Tokyo Olympiki: Ushindi wa dhahabu wa muogeleaji wa Tunisia Hafnaoui wawashangaza wengi kwa kushinda medali ya dhahabu

Muogeleaji wa Tunisia Ahmed Hafnaoui amewashangaza wengi kwa kupata medali ya dhahabu katika mchuano wa mita 400 wanaume siku ya Jumapili. Ahmed Hafnaoui mwenye umri wa miaka 18-alishinda fainali hiyo licha ya kufuzu kwa kasi ya chini, lakini alimaliza kwa kasi ya juu na kumshinda Muaustralia Jack McLoughlin ambaye alikuwa akipigiwa upatu."Siwezi kuamini. Ni ndoto na imekuwa kweli. Ilikua ni vizuri sana, zilikuwa ni mbio zangu bora kuwahi kushuhudiwa ," alisema Hafnaoui.Ilikuwa ni dhahabu ya tano ya Tunisia ya - na ni ya tatu katika uogeleaji. Hii ni medali ya kwanza ya dhahabu kwa Afrika katika michuano ya Olimpiki inayoendelea Japani. Muogeleaji wa Marekani Kieran Smith alipata medalist ya shaba katika Tokyo Aquatics Centre.Hafnaoui, mtoto wa kiume wa mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu Mohamed Hafnaoui, alishiriki katika mashindano ya Olympiki ya vijana 2018, akamaliza akiwa wa nane katika mita 400 na wa saba katika mita 800.

Mwaka 2019, aliliambia gazeti la Tunisia, La Presse, kuwa alikuwa analenga kushinda medali yake ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya Olympiki 2024 itakayofanyika jijini Paris.

Wenyeji Japani pia wamesherehekea medali ya dhahabu ya kushiriki za katika mchuano wa kuogelea wa mita 400 kwa upande wa wanawake baada ya Yui Ohashi kuwashinda waogeleaji wawili Wamarekani ambao walitarajiwa kushinda. "Nahisi si kama jambo halisi. Ni kama ndoto kwangu," alisema Yui Ohashi mwenye umri wa miaka 25. "Sikuweza kwenda katika Olimpiki Rio, kwahiyo kwa miaka mitano iliyopita hii ilikuwa ndoto kubwa kwangu. Mafanikio haya ni ya kufurahisha."