Jimbo la Carolina Kusini lawapa wanaume wawili chaguo la kuamua wanavyotaka kufa

Chanzo cha picha, SOUTH CAROLINA DEPARTMENT OF CORRECTIONS
Mahakama kuu katika jimbo la South Carolina nchini Marekani imezuia hukumu mbili za mauaji hadi wafungwa watakapopewa machaguo ya kufa kwa kutumia umeme au kwa kikosi cha kuua kwa risasi.
Sheria hiyo mpya inahitaji wafungwa wanaokabiliwa na hukumu ya kifo kuamua kati ya njia hizo mbili wangependelea gani ikiwa njia ya kuuawa kwa dawa za kuua haipo.
Lakini kwasababu mamlaka ya magereza bado haijaunda kikosi chake cha kuua kwa risasi, hukumu hizo za mauaji zimesitishwa na mahakama ya juu zaidi.
Wafungwa Brad Sigmon na Freddie Owens walitakiwa kuuawa mwezi huu.
Wafungwa hao wa makosa ya mauaji walinyimwa ombi la kudungwa sindano za sumu - changuo walilokuwa wanalipendelea kwasababu mamlaka ya gereza haikuwa na dawa zinazohitajika.

Chanzo cha picha, Getty Images
Upungufu wa dawa hizo umesababisha kusistishwa kwa njia hiyo ya hukumu ya mauaji kwa kipindi cha miaka 10 katika jimbo hilo.
Sheria mpya ambayo ilianza kutekelezwa mwezi jana, ilianzishwa kuziba pengo ambalo lilikuwa linaruhusu wafungwa kuahirisha hukumu ya mauaji dhidi yao milele ikiwa dawa hizo hazipatikani.
Kwasababu hakuna kikosi cha kuua kwa kutumia risasi, njia pekee ya kutekeleza hukumu ya mauaji iliyosalia jimboni humo ni kupitia njia ya kuuawa kwa umeme.
Lakini mawakili wa Sigmon na Owens walipinga utumiaji wa njia hio mahakamani, wakidai kwamba wateja wao wana haki ya kuchagua kutaka kuuawa kwa njia ya kudungwa sindano.
Ombi la kupinga hukumu hiyo liliwasilishwa katika mahakama ya juu zaidi iliyopo Carolina kuzuia utekelezaji wa hukumu ya kifo dhidi ya wateja wao hadi rufaa zao zitakaposikilizwa.
Jumatano, mahakama ilitoa uamuzi uliopedelea wafungwa ikisema kuwa hawakupewa machaguo ya "kuamua namna ya wao kunyongwa".
Mahakama ilisema kwamba hakumu za mauaji zaidi zisitolewe tena hadi "itifaki na sera zitakapoimarishwa kutekeleza hukumu ya mauaji kwa kupigwa risasi".
Hakuna njia nyingine
Kufuatia jibu la agizo la mahakama, mamlaka ya gereza kwenye jimbo hilo ilisema kuwa "inasonga mbele na utengenezaji wa sera na michakato ya kutekelezwa kwa hukumu ya mauaji kwa njia ya kupigwa risasi".
"Tunafuatilia majimbo mengine kwa ajili ya miongozo kupitia mchakato huu. Tutafahamisha mahakama pale chaguo la kufa kwa kupigwa risasi litakapokuwepo," Idara ya kurekebisha tabia ya South Carolina imesema.

Chanzo cha picha, Getty Images
South Carolina ni moja ya majimbo manne ambayo yanaruhusu hukumu ya mauaji kwa kupigwa risasi. Oklahoma, Mississippi na Utah pia nayo yanaruhusu njia hiyo.
Sigmon, 63, alikuwa amepangiwa kunyongwa Ijumaa. Amekuwa katika akikabiliwa na hukumu ya kifo kwa karibu miongo miwili tangu alipohukumiwa mwaka 2002 kwa makosa ya kuwaua wazazi wa aliyekuwa mchumba wake kwa fimbo za kuchezea mchezo wa besiboli.
Hukumu ya mauaji dhidi ya Owens ilikuwa imepangwa kutekelezwa Juni 25. Mwanamume huyo, 43, amekuwa kwenye sintofahamu hiyo tangu mwaka 1999, alipohukumiwa kwa makosa ya kumuua mfanyakazi wa dukani wakati wa wizi wa mabavu.













