Unataka kwenda anga za mbali? naul ni hii…

Richard Branson

Chanzo cha picha, VIRGIN GALACTIC

Kampuni ya Virgin Galactic imefungua tena mauzo ya tiketi kwa safari zake za anga za mbali kwa bei ya kuanzia $ 450,000 kwa kiti.

Inakuja baada ya kampuni hiyo, ikiongozwa na bilionea Richard Branson, kukamilisha safari yake ya kwanza ya kwenda anga za mbali mwezi Julai.

Kampuni hiyo inatarajia kuanza safari za kibiashara mwaka ujao baada ya kumaliza safari kadhaa za majaribio.

Hapo awali ilikuwa imeuza tiketi kwa $ 250,000 kila moja lakini ilisimamisha mchakato huo mnamo mwak 2014 baada ya ajali mbaya.

Katika taarifa, Michael Colglazier alisemaufanikiwa la jaribio la mwezi uliopita limeongeza tena hamu ya umma kwa ofa ya kampuni hiyo.

"Kwa kuzingatia kuongezeka kwa maslahi ya watumiaji kufuatia ndege ya Unity 22, tunayo furaha kutangaza kufunguliwa tena kwa mauzo leo," alisema.

"Tunapojitahidi kuleta maajabu ya anga za mbali kwa sehemu kubwa ya ulimwengu, tunafurahi kufungua mlango wa tasnia mpya na uzoefu wa watumiaji."

Virgin Galactic kwa sasa inashindana na Blue Orogin, inayoendeshwa na Jeff Bezos wa Amazon, na Space X, inayomilikiwa na Elon Musk, kukuza soko la utalii wa anga za mbali.

Siku chache baada ya safari mwezi Julai, Bwana Bezos alishiriki katika safari ya kwanza ya majaribio ya ndege yake mwenyewe angani.

Bezos anatarajjiwa kuuza tiketi za safari za baadae za Blue Origin kati ya $200,000 and $300,000.

Kwa upande wa Space X mwaka jana ilifanikiwa katika safari yake ya majaribio ikiwa na marubani wake wa ndege ya aina ya Dragon kufika katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Mbali (ISS).

Chini ya ushirikiano na Nasa, wanapanga kupeleka wanaanga ISS siku za usoni. Pia kampuni hiyo inapanga kupeleka watalii watatu katika kituo hicho katika safari ya jumla ya siku 10 baadae mwaka huu.

Kampuni ya Virgin inasema watalii katika siku za usoni watakuwa na machaguo ya kununua aidha tiketi moja mojja ama kununua tiketi za firushi na kusafiri kama marafiki na familia au kukodi ndege nzima.

Wale ambao wametia nia ya kusafiri wanatakiwa kwanza kuweka oda ya tiketi hizo. Tiketi takribani 600 zilishauzwa awali kabla ya kusitisha mauzo.

Safari inayofuata ya kampuni hiyo kuelekea safari za mbali kwa kutumia ndege iitwayo, Unity 23, inatarajiwa kuwa mwishoni mwa mwezi wa Septemba ikianzia kituo kiitwacho Spaceport America kilichopo jimboni New Mexico, Marekani.