Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 13.08.2021: Kane, Ronaldo, Coutinho, Rudiger, Locatelli, Ward-Prowse, Costa, Doku
Paris St-Germain itatafuta kusaini mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, kutoka Juventus msimu wa joto wa 2022 kama mbadala wa mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Kylian Mbappe, ambaye amekuwa lengo la muda mrefu la Real Madrid. (AS - in Spanish)
Juventus iko tayari kukamilisha mpango wa kumnasa kiungo wa kati wa Sassuolo wa Italia Manuel Locatelli, ambaye Arsenal ilikuwa ikihusishwa naye(Goal)
Manchester City wako tayari kulipa € 150m (£ 127m) kumsajili mshambuliaji wa England Harry Kane, 28, kutoka Tottenham. (Guardian)
Kane ana matumaini kuwa hatima yake itakuwa wazi zaidi wiki ijayo baada ya Spurs kuanza kampeni yao ya Ligi Kuu nyumbani dhidi ya City, klabu inayomtaka.(Telegraph, subscription required)
Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho amehusishwa na kurudi Liverpool akitokea Barcelona, kilabu alichoondoka Merseyside kujiunga nacho kwa pauni milioni 142 mnamo Januari 2018. Everton, Manchester United, Chelsea, Arsenal, Tottenham na Leicester City hivi karibuni wamehusishwa na nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 (Liverpool Echo)
Liverpool inasemekana pia inavutiwa na fowadi wa Ubelgiji Jeremy Doku kutoka Rennes, ambayo itahitaji pauni milioni 38 kwa mchezaji huyo wa miaka 19. (Voetbal24 - in Dutch)
Kocha wa the Reds Jurgen Klopp, hata hivyo, amesema kilabu "haitaki wachezaji zaidi".(Mail)
Real Madrid na Paris St-Germain wanafuatilia hali ya beki wa kati wa Ujerumani, Antonio Rudiger huko Chelsea, wakijua kwamba makubaliano ya mkataba wa mapema yanaweza kusainiwa na mchezaji huyo wa miaka 28 mnamo Januari. (Sky Sport)
Tottenham inaweza kumchukua beki wa Villarreal mwenye umri wa miaka 24, Pau Torres. (Express)
Crystal Palace wamejiandaa kushindana na Leeds United katika harakati zao za kumfuata kiungo wa kati wa Uingereza na Huddersfield Town mwenye umri wa miaka 22, Lewis O'Brien(Football Insider)
Kocha wa Southampton Ralph Hasenhuttl ameazimia kumbakisha kiungo wa England mwenye umri wa miaka 26 James Ward-Prowse, ambaye anatafutwa na Aston Villa na Tottenham. (Football London)
Manchester United wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ivory Coast wa miaka 19 Amad Diallo aondoke kwa mkopo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)
West Ham imepata pigo baada ya ofa yao ya pauni milioni 17 kwa beki wa Morocco mwenye umri wa miaka 25 Nayef Aguerd kukataliwa na Rennes. (Football Insider)
Leeds United inaweza kufanya juhudi mpya kumsaini mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 Kent Ryan kutoka Ranger baada ya kampeni ya klabu hiyo ya scotland ya Ligi ya Mabingwa kumalizika. (Athletic, subscription required)
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta bado ana matumaini ya usajili zaidi kabla ya tarehe ya mwisho ya uhamisho. (ESPN)
Mshambuliaji wa Uhispania Diego Costa, 32, yuko mbioni kuanza tena taaluma yake huko Brazil na Atletico Mineiro, kwani hajacheza tangu alipoondoka Atletico Madrid mnamo Desemba (Goal)
Mlinda lango wa Barcelona mwenye umri wa miaka 32, Neto anaweza kuhamia Arsenal katika msimu huu wa joto, lakini uhamisho wa mkopo pia unawezekana .(Athletic - subscription required)