Wagner: Oparesheni ya mamluki wa Urusi nchini Libya yafichuliwa

Uchunguzi mpya wa BBC umebaini kiwango cha oparesheni inayofanywa na mamluki wa Urusi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo inahusisha jeshi la Urusi na uhalifu wa kivita.
Tableti ya Samsung iliyoachwa nyuma na mpiganaji wa kundi la Wagner ilifichua jukumu lake muhimu - Pamoja na majina fiche
Na BBC ina "orodha ya ununuzi" ya vifaa vya kisasa vya kijeshi ambavyo mashahidi wataalamu wanasema vinaweza tu kutoka kwa jeshi la Urusi
Urusi imekana kuwa na uhusiano na Wagner.
Kundi hilo lilitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014 lilipounga mkono mara waaasi wanaounga mkono Urusi katika mzozo mashariki mwa Ukraine
Tangu wakati huo, limejiusisha katika maeneo kadhaa ikiwa ni Pamoja na Syria, Msumbiji, Sudan, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wapiganaji wa Wagner waliingia Libya Aprili mwaka 2019 wakati walipoungana na vikosi vya jenerali muasi, Khalifa Haftar, baada ya kushambulia serikali inayoongwa mkono na Umoja wa Mataifa katika mji mkuu, Tripoli.
Mzozo huo ulimalizika baada ya kusitishwa kwa mapigano mwezi Oktoba mwaka 2020.
Kundi hilo linaendesha shughuli zake kwa usiri mkubwa , lakini BBC imefanikiwa kupata nafasi adimu ya kuzungumza na wapiganaji wawili wa zamani. Walifichua ni mtu wa aina gani alijiunga na Wagner - na ukosefu wake wa kanuni yoyote ya inayoongozo utendakazi.
Hakuna shaka kuwa wanawaua wafungwa - kitu ambacho mpiganaji wa zamani wanakubaliana wazi wazi. "Hakuna mtu anayetaka kinywa cha ziada kulisha."
Hii inaenda sambamba na sehemu zingine za makala maalum ya Tevisheni -Mamluki wa Kirusi wa Haftar: Fahamu Kikundi cha Wagner - na BBC Idhaa ya Kiarabu na BBC Idhaa ya Kirusi. Ufichuzi wake mwingine ni pamoja na ushahidi wa watuhumiwa wa uhalifu wa kivita, pamoja na mauaji ya kukusudia ya raia.
Mwanakijiji mmoja wa Libya anaelezea jinsi alivyojianya amekufa wakati jamaa zake walipouawa. Ushuhuda wake ulisaidia timu ya BBC kumtambua muuaji anayeshukiwa.
Akielezea uhalifu mwingine wa kivita, mwanajeshi wa serikali ya Libya pia anakumbuka jinsi afisa mwezake na rafiki yake, alijisalimisha kwa wapiganaji wa Wagner lakini alipigwa risasi mara mbili tumboni
Mwanajeshi huyo hajawahi kumuona tena tangu wakati huo, au marafiki wake wengine waliochukuliwa wakati mmoja.

Kompyuta hiyo ya Samsung pia ilitoa ushahidi wa kuhusika kwa mamluki katika uchimbaji madini na kutegwa kwa mabomu ya ardhini katika maeneo yanayokaliwa na raia.
Kutega bomu la ardhini bila kuweka alama ni uhalifu wa kivita.
Ufichuzi wa kompyuta ndogo ya Samsung
Tableti hiyo iliachwa nyuma na mpiganaji wa Wagner asiyejulikana baada ya waoiganaji wa kundi hilo kurejea nyuma katika maeneo ya kusini mwa Tripoli msimu wa spring wa mwaka 2020.
Yaliyomo ni pamoja na ramani ya sehemu ya vita ya Urusi, hii ikiwa ni uthibitisho wa jukumu muhimu la Wagner na maelezo ya kina ya oparesheni ya kundi hilo.
Kuna kanda ya video iliyonaswa kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani na majina ya kisiri ya wapiganaji wa Wagner, angalau mmoja ambayo BBC inaamini kutambua. Kompyuta hiyo sasa imehifadhiwa mahali salama.

Orodha ya silaha
Orodha kamili ya silaha na vifaa vya kijeshi imejumuishwa katika waraka wa kurasa 10 wa tarehe 19 Januari 2020, uliyopewa BBC na chanzo cha ujasusi cha Libya na labda iilipatikna kutoka eneo la Wagner.
Hati hiyo inaonyesha ni nani anayeweza kufadhili na kuunga mkono shughuli hiyo. Inaorodhesha vifaa vinavyohitajika kwa "kukamilisha malengo ya kijeshi" - pamoja na mizinga minne, mamia ya bunduki za Kalashnikov na mfumo wa kisasa wa rada.
Mchambuzi wa kijeshi aliiambia BBC kwamba baadhi ya teknolojia ya silaha inapatikana tu kutoka kwa jeshi la Urusi. Mtaalam mwingine wa kikundi cha Wagner, alisema orodha hiyo inaashiria kuhusika kwa Dmitry Utkin.
Yeye ni afisa zamani wa ujasusi wa jeshi la Urusi anayeaminika kuwa alianzisha Wagner na kuipatia jina lake (jina lake la zamani la kivita). BBC ilijaribu kuwasiliana na Dmitry Utkin lakini haijapata jibu.
Na katika uchambuzi wetu wa kuona kilichomo katika "orodha ya ununuzi" na hati nyingine, mtaalam anasema majina ya Evro Polis na Mkurugenzi Mkuu yanaonekana kuhusika kwa Yevgeny Prigozhin, mfanyabiashara tajiri ambaye ni mshirika wa Rais Vladimir Putin.
Hazina ya kitaifa ya Marekani iliitilia vikwazo Evro Polis mnamo 2018, na kuiita kampuni ya Kirusi iliyopewa kandarasi ya "kulinda" viwanja vya mafuta huko Syria ambavyo "vinamilikiwa au kudhibitiwa" na Bwana Prigozhin.
Uchunguzi wa waandishi wa habari wa Magharibi umemhusisha Bwana Prigozhin na Wagner. Amekataa kuwa na uhusiano wowote na Evro Polis au Wagner.
Msemaji aliiambia BBC kwamba Yevgeny Prigozhin hana uhusiano wowote na Evro Polis au Wagner. Bwana Prigozhin alitoa maoni kuwa alikuwa hajasikia chochote juu ya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Libya na Warusi: "Nina hakika kuwa huu ni uwongo mtupu."
Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Urusi iliambia BBC inafanya "yote iwezalo kuleta usitishaji wa mapigano na suluhu ya kisiasa kwa mzozo nchini Libya."
Wizara hiyo iliongeza kuwa maelezo juu ya Wagner nchini Libya yanategemea zaidi "data za wizi" na zililenga "kudhalilisha sera ya Urusi" nchini Libya.
Wagner ni nini? Wapiganaji wake wa zamani wazungumza
Kirasmi kampuni hiyo haipo - lakini hadi watu 10,000 wanaaminika kuchukua angalau kandarasi moja na Wagner tangu ilipoibuka kupigana pamoja na wapiganaji waliotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine mnamo 2014 walio na uhusiano na Urusi.
Karibu wanaume 1,000 wa Wagner wanakadiriwa kupigana na Jenerali Khalifa Haftar huko Libya kutoka 2019 hadi 2020.
BBC nchini Urusi iliuliza mmoja wa wapiganaji wa zamani aileze Wagner. Alijibu: "Ni muundo, unaolenga kulinda masilahi ya serikali nje ya mipaka ya nchi yetu."
Kwa wapiganaji wake, alisema labda walikuwa "wataalamu wa vita", watu wanaotafuta kazi, au wanaopenda kutumikia nchi yao.
Mpiganaji mwingine wa zamani aliiambia BBC hakukuwa na sheria wazi za mwenendo. Ikiwa mfungwa aliyekamatwa hakuwa na ujuzi wa kujifanya amepoteza fahamu , au hakuweza kufanya kazi kama "mtumwa", basi "matokeo ni dhahiri".
Andrey Chuprygin, mtaalam anayefanya kazi na Baraza la Kimataifa la Urusi, alisema msimamo wa serikali ya Urusi ulikuwa - "wacha wajiunge na jambo hili, na tutaona ni nini matokeo yake . Ikiwa inafanya kazi vizuri, tunaweza kuitumia kwa faida ikiwa inageuka vibaya, basi hatukuwa na uhusiano wowote nayo ".

Libya - Muongo wa machafuko
Kuanguka kwa utawala wa Gaddafi mnamo 2011: utawala Kanali Muammar Gaddafi wa zaidi ya miongo minne unaishia katika ghasia baada ya mapinduzi ya Kiarabu. Anajaribu kukimbia lakini anakamatwa na kuuawa
Mgawanyiko wa nchi: Baada ya 2014, vikundi vikubwa vyenye silaha vinaibuka mashariki na magharibi
Waaasi waelekea Tripoli mnamo Aprili 2019: Jenerali Haftar, kiongozi wa vikosi vya mashariki, aelekea kuuteka mji wa Tripoli na serikali inayoungwa mkono na UN huko. Pande zote mbili zinapata msaada wa kijeshi na kidiplomasia kutoka kwa mamlaka tofauti za kieneo, licha ya zuio la silaha la UN
Vita kusistishwa mnamo Oktoba 2020:Mwanzoni mwa 2021 serikali mpya ya umoja yachaguliwa na kuapishwa, kupeleka taifa kwenye uchaguzi mnamo Desemba. Wapiganaji wa kigeni na mamluki walipaswa kuondoka, lakini maelfu wanasalia nchini humo

















