Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Zambia: Je vijana ndio wenye kura ya turufu?
Zambia inatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa urais na ubunge siku ya Alhamisi na wapiga kura wengi - haswa vijana - wana wasiwasi juu ya msukosuko wa uchumi ambao umelikumba taifa hilo lenye utajiri wa shaba.
Chama tawala cha Patriotic Front (PF) kiliingia madarakani mwaka 2011 kwa ahadi ya "ushuru mdogo, pesa zaidi mifukoni mwa watu na ajira zaidi". Inasema imedumisha sera zake kuwajali maskini.
"Hatua kubwa imechukuliwa kukwamua uchumi na sasa tunaelekea kurejea kwenye mkondo," msemaji wa kampeni ya PF Amos Chanda alisema
Lakini chama kikuu cha upinzani cha United Party for National Development (UPND )kinasema Rais Edgar Lungu - ambaye anagombea mhula mwingine - hajafikia matarajio ya Wazambia.
Kauli hiyo inaungwa mkono na mhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Zambia Charity Musamba.
"Tumeshuhudia uharibifu mkubwa wa rasilimali,ambao umechangia changamoto za kiuchumi zinazoshuhudiwa nchini," aliiambia BBC.
Chama cha PF kinasema katika miaka yake 10 madarakani kimeimarisha maisha ya watu kupitia mpango wake mkuwa wa kupanua miundo msingi.
Kinaangazia viruo vipya vya umeme, shule, hospitali na uwana wa kimataifa wa ndege katika mji mkuu wa Lusakana ndula ambayo ni njia kuu ya kueleke maeneo ya uchimbaji madini ya copper ambayo ni chanzo kikuu cha uchumi wa Zambia.
BLakini wakosoaji wake wanasema uchumi unakabiliwa na hali mbaya.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998, Zambia ilitumbukia kwenye mgogoro wa uchumi mwaka jana wakati janga la Covid-19 lilipotangazwa kote duniani.
Kando na hayo Shirika la kimataifa la wafanyakazi (ILO) linakadiria kwamba ukoseru wa ajira ulipanda kwa asilimia 12.17 mwkaka 2020 - kiwango cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu chama cha PF kiliingia madarakani mwaka 2011.
Hali imekuwa mbaya zaidi kwa vijana,ikikadiriwa kuwa mmoja kati ya watu watatno hana kazi. Gharama ya maisha pia ilipanda zaidi.
Nchi hiyo pia inadaiwa na wakopeshaji wa kigeni deni linalokadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni 12 sawa na (£8.6bn).
Hii inamaanisha kuwa serikali inatumia hadi asilimia 30 ya mapato yake kulipa riba kulingana na shirika la kimataifa la S&P linalokadiria viwango vya madeni.
Mwaka jana Zambia ilikosa kulipa deni, na kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kushindwa kulipa deni lake wakati wa janga la corona. Pia inakabiliwa na changamoto ya kilipa mikopo mingine.
Uchaguzi nchini Zambia kwa kiasi kikubwa huambuliwa na vijana wanaojumuisha wapiga kura wa mara ya kwanza.
'Napigia kura kazi yanguI'
Zaidi ya nusu ya wapiga kura milioni nane waliosajiliwa wana umri wa chini ya miaka 35. Zamani wao pamoja na wapiga kura wa mjini walikuwa wafuasi shakiki wa chama tawala cha PF.
Lakini kutokana na kudorora kwa uchumi, Bw. Lungu na chama chake hawawezi kutegemea kura yao kirahisi.
"Simpigii kura mtu yeyote katika uchaguzi huu - Napigia kura kazi yangu. siwezi kuishi bila kazi kwa miaka minne," anasema Silvia Mutila, nesi wa miaka 25 ambaye hana ajira ijapokuwa alihitimu mwaka 2017.
Licha ya uhaba wa wafanyakazi muhimu katika sekta ya elimu na afya, Zambia ina zaidi ya walimu 50,000, manesi 17,000 na madaktari 500 ambao hawana ajira.
Serikali imekuwa ikibuni na 650 za afya kwa kutumia mkopo kutoka kwa benki ya EXIM ya India, huku baadhi ya hospitali zikijengwa kwa kutimia mikopo kutoka kwa wakopeshaji wengine.
Na uchumi unakadiriria kukuwa kwa karibu asilimia 1.5% mwaka huu, kutokana na ongezeko la bei ya madini ya copper, mavuno mazuri na kuimarishwa kwa uwezo wa uzalishaji umeme.
Chama cha upinzani cha UPND na mgombea wake wa urais - mafanyabiashara tajiri Hakainde Hichilema - wanatarajiwa kudumisha uungwaji mkono wao katika Jimbo la Kusini, Mkoa wa Magharibi na Mkoa wa Kaskazini-Magharib wenye utajiri wa madini.
Wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika mara kwa mara kwamba hakuma maendeleo ya kiuchumi licha ya kuwa na igodi mikubwa ya madini
Wengine wanaamini chama cha kisosholisti cha upinzani - ambacho kilishiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi kufuatia uzinduzi wake mwaka 2018 - kimefanikiwa kujiimarisha katika Mkoa wa Magharibi.
Hapa ni mahali ambapo mwanahabari aliyegeuka mwanasiasha, Fred M'membe,alikulia na amefanya kampeni kubwa kuwashawishi wamuunge mkono.
Anasadikiwa pia kumegua ufuasi wa UPND katika Mkoa wa Kaskazini- Magharibi, mwanauchumi wa Lusaka, Oliver Saasa, anasema hatarijii kuona mabadiliko makubwa katika mwenendo wa wapiga kura hasa katika maeneo ya mashambani ambayo ni ngome ya vyama viwili vikuu.
'Kulengwa kwa wanahabari na wanaharakati'
Rais Lungu ameshtumiwa kwa kuonyesha sifu za kimabavu dhidi ya mpinzani wake Bwana Hichilema, ambaye alimshindwa katika chaguzi tano za urais.
Mnamo mwezi Juni, shirika la kutetea haki la Amnesty International lilitoa ripoti kwa jina Kutawala kwa Hofu na Ukandamizaji.
"Viongozi wa upinzani, waandishi wa habari, vyombo vya habari na wanaharakati wamekuwa wakilengwa, na kuangazia madai ya ufisadi au unyanyasaji wa serikali imekuwa hatari zaidi, "Amnesty ilisema.
Pia ilidai kuwa nguvu zaidi hutumiwa wakati mwingine kuvunja maandamano.
Kampeini ya Bw. Hichilema inasema vikosi vya usalama vimedhibiti vikali juhudi zao za kutafuta uungwaji mkono, huku Rais Lungu na mgombea mwenzake, mwanabiolojia Nkandu Luo, wakizuru maeneo tofauti ya Zambia bila vikwazo.
Mapema mwezi huu, Bw Lungu aliamuru kupelekwa kwa wanajeshi sehemu za Lusaka, kufuatia kuuawa kwa wafuasi wawili wa PF katika makabiliano na wafuasi wa UPND katika eneo la Kanyama mwishoni mwa mwezi uliopita.
Upinzani ulikosoa hatua hiyo, ukisema unaweza kuwatisha wapiga kura.
Uchaguzi huo unafuatiliwa kwa karibu na serikali za kigeni - ikiwemo Marekani.
Katika taarifa, ubalozi wake mjini Lusaka umesema wale ambao wanaendeleza vurugu au wanaodhoofisha uchaguzi watawajibishwa.
Raia wa Zambia wana matumaini kwamba wanasiasa watadumisha amani.