Waandishi wanaamini kubadilika kwa sauti sio tu onyo rahisi, lakini ishara isiyo na kawaida ya mawasiliano ya jamii mbalimbali za viumbe.

"Kubadilika huko kwa ghafla hadi masafa ya juu ni kama ishara nzuri inayompumbaza msikilizaji kuhusu umbali wake halisi na chanzo cha sauti," anasema mwandishi mwandamizi Boris Chagnaud kutoka Chuo Kikuu cha Karl-Franzens-Graz, Austria.

"Tafsiri isiyo sahihi ya umbali na msikilizaji hutengeneza umbali kwa ajili ya usalama."

Waandishi wanaamini kuwa tabia ya nyoka inatumia vibaya mfumo wa ukaguzi wa binadamu, ambao umebadilika kutafsiri kuongezeka kwa sauti kubwa kama kitu kinachokwenda kwa kasi na kukaribia.

"Mageuzi ni mchakato usio na utaratibu maalum, na kile tunaweza kutafsiri kutokana na mtazamo wa leo kama ubunifu wa kifahari ni matokeo ya maelfu ya majaribio ya nyoka kukabiliana na wanyama wakubwa wanaonyonesha yaani mamalia," alisema Dk Chagnaud.

"Sauti ya nyoka ilibadilika na mtazamo wa ukaguzi wa mamalia wakati wa majaribio, na kuwaacha wale nyoka ambao waliweza kuzuia kukanyagwa."