Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Laila Khalid: Mwanamke jasiri wa Kipalestina aliyeiteka ndege ya Israel na kuielekeza Syria
Siku ya tarehe 29 Agosti,1969 . Mwanamke mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa amevalia suti nyeupe na kofia ya kujikinga na jua pamoja na miwani ya jua alikuwa akisubiri ndege ya TWA 840 katika uwanja wa ndege wa Roma.
Alikuwa mwenye wasiwasi. Kijana wa kike ambaye alikuwa na muonekano wa mchezaji filamu wa Hollywood Audrey Hepburn, alifanikiwa kuingiza silaha ndogo aina ya pistol na guruneti mbili za kurushwa kwa mkono kwa kuwadanganya maafisa wa usalama wa uwanja wa ndege.
Alikuwa akijaribu kuonesha kwamba hakuwa anamtambua mtu yeyote mwingine.
Salim Isavi, alikuwa ameketi kwenye eneo wanalokaa wasafiri katika uwanja wa ndege kusubiria safari zao.
Mwanaume huyu alikuwa mjumbe muhimu wa kikosi cha makomandoo cha Che Guara cha ukombozi wa Wapelestina (the Popular Front for the Liberation of Palestine) na jina la msichana lilikuwa ni Laila Khalid. Laila Khalid alikuwa amefika Roma kwa ndege ya kibinafsi kutoka Beirut.
Laila na mwenza wake Isavi walikuwa wamepanga makusudi kununua viti vyao katika daraja la kwanza ndani ya ndege(first class) ili kuwawezesha kulifikia eneo la rubani kwa urahisi.
Isavi aliniambia kwamba alikuwa akisafiri kuelekea nyumbani kwao Ugiriki kukutana na mama yake baada ya kuishi Marekani kwa takriban miaka 15 . Wakati mmoja nilihisi kumwambia kwamba atoke katika ndege hiyo na kuchukua usafiri mwengine wa ndege , lakini nikajizuia.
Laila Khalid na Isavi walivyofika chumba cha rubani
Viti vya Laila Khalid na Salim Isavi vilikuwa vimekaribiana ndani ya ndege. Mhudumu wa ndege alimpatia Laila Kahawa na akampatia pombe Isavi. Lakini baada ya hilo, Laila Khalid hakula chochote licha ya mhudumu kusisitiza sana ale chakula.
Badala yake alimwambia mhudumu kwamba anahisi kuwa na mafua na maumivu ya tumbo, kwahiyo nipe blanketi ya ziada nijifunike. Mara baada ya kupokea blanketi, Laila aliweka guruneti yake ya mkono na pistol chini ya blanketi ili zisiweze kufikiwa kwa haraka.
Katika mahojiano na Eileen Macdonald, mwandishi wa kitabu cha 'Shoot the Woman First', Laila Khalid anasema, 'wakati mhudumu wa ndege alipoanza kumpatia chakula, Salim aliruka haraka na kuingia ndani ya chuma cha rubani.
Pia nilikimbia nyuma yake na guruneti yangu ya mkononi iliyokuwa kwenye mapaja. Ilianguka kutoka kwenye mikono ya mhudumu wa ndege akapiga mayowe kwa sauti ya juu.
Halafu pisto yangu iliyokua imekwama kiunoni ikaanguka kwenye sakafu ya ndege .Mimi na Isaavi tulipaza sauti na kuwaamrisha wasafiri wote wa daraja la kwanza kuhamia katika daraja la pili.
Layla aliamrusha ndege ipelekwe Israeli
Katika utekeji huu wa ndege, Laila Khalid alipewa jukumu la kuzungumza na rubani na kituo cha uongozaji wa ndege. Laila alimtaka rubani kupeleka ndege hadi kwenye uwanja wa ndege wa Lod ambao kwa sasa unaitwa-David Ben Gurry Airport.
Ilipokuwa ikiingia katika eneo la Israeli, ndege nyingine tatu za kivita za Israeli zilianza kupaa kando ya ndege hiyo. Kutokana na mkanganyiko waliokuwa nao wasafiri kutokana na tukio lililotokea. Walifikiri ndege za Israeli zingeidungua ndege yao.
Laila Khalid aliwasiliana na kituo cha uongozaji wa ndege na akasema kwamba sasa mtatupokea kama ndege ya PFLP Free Arab Palestine, na sio Flight TWA 840. Rubani wa ndege awali alikuwa amekataa kuheshimu agizo lakini wakati Laila alipomuonesha guruneti ya mkono, ilibidi afuate amri.
Ndege iligeuzwa na kupelekwa Damascus
Amri ya kuelekea uwanja wa ndege wa Israeli Lod ilikuwa tu ni kuwadanganya Waisraeli. Ndege ilipita juu ya Lod. Mamia ya wanajeshi wa Israeli na vifaru vyao walikuwa wamesimama chini, tayari kukabiliana nao. Halafu Laila Khalid alimuamuru rubani kuipeleka ndege katika mji wa Damascus Syria
Wakiwa njiani, alimtaka rubani apite juu ya anga la mji wa Haifa, mahala alikozaliwa.
Baadaye Laila Khalid aliandika kuhusu wasifu wa maisha yake, 'wakati nilipoiona Palestina kutoka juu, nilisahau kwa dakika kwamba nilikuwa sehemu ya utekaji. Nia hii ikaibuka akilini mwangu kwamba ninapaswa kupaza sauti niwasalimie bibi yangu ,mashangazi zangu na kila mmoja aliyeko pale kwamba tunarejea nyumbani . Baadaye rubani pia alisema kwamba walikuwa wanapita kwenye anga la Haifa, aliona vinyweleo kwenye ngozi yangu vikisisimka na kusimama.
Ndege ililipuliwa na vilipuzi
Baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Damascus , Salim Isavi aliweka vilipuzi kwenye chumba cha rubani na kuilipua ndege. Kwa mtazamo wake, hii ilikuwa ndio njia bora zaidi ya kupeleka ujumbe wa watu Palestina kwa dunia.
Alifahamu kwamba Israeli haingefanya lolote kumteka nyara na kumuua Laila Khalid, lakini hata wakati huo alikuwa ametumwa kutembelea nchi za kiarabu. Lakini walinzi aliopewa walikuwa wamemzingira. Laila Khalid alikuwa amekuwa shujaa wa kike katika ulimwengu wa Kiarabu.
Upasuaji wa kubadili umbile la uso
Laila Khalid baadaye alifanyiwa upasuaji mara sita wa kubadili pua, mashavu, macho na mdomo wake ili kubadili kabisa muonekano wake na kumuandaa kwa ajili ya utekaji nyara mwingine.
Mwezi Septemba 1970, Laila Khalid alihama kutoka Lebanon kuelekea Ulaya . Tarehe 4 Septemba mjini Stuttgart, Ujerumani, alikutana na Patrick Arugullo, ambaye alimsindikiza katika utekeji unaofuatia. Hawakuwa wamewahi kufahamiana.
Tarehe 6 Septemba, wawili hao pamoja, walisafiri kutoka Stuttgart hadi Amsterdam wakiwa na tiketi ya kuelekea New York.
Arugullo alikuwa ni Mnicaragua aliyezaliwa Marekani. Wakiwa Amsterdam, wote walipanda ndege ya Boeing 707 ya Shirika la ndege la Israeli Airlines chapa ELAI 219 iliyokuwa ikielekea New York.
Sarah Irving aliandika katika kitabu chake 'Laila Khalid's Icon of Palestinian Liberation', ' kwamba wakati wawili hao walipopanda ndege, hawakujua kuwa wangesaidiana katika utekaji , Wahudumu wa ELAI waliwapatia viti, lakini tulivikataa.'
"Ilikuwa imekwisha amriwa kuwa wakati wa utekeji kwamba watu zaidi ya wawili watahitajika kuiteka ndege ya ELAI kwasababu ndege hiyo inakuwa na walinda usalama na wasafiri husakwa mara tatu ." .'
Rubani alifunga chumba cha rubani
Mara hii Laila Khalid na mshirika wake walikuwa wameketi katika daraja la tatu (economy class).
Laila Khalid alisema katika mahojiano na BBC kuwa 'Arugulo alifahamu kile alichotakiwa kufanya na alifahamu kuwa lazima akifanye. Tulikuwa na silaha zetu wenyewe.
Nilikuwa na guruneti mbili za mkononi. Patrick pia alikuwa na guruneti. Nilikuwa nimevaa sketi fupi sana. Nilikuwa nimeficha ramani zote ndani ya sketi ile.
Patrick alilipiza kisasi, ambayo ilimpiga Marshal Shlomo Weider kwenye mguu wake. Wakati huo huo, Patrick pia alipigwa risasi. Khalid alishambuliwa na walinzi wawili na wasafiri. Watu wakaanza kumpiga kiasi kwamba mbavu zake nyingi zilivunjika na akafungwa gerezani.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 77 kwasasa anaishi Amman. Ameolewa na daktari fayaz Rashid Hilal, ambaye amezaa naye Watoto wawili Badr na Bashar.
Ukimtazama , hakuna anayeweza kusema kwamba alikuwa msichana aliyeshiriki katika vita vya ukombozi wa Palestina akiwa ameshikilia bunduki aina ya Ak 47 mkononi.