Makabubri yanayoashiria unyama uliofanywa na 'Familia ya Jehanamu' Libya

Wadah al-Keesh

Kwa miaka kadhaa walifahamika kama familia kutoka jehanamu.

Hadi msimu wa joto uliyopita, ndugu hao wa Kani waliudhibiti mji mdogo Libya, kuwaua wanaume , wanawake na watoto kudumisha mamlaka yao.

Sasa uhalifu wao umeanza kufichuliwa pole pole.

Kwa miaka saba wafanyakazi, waliovalia suti nyeupe za kujilinda dhidi ya kemikali wamekuwa wakirejea katika mji mdogo wa kilimo Tarhuna, uliopo kusini- mashariki mwa mji kuu wa Libya, Tripoli.

Wameweka alama katika ploti ambazo wametoa miili 120 kwa kutumia tepu nyekundu na nyeupe japo sehemu kubwa ya ardhi hiyo haijaguswa.

"Kila wakati ninapochimba mwili mpya, najaribu kufanya hivyo kwa umakini kadri ya uwezo wangu," anasema mmoja wa wafanyakazi wa, Wadah al-Keesh. "Tunaamini kwamba tukivunja mfupa, roho yake itasikia."

Baadhi ya miili hiyo inasadikiwa kuwa ya wapiganaji wadogo waliouawa vitani karibu na Tarhuna msimu uliyopita wa joto, katika mwaka wa tisa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya.

Lakini wengi wao ni raia - wakiwemo wanawake na watoto wadogo waliyo na umri wa hadi maka mitano - baadhi yao wakiwa na alama za kuteswa.

Makaburi hayo ni ishara inayoangazia utawala wa ugaidi uliyodumu kwa karibu miaka minane, ukiendeshwa na familia ya Kanis, na wanamgambo wao.

Watatu kati ya ndugu saba wa Kani wamefariki, na wengine walitoroka mwezi Juni mwaka 2020 bade ya kushambuliwa na vikosi tiifu kwa Serikali ya Muungano ya Libya(GNU) inayotambuliwa na Umoja wa mataifa, lakini mpaka sasa wakazi wa Tarhuna wanaogopa kuzungumzia uhalifu wao.

Baadhi yao wanasema kuwa wanatishiwa na wafuasi wa ndugu wa Kani.

Kukusanya pamoja taarifa kuwahusu ndugu hao - Abdul-Khaliq, Mohammed, Muammar, Abdul-Rahim, Mohsen, Ali na Abdul-Adhim sio mambo rahisi.

Lakini kutokana na simulizi za kuogofya kutoka kwa watu waliowajua, familia hiyo masikini ilitumia ghasia iliyokumba Libya baada ya mapinduzi ya mwaka 2011 dhidi ya, Kanali Muammar Gaddafi - na kuongoza jamii yao kwa kutumia ukatili mkubwa.

Two of the brothers' lions

"Ndugu hao saba walikuwa wabaya sana na wala hawakuwa na ustaarabu katika jamii," anasema Hamza Dila'ab, wakili na mwanaharakati wa kijamii, ambaye anakumbuka kukutana nao katika maharusi na mazishi kabla ya mwaka 2011.

Mapinduzi yalipofanyika, watu wengi katika mji wa Tarhuna walisalia kuwa watiifu kwa Gaddafi.

Koingozi huyo wa kiimla aliupendelea sana mji huo, kwa kuwapatia wanaume kutoka familia kubwa kazi nzuri katika vikosi vyake vya usalama.

Familia ya Kani ilikuwa miongoni mwa watu wachache waliounga mkono mapinduzi - lakini sio kwa maslahi ya wananchi, anasema Hamza Dila'ab, bali ni kutokana na uhasama wa miaka 30 kati yao na ndugu wa familia ya wafuasi wa Gaddafi.

Baada ya kung'olewa madarakani kwa Gaddafi, ndugu hao walipata nafasi ya kutekeleza maovu yao.

" Ndugu wa Kani walifanikiwa kuua familia hiyo kisiri mmoja baada ya mwingine ," anasema Hamza Dila'ab.

Lakini msururu huo wa mauaji ya kulipiza kisasi ilichangia kuawa kwa ndugu mdogo wa Kani, aliyefahamika kama Ali mwaka 2012.

"Ali alikuwa ndugu mdogo mtanashati wa Kani, na alipofariki,alimfanya shujaa,"anasema Jalel Harchaoui, mtaalamu wa Libya katika taasisi ya Clingendael nchini Uholanzi, ambaye alifanya utafiti wa historia ya familia hiyo.

Three of the brothers
Maelezo ya picha, Mohammed al-Kani,Salafist (kushoto),na wauaji wengine wawili wakuu ni, Mohsen na Abdul-Rahim
1px transparent line

"Ndugu hao waliamua kulipiza kisasi kifo chake sio tu kwa kuwasaka waliohusika na mauaji yake na kuwaua. Walichofanya ni kuangamiza familia yao yote ."

Familia ya Kani iliendelea mbele kwa kuimarisha vikosi vilivyokuwepo mjini humo na kabuni vikosi vyao vipya vya wanamgambo vilivyojumuisha maelfu ya wapiganaji.

Sawa na wanamgambo wengine nchini Libya walipata ufadhili kutoka kwa serkali. Na kuachana na suala la kulipiza kisasi huku ndugu walisalia wakitumia mamlaka yao kikamilifu mjini Tarhuna.

Hanan Abu-Kleish with photograph of one of her missing uncles

Chanzo cha picha, Hanan Abu-Kleish

Maelezo ya picha, Hanan Abu-Kleish akiwa na picha ya mjomba wake aliyepotea

"Sera ilikuwa ni kuwatesa watu kwa lengo la kuwaogopesha. Waliwaua watu kinyama ili kutimiza lengo hilo. Mtu yeyote mjini Tarhuna ambaye aliwapinga alikumbana na mauti," anasema Hamza Dila'ab.

Hanan Abu-Kleish alikuwa nyumbani Aprili 17 mwaka 2017 wakati wanamgambo wa Kani walipowavamia.

"Mmoja wao aliniwekea bunduki kichwani," anasema. "aliniuliza ni nani yuko nyumbani, nikamwambia, ' akuna mtu.' Lakini aliniburuza chini na na kunipeleka chumbani kwa baba yangu. wakamwambia: ' utakuua wewe kwanza.' Na bila lusitanien wakamuua. Nilijaribu kuwazua lakini walimmiminia risasi kifuani."

Ndugu watatu wa kiume wa Hanan pia waliawa siku hiyo pamoja na watoto wao wawili waliyokuwa na umri wa miaka 14 na 16.

Jamaa zake wengine hawajulikani waliko baada ya kutekwa na vikosi vya Kani.

One of the exhumed bodies is buried on 13 November 2020

Chanzo cha picha, AFP

Hanan anasema sababu ya wao kuvamiwa ni kwamba walikuwa jamaa wa familia inayoheshimika mjini Tarhuna.

Kufikia wakati huo ndugu wa Kani walikuwa wamebuni jimbo dogo ndani na nje ya Tarhuna na hata kuongoza polisi waliokuwa na sare.

Waliendesha biashara kubwa kupitia fedha walizopora kupitia "kodi" walizotoza kiwanda cha simiti na wafanya biashara katika eneo hili, majengo ya maduka makubwa miongoni mwa zingine.

The grave excavations seen from above

Chanzo cha picha, AFP

Wajinufausha katokana na ada ya "ulinzi" waliyotoa kwa walanguzi wa dawa za kulevya na wahamiaji waliyopitia eneo hilo kutoka jangwa la Sahara kuelekea pwani ya Mediterranea.

Huku wakijidai kukabiliana na walanguzi na kubuni kisiwa ambacho kinazingatia sheria katika eneo ambalo linakabiliwa na vita nchini Libya.

Mwaka 2017, nudge hao waliandaa onyesho la kijeshi lililojumuisha silaha nzito nzito, polisi ambao hawakuwa wamevalia sare rasmi wakiwa na simba.

Simba hao ni mali ya kibinafsi ya ndugu hao ambao wanadaiwa kulishwa kwa kutumia nyama ya baadhi ya wathiriwa wao.

An olive grove in Tarhuna

Chanzo cha picha, AFP

Kisha mwaka 2019, ndugu wa Kani aliamua kubadili mkondo wao katika vita vya Libya.

Walijitenga na serikali ya GNA, ambayo inadhibiti eneo la magharibi mwa Libya, na kuungana na hasimu mkuu wa serikali, Jenerali Khalifa Haftar, ambaye anadhibiti nusu ya eneo la mashari ya nchi, na hatimaye kumruhusu atumie eneo lao kushambulia tmji mkuu wa Libya, Tripoli.

Mara baada ya hatua hiyo, mji mdogo wa Tarhuna uligeuka kuwa ngome ya vita katika harakati za kimataifa.

Haftar anaungwa mkono na Ufaransa, misri ,Umoja wa Falme za Kiarabu UAE- na Urusi ambayo imewapeleka mamluki kupiga kambi katika mji huo unaodhibitiwa na nudge wa Kanis.

Uturuki inayopinga marengo huo, iliamua kusaidia serikali ya Tripoli kwa silaha.

Na bila shaka huenda ni ndege ya Uturuki isiyokuwa na urbani iliyomuua Mohsen al-Kani na ndugu yake mdogo, Abdul-Adhim,22, mwezi Septemba mwaka 2019.

Mauji yao na kutibuka kwa mpango wa kuteka mji wa Tripoli yalisababisha umwagikaji mkubwa wa damu kuwahi kushuhudiwa Tarhuna.

"Mauaji yalikuwa yakifanywa mara kwamara kwasababu mambo hayakuenda kama yalivyopangwa," nasema Jalel Harchaoui. "Utahakikisha vipi watu wako hawaungani ma maadui wako?

Kwa hivyo familia ya Kani iliendeleza ukatili kwa kiwango kikubwa."

Celebrations in the centre of Tarhuna when Gen Haftar and the Kani brothers were driven out in June 2020

Chanzo cha picha, AFP

Lakini baada ya makabiliano makali wapiganaji wanaounga mkono serikali walifanikiwa kuuteka mji wa Tarhuna mapema mwezi Juni mwaka 2020 na ndugu wanna wa Kani waliosalia na wanamgambo wao walitoroka na vikosi vya Haftar hadi mashariki mwa Libya.

"Tulikuwa na matumaini makubwa, hatulala usiku huo, twatoto walikuwa na furaha," Rabia Jaballah, moja wa wakaazi alisema.

A defaced mural of Mohsen, who served as "minister of defence", at the brothers' detention centre

Chanzo cha picha, AFP

Asubuhi iliyofuata, yeye pamoja na wakazi wengine ambao waume zao au nudge zao walikuwa wametekwa, walikimbilia kituo cha Kani cha kuwazulia wafungwa kuwatafuta.

Lakini walipigwa na butwaa kupata seli ndogo kiasi cha sentimita 70 kwa 70 - zikiwa wazi na hawakumpata mfungwa yeyote.

"Tulivunjika moyo sana," anasema Rabia. "Vyumba hivyo vilikuwa na damu. Sikuweza kujizuia. Nililia kwa machungu."