Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kidimbwi cha kuogelea kilicho 'angani' kinachozua utata miongoni mwa wakaazi
Mita 35 kutoka ardhini kuna kidimbwi cha kuogelea kilichotengenezwa angani ambapo unaweza kumuona anayeogelea kutoka pande zote - ikimaanisha kutoka juu, kutoka chini na upande upande.
Kidimbwi hiki kinajulikana kama Sky Pool .
Kikiwa ndicho cha kwanza kutengenezwa angani duniani, kidimbwi hicho chenye urefu wa mita 15 kinashikiliwa na majumba mawili marefu - ijapokuwa kwa ujumla kina urefu wa mita 25.
Ni mojawapo ya miujiza ya usanifu mjini London, iliofunguliwa mwezi Januari na ambayo wakaazi walifanikiwa kujivunia na jua lililokuwa likiangaza katika siku ya kwanza ya majira ya joto. Ijapokuwa sio wote waliweza kuogelea.
Kidimbwi hicho cha kuogelea hakitumiki na wale wanaoishi katika majumba hayo mawili pekee.
Ukitazama kutoka juu kiinaweza kukusababishia kisunzi, lakini watumiaji wake hawana tatizo kuangalia chini.
Pengine ni kwasababu chini ya kidimbwi hicho ni glasi yenye uzito wa sentimita 35.
Kidimbwi hicho kimezungukwa na chuma kinachoweza kuhimili upepo mkali wa London , na lita 148,000 za maji zinazotumika kukijaza.
Wakosoaji
Kidimbwi hicho cha kibinafsi ambacho kinaweza kutumika na baadhi ya wakaazi wa majumba hayo marefu kimezua ukosoaji.
Nyumba zilizojengwa kando ya kidimbwi hicho zinagharimu US $ 2.2 million iwapo unataka kutumia eneo la mazoezi, ukumbi wa sinema , kidimbwi cha kuogelea, kituo cha kibiashara, migawa ama ofisa ya posta.
Vilevile unaweza kukodisha kwa kati ya $ 2,500 hadi $ 9,000 kwa mwezi.
Hatahivyo, baadhi ya wakaazi walipata nyumba zao kupitia mfumo wa ufadhili unaojulikana kama umiliki wa ushirikiano, ambapo hununua asilimia 25 ya nyumba mpya na kulipa kodi kwa gharama iliosalia.
Na hawawezi kufurahia faida sawa.