Nyuklia: Inawezekana dunia ikawa bila silaha hizi hatari zaidi?

Kwa mujibu wa ripoti ya wataalam kutoka Kituo cha Kimataifa cha Uchuguzi na utafiti wa masuala ya Amani, (SIPRI) silaha za nyuklia zimeongeza duniani.

China imetengeneza vinu 30 zaidi vya Nyuklia kulinganisha na mwaka jana. Kwa sasa kuna vinu vya silaha hizo za nyuklia 350. Kwa upande wa Pakistan iliongeza kuongeneza vinu vitano na kufikisha vinu 165 vya silaha za nyuklia.

Nchi ngapi duniani zinamiliki silaha za Nyuklia? Na duniani kuna silaha ngapi ?

Kuna wakati kulikuwa na hofu kuhusu silaha za nyuklia kati ya Marekani na Iran. Silaha hizi zinatajwa ni moja ya silaha hatari na zenye madhara zaidi duniani. Bomu moja tu la Nyuklia linaweza kusambaratisha mji mzima. Silaha hizi zina madhara makubwa pia kwa binadamu.

Ziko nchi nyingi duniani , ikiwemo Iran ambazo haziruhusiwi kumiliki silaha za Nyuklia ingawa nchi zingine zina hizo silaha. Kwanini Ethiopia inapanga kuishambulia Misri kwa silaha za nyuklia?

Mpango gani uliopo wa nyuklia kati ya Urusi na Marekani? Unaweza kujiuliza maswali mengi kuhusu silaha za nyuklia, lakini usijali maswali yako yatapata majibu hapa.

Ukisikia Silaha ya Nyuklia unaelewa nini?

Ni vipulizi vyenye nguvu zaidi. Unaweza kukumbuka jina Atomiki, wakati unasoma sayansi kama uliwahi kusoma huko nyuma, Atomiki ni sehemu tu ya mchakato wa kutengeza mabomu ya nyuklia. Ndio maana mabom,u ya nyuklia wakati mwingine huitwa mabomu ya atomiki

Silaha za nyuklia huundwa na mionzi mingi ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa, madhara ambayo yanaweza kuendelea kuwepo hata baada ya mlipuko kutokea.

Ni mara mbili tu dunia imeshuhudia silaha hizi za nyuklia zikitumika, ilitumika na Japan wakati wa vita ya pili ya dunia. Maelfu ya watu walipoteza maisha, Mionzi ya bomu huko Hiromshima iliendelea kuishi kwa miezi kadhaa na kuendelea kuua watu mpaka kufikia 80,000 . Bomu lingine lilipigwa Nagasaki na kuua watu 70,000

Tangu wakati huo, mabomu ya nyuklia hayajawahi kutumika tena. Nchi tisa sasa duniani zinamiliki silaha za nyuklia, ambazo ni Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa, China, India, Pakistan, Israel na Korea Kaskazini.

Nani anaweza kutengeneza silaha hizi?

Kwa ujumla, yeyote anaweza kutengeneza silaha hizi ili mradi tu awe na ujuzi huo wa kisayansi na uwezo wa kiteknolojia, Lakini linapokuja swala la nchi zinaruhusiwa kutengeneza silaha hizi? jibu lake linaleta ukakasi na historia ndefu yenye utata. Kuna kitu kinaitwa kwa kimombo 'Mutual consent of the nuclear arms control (NPT) - chenye jukumu la kudhibiti usambaji wa silaha za nyuklia duniani.

Tangu mwaka 1970, nchi takribani 191 ikiwemo Marekani, China, Urusi, Uingereza na Ufaransa zilisaini makubaliano kuhusu masuala ya kudhibiti silaha za Nyukila.

Nchi hizi tano, zinaitwa mataifa ya nyuklia ndiyo yanayoruhusiwa kumiliki silaha hizo, kwa sababu walitengeneza na kufanya majaribio silaha hizo kabla ya makubaliano ya NPT kuanza Januari 1, 1967.

Licha ya kwamba nchi hizi zinamiliki silaha za nyukilia kama sehemu ya makubaliano zinapaswa kupunguza uwezo wake na hazipaswi kumiliki wakati wote silaha hizo.

Israel (ambayo haijawahi kukiri wala kukana kumiliki silaha hizo), si India wala Pakistan ni sehemu ya makubaliano hayo, na wala hawajasaini makubaliano hayo.

Korea Kaskazini yenyewe ilijiondoa mwaka 2003.

Vipi kuhusu Iran?

Iran ilizindua mpango wake wa nyuklia katika miaka ya 1950s, na wakati wote imekuwa ikisisitiza kwamba mpango wake wa nyuklia ni salama.

Lakini kuna wasiwasi kwamba inatengeza silaha za nyuklia kwa siri. Kutokana na hilo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani na Umoja wa Ulaya waliiwekea vikwazo nchini hiyo mwaka 2010.

Kutokana na hilo Iran ikakubali kuondoa kinu chake katika makubaliano ya mwaka 2015, lakini Rais wa Marekani wakati huo, Donald Trump akavunja mpango huo mwezi May 2018.

Dunia bila Silaha za nyuklia inawezekana?

Kuondoa silaha za nyuklia dunia ni mpango wa kimataifa. Kitakwimu silaha za nyuklia zimepungua kutoka 70,0000 mwaka 1986 mpaka 14,000 kwa sasa.

Marekani, Uingereza na Urusi zote zimepunguza silaha zake za nyuklia lakini China, Pakistan, India na Korea Kaskazini zinatajwa kwamba zinaendelea kutengeneza mabomu zaidi kulingana na taarifa za wanasayansi wa Marekani.

Julai 2017, nchi zaidi ya 100 zilisaini azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu kusambaratisha silaha hizo na kupiga marufuku uzalishaji na umiliki wa silaha hizo. Lakini Marekani, Uingereza, Ufaransa na Urusi zikazuia utekelezaji wake. Uingereza na Marekani zikasema azimio hilo halimaanishi kuihakikishia dunia usalama, ila silaha hizo zimekuwa kama nyenzo muhimu kuhakikisha dunia imekuwa salama kwa miaka zaidi ya 70.

Wakati Uingereza inaendelea kuboresha silaha zake za nyuklia , Marekani inatarajia kutumia dola 1 trillion , kuongeza uwezo wake wa kinyuklia kufikia mwaka 2040.

Korea Kaskazini yenyewe inaendelea na majaribio ya mabomu yake ya nyuklia, na imefanya hivyo hivi karibuni.

Ingawa mabomu hayo ya nyuklia yanapungua dunaini ukilinganisha na miaka 30 iliyopita, lakini haionekani kwamba silaha hizi hazitakuwepo ama zitaangamizwa katika siku za hizi karibuni.