Kajal aliolewa mwaka jana ,hivi sasa mwili wake umepatikana vipande vipande

Chanzo cha picha, Familia ya Kajal
Mtoto wa kike wa Manju aliyekuwa mjamzito alidaiwa kuuawa kutokana na suala la mahari kutoka kwa familia ya muwe wake.
Inadaiwa kwamba baada ya mauaji hayo , mwili wake ulikatwa vipande vipande na baadaye kuuchomwa moto.
Familia ya Kajal inadai kwamba mwili wake ulipatikana katika uwanja ulio karibu na nyumbani kwao na ulikuwa katika hali mbaya ,na vipande hivyo vilikusanywa na kutiwa katika mifuko.
Na sasa kuna kesi mahakamani iliowasilishwa tarehe 20 Julai lakini polisi hawajamkamata hata mshukiwa mmoja.

Chanzo cha picha, VISHNU NARAYAN/BBC
Je kuna tatizo gani?
Kajal, mkazi wa Kijiji cha Bihta katika wilaya ya Bakhtiyarpur huko Patna aliolewa na Sanjeet Kumar kutoka Kijiji cha Nonia Bigha huko Nalanda mwaka uliopita. Sanjeet anafanya kazi katika shirika la reli katika eneo la Bengaluru.
Familia ya Kajal inasema kwamba ilitoa vito vya thamani, pikipiki na mahari ya Rupia 12 wakati wa ndoa yao , lakini mwaka mmoja baadaye , na baada ya mwanamke huyo kupandishwa ngazi kazini Rupia zengine laki sita zilihitajika na mume wake.
Familia ya Kajal ilisema kwamba katika malalmishi yao kwamba mvulana huyo alipanda ngazi kazini na hivyobasi alikuwa anataka kuongezewa mahari.
Msichana alikuwa hapo awali amelalamikia unyanyasaji kutoka kwa familia yake.

Chanzo cha picha, KAJAL'S FAMILY
Kulingana na Manju Devil, mara ya mwisho walipozungumza na msichana wake katika simu ilikuwa Julai17.
"Alisema kwamba wanaogopa', aliambia BBC.
Baadaye saa tatu simu yake ilizima .

Chanzo cha picha, VISHNU NARAYAN/BBC
Watu wa familia hiyo walianza kumsaka Kajal baada ya kupoteza mawasiliano naye.
Anadai kwamba baadhi ya wanavijiji walimtaka kumtafuta maeneo yalio karibu.
Baadaye watu hao wa familia wakishirikiana na maafisa wa polisi walifanikiwa kui pata maiti iliokatwa vipande vipande katika maeneo yaliopo mita 500 kutoka barabarani.
Familia hiyo ilidai kwamba mbele ya maafisa hao wa polisi waliweka vipande hivyo ndani ya mfuko.
Babake Kajal Arvind Kumar aliambia BBC , kwamba mwanawe alipotea asubuhi ya tarehe 17 na kupatikana tarehe 21 siku nne baadaye akiwa amechomwa hadi kufa.
Mikono na miguu yake pia ilikatwa hivyobasi wakavitia vipande hivyo katika mfuko huo.
''Kulikuwa na maafisa wa polisi lakini hawakugusa vipande hivyo vya mwili, ni kazi yao lakini tungefanyaje''?
Wanasema kwamba washukiwa bado walikuwa katika Kijiji hicho hadi siku moja kabla ya mwili huo kupatikana.
''Alama za mbao zilizochomeka moto pamoja na nyasi zilipatikana sio mbali na pale ambapo vipande vya mwili huo vilipatikana''.
Majani ya miti iliokuwepo katika eneo hilo pia yalichomeka moto.

Chanzo cha picha, VISHNU NARAYAN/BBC
Kesi ya mauaji iliwasilishwa mahakamani
Polisi waliwasilisha mahakamani kesi hiyo Julai 20. Ni siku hiohio ambapo vipande vya mwili huo vilitumwa kwa uchunguzi zaidi mbali na kufanyiwa uchunguzi wa DNA.
Hatahivyo família hiyo inasubiri ripoti hiyo.
Polisi walipeana vipande vya mwili huo kwa familia ya Kajal ambayo baadaye iliuchoma tarehe 23 Julai kandokando yam to Ganga huko Patna.
Watu saba wametajwa kuhusiana na mauaji hayo.
Mume, ndugu ya mume, madada zake wawili na wanaume zao.
Maafisa wa polisi wanasema kwamba hawajathibitisha iwapo kesi hiyo itakuwa ya mauaji au iwapo mwili huo ulikatwakatwa na kuchomwa, lakini kuna ushahidi wa kutosha kwamba kifo hicho kilisababishwa na mateso.
Hakuna aliyekamatwa hadi wakati BBC India ilipokuwa ikisandika habari hii.

Chanzo cha picha, VISHNU NARAYA/BBC
Nyumba ya washukiwa na majirani wasiojulikana
Nyumba ya mshukiwa ipo mita 500 kutoka mahali ambapo mwili huo ulipatikana. Kuna nyumba kutoka pande zote mbili katika barabara hiyo, ni eneo lililo na idadi kubwa ya watu , lakini majirani hawana habari zozote kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea.
Baadhi ya wanawake waliohojiwa walisema kwamba uhusiano wao na jirani zao ulikuwa mdogo.
Hatahivyo, pia alisema kwamba hawakusikia kelele zozote zilizotokana na vita katika nyumba hiyo.












