Betri na data ya simu yako vinakwisha haraka, ni ishara ya udukuzi?

Je! betri ya simu yako huisha haraka? Je! simu inaishiwa data haraka?

Ikiwa umeanza kutumia simu sana, basi inaweza kuwa wakati wa kubadilisha mpango wako wa data.vinginevyo, basi inawezekana kuwa mdukuzi anachezea simu yako.

Kuchezea usalama wa simu yako kunaweza kusababisha kuvuja kwa utambulisho wako na data zako binafsi.

Katika enzi ya sasa, njia za utapeli wa simu zinabadilika na sasa imekuwa ngumu kuwapata wadukuzi.

Ni kwa namna gani utagundua kuwa simu yako imedukuliwa?

Kama tulivyokuambia mapema kuwa ikiwa simu yako inatumia data nyingi basi inaweza kuwa ishara ya udukuzi.

Kwa mujibu wa kampuni ya usalama ya kompyuta ya Norton ya Amerika, "Kunaweza kuwa na sababu nyingi za kutumia data zaidi, kama vile matumizi ya simu ya kupindukia. Lakini ikiwa unatumia simu yako kwa kawaida kama awali lakini data inakwisha kwa kasi basi unapaswa kuhitaji kuchunguza. "

Kulingana na Norton, betri inagharimu kiasi gani? Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwenye hili. Ikiwa njia unayotumia simu yako haijabadilika, lakini betri inaisha haraka, huenda simu yako ilidukuliwa.

Kwa mujibu wa Kaspersky, kampuni nyingine ya usalama wa kompyuta, "Nguvu zote za usindikaji katika simu iliyoshambuliwa iko mikononi mwa wadukuzi. Kwa hivyo simu yako inaweza kufanya kazi polepole. Inawezekana kwamba wakati mwingine simu inaweza kuacha kufanya kazi au ghafla Ikazima na kuwaka tena."

Wote Kaspersky na Norton wanasema kwamba unapaswa kuendelea kufuatilia simu yako.

Kunaweza kuwa na programu kwenye simu ambayo haujaiweka au kunaweza kuwa na kumbukumbu ya namba ya simu ambayo hukumbuki kama ulifanya mawasiliano nayo. Kulingana na Kaspersky, fuatilia kwenye barua pepe zako na akaunti za mitandao ya kijamii kama haupati arifa zinazohusiana na mabadiliko ya nenosiri ya mara kwa mara au arifa ya maeneo tofauti, ambayo haujawahi kwenda.

Namna ya kuiweka simu yako katika hali ya usalama

Simu yako inaweza kudukuliwa kwa njia nyingi. Unapaswa kuwa mwangalifu wakati unapakua programu, nyingine zinaweza kuwa na virusi. Kawaida unapaswa kupakua programu kutoka kwa Google au duka la Apple yenyewe.

Kulingana na Norton, "Ukipokea barua pepe au ujumbe kutoka kwa mtu usiyemjua, usibofye popote katika ujumbe huo, vinaweza kuwa na programu za udukuzi."

Kampuni ya usalama ya kompyuta McCafe inasema "Ni rahisi kwa wadukuzi kudukua simu yako kwa msaada wa Bluetooth na Wi-Fi. Kwa hivyo zizime unapokuwa huzitumii."

Kulingana na Kaspersky, ni muhimu kila wakati uwe sambamba na simu yako, usihifadhi neno siri kwenye kifaa chako, na uendelee kuboresha programu kila wakati.

Licha ya kuchukua tahadhari, mara nyingi kuna hatari ya kudukua simu. Katika hali kama hiyo, kulingana na Norton, kuwa wa kwanza kuwaambia watu ambao nambari zao zimehifadhiwa kwenye simu kuwa simu yako ilidukuliwa na kuwatahadharisha wasibonyeze tovuti yoyote iliyotumwa kutoka kwenye namba yako.

Kisha, ondoa programu zozote unazofikiria zilimsaidia mdukuzi. Inashauriwa pia kuweka programu ya kupambana na virusi kwenye simu ili iweze kugundua virusi kwa wakati na kukujulisha uwepo. Kupakua tena simu pia ni suluhisho lakini kuna hatari ya kupoteza data pia.

Na mwisho ni muhimu ubadilishe nywila zote. Katika tukio la kushambuliwa kwa simu, kuna hatari ya nenosiri kuvujishwa.