Wafahamu wafungwa 5 wanaohudumia vifungo vya muda mrefu zaidi duniani

Jel nchini El Salvador

Chanzo cha picha, TARIQ ZAIDI

Maelezo ya picha, Wafungwa nchini El Salvador

Hawa ndio wafungwa watano wanaohudumia vifungo vya muda mrefu zaidi kote duniani. Wafungwa hawa kutoka Marekani na Ujerumani wanahudumia zaidi ya miaka 57 jela ikiwa ni sawa na vifungo vya maisha.

1.Francis Clifford Smith

Ni miongoni mwa wafungwa wanaohudumia kifungo cha muda mrefu zaidi huko Connecticut. Alihukumiwa kifo kwa mauaji ya mlinzi wa usiku wakati wa ujambazi uliofanyika katika klabu moja ya burudani mwezi Julai 1949. Kifungo chake kilibadilishwa na kuwa cha maisha mwaka 1954, saa mbili tu kabla ya kunyongwa. Kwa sasa anahudumia kifungo cha miaka 71 na siku 49. Mzee huyo anayedaiwa kuwa mfungwa mwenye kifungo kirefu zaidi nchini Marekani alifungwa katika jela ya Taasisi ya Osborn lakini baadaye akahamishwa hadi katika nyumba moja ya wazee 2020. Alianza kuhudumia kifungo chake tarehe 7 mwezi Juni 1950.

Wafungwa

Chanzo cha picha, Getty Images

2.Booker T Hillary

Ndiye mfungwa aliyehudumu kifungo cha miaka mingi zaidi gaerezani katika jimbo la Carlifornia nchini Marekani. Booker T alipatikana na hatia ya mauaji lakini hukumu yake ikabadilishwa hadi kifungo cha maisha 1970. Kesi yake ilipelekwa katika mahakama ya rufaa lakini akapatikana na makosa mara ya pili 1986. Hukumu yake ilianza kutekelezwa mwaka 1962 na anahudumia kifungo cha miaka 58 na siku 267.

3.Hans-Georg Neumann

Alipatikana na hatia yay a utekaji nyara na kuwauwa wanandoa wawili katika barabara ya lovers Lane. Ndiye raia wa Ujerumani anayehudumia kifungo cha muda mrefu zaidi nchini Ujerumani na Ulaya kwa ujumla. Mnamo tarehe 17 mwezi Machi 2021 mahakama ya Ujerumani iliagiza kuachiliwa kwake katika siku isiojulikana kabla ya maandalizi ya kumrudisha katika jamii kuanza mara moja. Bwana Hans George ambaye anahudumia kifungo cha maisha jela cha miaka 58 na siku 57 alianza kuhudumia kifungo hicho mwaka 1963 .

Jela nchini El-Salvador

Chanzo cha picha, TARIQ ZAIDI

Maelezo ya picha, Jela nchini El-Salvador

4.Henry Montgomery

Alipatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumuua afisa wa polisi nchini Marekani katika eneo la East Baton Rouge, mjini Louisiana akiwa na umri wa miaka 17. Alihukumiwa kifo 1966 lakini Mahakama ya kilele ya Lousiana ikafutilia mbali uamuzi huo baada ya kubaini kwamba hakupata haki wakati wa kesi hiyo kutokana na chuki ya umma dhidi yake .Mwaka 1969, alipatikana na hatia ya mauaji hatua iliolazimu kupatiwa kifungo cha maisha gerezani bila kuachiliwa. Mwaka 2016 hukumu yake ya maisha jela iliondolewa ili ahukumiwe upya. Alinyimwa msamaha mara mbili. Anaendelea kuhudumia kifungo cha miaka 57 na siku 296 tangia mwaka 1963 ambapo hukumu hiyo ilianza kutekelezwa.

Wafungwa nchini El Salvador

Chanzo cha picha, TARIQ ZAIDI

James R. Moore

Alikiri kuhusika na ubakaji na mauaji ya msichana mwenye umri wa miaka 14 ili kukwepa hukumu ya kifo na hivyobasi kupatiwa kifungo cha maisha jela. Pia alikiri kuwanyanyasa kingono makumi ya wasichana wengine . Alinyimwa msamaha alipowasilisha ombi hilo 2019. Kwa sasa anahudumia kifungo cha miaka 57 na siku 231 alichoanza kutekeleza mwaka 1963.